Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Tuesday, December 17, 2013

Ujangili wapungua hifadhi ya Saadani



Mhifadhi wa Hifadhi ya Taifa Saadani, Ismail Omar, akizungumza na waandishi wa habari wa Chama cha Habari za Sayansi Tanzania (TASJA), wakati walipotembelea hifadhi hiyo, mkoani Pwani, wakiwa katika ziara ya kujifunza kuhusu mazingira na viumbe hai.

Na Mwandishi Wetu, TASJA.

VITENDO vya ujangili katika Hifadhi ya Taifa ya Saadani iliyopo wilaya ya Bagamoyo Mkoani Pwani vimeendelea kupungua siku hadi siku kutokana na ushirikiano uliopo baina ya wananchi wa kijiji wa Kijiji cha Saadan.

Kauli hiyo imetolewa na Mhifadhi ya hifadhi hiyo idara ya ulinzi Ismail Omary alipokuwa akitoa taarifa kwa wanachama wa Chama cha waandishi wa habari za sayansi(TASJA) waliotembelea hifadhi hiyo kujifunza masuala mbalimbali.

Alisema ikilinganishwa na kipindi cha nyuma, kwa sasa vitendo vya ujangili hifadhini hapo ikiwemo ya uharibifu wa misitu na uwindaji haramu wa wanyama, vimepungua kwa kiasi kikubwa kutokana na wananchi kutambua umuhimu wa hifadhi hiyo yenye ukubwa wa kilomita za mraba 1100.

Katika ziara hiyo ya mafunzo iliyowezeshwa na Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa(UNESCO)waandishi hao walijifunza masuala mbalimbali yanayohusiana na umuhimu wa hifadhi za Taifa, kuzitunza na kuziendeleza.


Kutokana na kufanisha mafunzo hayo Mwenyekiti wa TASJA Greyson Mutembei, aliishukuru UNESCO kwa niaba ya wananchi kwa kuhakikisha wanajenga wigo mpana kwa wanahabari kuhusu taarifa za mazingira hasa za wanyama na vioumbe hai.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...