Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, December 4, 2013

Mnadhimu wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Tundu Lissu: Kambi ya Rasmi ya Upinzani Bungeni, itafanya mabadiliko makubwa katika Baraza lake Kivuli wakati wa Mkutano Mkuu wa 14 wa Bunge unaoanza leo mjini Dodoma.
Mnadhimu wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Tundu Lissu
-----
Kambi ya Rasmi ya Upinzani Bungeni, itafanya mabadiliko makubwa katika Baraza lake Kivuli wakati wa Mkutano Mkuu wa 14 wa Bunge unaoanza leo mjini Dodoma.

Panga pangua hiyo ambayo imesukumwa na kuvuliwa nyadhifa zote kwa aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chadema na Naibu Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Zitto Kabwe itawalenga pia mawaziri vivuli walioshindwa kutimiza majukumu yao kikamilifu.
Habari zilizopatikana jana mjini Dodoma zilisema Zitto ni mlengwa mkuu wa mabadiliko hayo ikiwa ni utekelezaji wa maazimio ya Kamati Kuu (CC) ya chama chake.
Kamati Kuu chini ya Mwenyekiti wake, Freeman Mbowe iliagiza kuvuliwa nyadhifa zote, Zitto pamoja na Mjumbe wa Kamati Kuu, Dk Kitilla Mkumbo kwa kile kilichodaiwa ni kukisaliti chama.Kwa habari zaid

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...