Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Saturday, December 7, 2013

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL ASAINI KITABU CHA MAOMBOLEZO YA KIFO CHA MZEE MANDERA


 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisaini kitabu cha maombolezo ya kifo cha Rais wa zamani wa Afrika ya Kusini, Nelson Mandera, aliyefariki usiku wa kuamkia leo wakati alipofika kwenye Ofisi za Ubalozi wa Afrika ya Kusini zilizopo Masaki  jijini Dar es salaam leo. Mzee Nelson Mandela (95) alifariki Dunia jana usiku nyumbani kwake Houghton, Jouhannesburg. Kushoto ni Balozi wa Afrika ya Kusini Nchini, Henry Thanduyise Chilize.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitoa heshima za mwisho mbele ya picha ya marehemu Nelson Mandera baada ya kusaini kitabu cha maombolezo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Balozi wa Afrika ya Kusini Nchini Tanzania, Henry Thanduyise Chiliza (kulia) na baadhi ya Viongozi wa Ubalozi huo kwenye ofisi za Ubalozi wa Afrika ya kusini Masaki jijini Dar es salaam leo, baada ya kusaini kitabu cha maombolezo.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...