


Na Miza Kona Maelezo Zanzibar
Vijana wametakiwa kushikamana na kujikuza kwenye ukweli ili wapate kuongoka katika maisha yao ya dunia na akhera .
Hayo yameelezwa leo na Naibu Kadhi Mkuu Shekhe Hassan Othman Ngwali wakati alipokuwa akifungua madrasa Amir ya Bweleo.
Amesema
kuwa ukweli na uaminifu ndio unaomkuza mja kuongoka katika misngi
iliyomema na kuachana na tabia mbaya inapelekea kujiingiza katika
vikundi viovu.
Aidha
amesema vijana wakijitahidi kujifunza katika misingi ya dini na
kishirikiana katika ukweli na uaminifu na kuyafanyia kazi wataweza
kuepukana na vishawishi vibaya na kuogopa kufanya maovu.
Aidha amewasitiza vijana kusoma kwa bidii na kuacha kufanya mchezo katika kutafuta elimu ili wasije kuijutia baabae.
Hata hivyo amewataka vijana hao kufufuata mwenendo wa Mtume SAW ili kuweza kuendeleza mbele dini ya kiislam.
Aidha
amewahimiza wazazi kuwakuza watoto wao katika misingi ya kiislamu kwa
kuitafuta elimu hiyo kwani vijana ndio taifa la kesho na kupata viongzi
wazuri wa baadae.
Aidha
ameuomba uongozi wa madrasa hiyo kuwa na umoja, imani na kujiepusha
na makundi kwa kuwa na maamuzi ya pamoja ili ipate kuendelea vizuri na
kuongeza watoto wenye misingi ya dini na imani.
Zaidi ya shilingi milioni 20 zimetumika hadi kukamilika ujenzi wa madrasa hiyo ambayo yenye madarasa manne.
No comments:
Post a Comment