Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Monday, March 31, 2014

SUPER D AMPIKA JUMA BIGLEE KUPAMBANA APRIL 15 CHALINZE



Kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' kulia akimwelekeza jinsi ya kutupa makonde bondia Juma Biglee wakati wa mazoezi yanayoendelea katika kambi ya Ilala amana CCM Dar es salaam jana Biglee anajiandaa na mpambano wake april 15 Chalinzo mkoa wa pwani picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' kulia akimwelekeza jinsi ya kutupa makonde bondia Juma Biglee wakati wa mazoezi yanayoendelea katika kambi ya Ilala amana CCM Dar es salaam jana picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' kulia akimwelekeza jinsi ya kutupa makonde bondia Juma Biglee wakati wa mazoezi yanayoendelea katika kambi ya Ilala amana CCM Dar es salaam jana Biglee anajiandaa na mpambano wake april 15 Chalinzo mkoa wa pwani picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

WINDHOEK AMBAO NI WADHAMINI WAKUU WA SHEREHE YA KUTIMIZA MIAKA 3 YA BONGO MOVIE


 Mwenyekiti wa Bongo Movie, Steve Mengele (Nyerere) akihojiwa na waandishi wa habari wakati wa sherehe ya Kutimiza miaka 3 ya Klabu ya Bongo Movie, sherehe iliyofanyika katika Ukumbi wa East 24 uliopo Katika Jengo la Arcade Mikocheni, Mwishoni mwa Wiki
Warembo wakiwa wamebeba Chupa za Windhoek zinazosambazwa na kuuzwa na Kampuni ya Mabibo Beer ambao ndio walikuwa wadhamini wakuu wa Sherehe ya Kutimiza Miaka 3 ya Klabu ya Bongo inayoongozwa na Steve Nyerere.
Mwenyekiti wa Makampuni yaliyo chini ya Proin Group Of Companies, Bw Johnson Lukaza akipokea cheti cha kuthaminiwa kutoka kwa Mwenyekiti wa Bongo Movie kama mmoja wa wamiliki wa kampuni ya usambazaji wa kazi za filamu nchini  iitwayo Proin Promotions Limited.
 Burudani pia zilikuwepo
 Mkurugenzi wa Kampuni ya Mabibo Beer, Mama Benadetha Rugemalila akiongea na waandishi wa habari wakati wa sherehe hiyo iliyofanyika mwishoni mwa wiki katika Ukumbi wa East 24 uliopo Mikocheni katika jengo la Arcade.
 First lady wa B Band inayoongozwa na Baba Zoro
 Wadau wakifuatilia burudani safi kutoka kwa wasanii mbalimbali waliopanda kwenye jukwaa
 Warembo wa Bongo Movie wakiingia ukumbi tayari kwa Kufurahia Miaka 3 ya Kuzaliwa kwa Bongo Movie.
 Nuruel akiendelea kuimba kwa hisia katika sherehe hiyo iliyofanyika mwishoni mwa wiki
 Mwenyekiti wa Bongo Movie akitoa maneno kwa wageni waalikwa pamoja na wasanii wa bongo movie na muziki nchini waliohudhuria sherehe hiyo iliyofanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa East 24.
 Keki ikikatwa kama ishara ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Bongo Movie ikiwa imetimiza miaka 3
 Rich Rich akilishwa keki na Mwenyekiti
 Mwenyekiti wa Makampuni yaliyochini ya Proin Group of Companies, Bw Johnson Lukaza akihojiwa na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa sherehe ya kutimiza miaka 3 ya kuzaliwa kwa Bongo Movie.
 Bi Mwenda akifurahi kukabidhiwa cheti cha sifa ya kuwa msanii mkongwe
 Mtitu akipokea Cheti kutoka Kwa Mwenyekiti.
 Hawa ndio mabalozi wa Windhoek waliochaguliwa katika sherehe hiyo ya kutimiza miaka 3 ya bongo movie.
 Mkurugenzi Mkuu wa Mabibo Beer, Mama Benadetha Rugemalila ambae alikuwa mdhamini mkuu wa sherehe hiyo kupitia kampuni ya Mabibo Beer akitoa maneno mawili matatu mara baada ya mabalozi wa Bia ya Windhoek kuchaguliwa
 Amin Akishusha Burudani 
 Linex akiimba kwa hisia
 Shilole hakuwa nyuma na wimbo wake wa chuna buzi
Christa Bela akitoa vionjo safi kabisa katika sherehe hiyo.

Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia yatoa wito kwa wananchi kuzingatia matumizi ya tehama



 Kaimu Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano Serikalini wa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia bi Prisca Ulomi akitoa wito kwa wananchi kuzingatia matumizi sahihi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA)  wakati wa mkutano  na waandishi wa habari leo jijini Dar es salam .
Kaimu Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano Serikalini wa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Bi Prisca Ulomi akiwaeleza waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kuhusu hatua iliyofikiwa na Serikali katika  Uandaaji wa Sheria ya Matumizi Salama ya Mtandao,kushoto ni Afisa habari wa Idara ya Habari Maelezo Bi Fatma Salum.

DARAJA LA RUVU LAFUNGWA, MKUU WA WILAYA YA BAGAMOYO AWAPIGA 'STOP' WAKAZI WA KIWANGWA KWENDA BAGAMOYO



 Wakazi wa Kiwangwa, wa Kiwangwa, wakivushwa na vijana waliojitolea kujipatia ajila katika Daraja la Ruvu kwa kuwavusha wananchi kwa kuwabea ama kuwaongoza njia ili kuvuka eneo hilo la daraja lililojaa maji kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha nchini. Kamera ya Sufianimafoto iliwashuhudia viajana hao wakiwavuja raia katika eneo hilo kwa ujila wa Sh. 2000 kwa kila aliyebebwa mgongoni asiyetaka kuvua viatu ama kugusa maji hayo, na Sh. 500 kwa kushikwa mkono kuongozwa njia kutoka mwanzo wa maji hayo hadi kuyavuka, na kuyaongoza magari kuvuka eneo hilo ni Sh. 3000 hadi 5000.

Kutokana na mvua kubwa iliyonyesha jana, Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Ahmed Kipozi, alifika eneo hilo na kujionea wananchi wakitaabika kuvuka ene hilo na huku magari ya abiria yaliyokuwa yakitokea Bagamoyo kwenda Kiwangwa, yakibeba abiria na kuishia eneo hilo na kubeba wengine walioshushwa upande wa pili na kugeuza kwa kila abiria kulipa Sh. 1000. Na kisha abiria hao wakipata usafiri mwingine wa kubebwa na Vijana waliopo eneo hilo kwa Sh. 2000 kwa aliyependa ama 500 kwa kuongozwa njia.
 Vijana hao wakiliongoza moja ya gari lililokuwa likivuka eneo hilo ambapo dereva anafuata njia wanayopita vijana hao wa kulia na kushoto hadi kuvuka ili kuoepuka kupita eneo hatarishi na kutumbukia ama kusukumwa na maji hayo yaliyokuwa yakionekana kuwa na nguvu kubwa.
 Mkuu wa Wilaya ya bagamoyo, Ahmed Kipozi, akizungumza na watendaji wake aliowaagiza kusimamia zoezi la kuwazuia wananchi kuvuka eneo hilo, ambapo watendaji hao walimueleza Mkuu huyo wa Wilaya kuwa wananchi wamekuwa wakaidi na kuamua kukataa kutii amri na kuvuka, jambo lililomfanya Mkuu wa wilaya kuamua kuagiza askari Polisi wenye silaha ili kulinda eneo hilo kuwazuia waanchi kuvuka ili kuepuka maafa.

''WA HUKU WA HUKU NA WA HUKO WA HUKO''
Baada ya hapo Mkuu huyo wa Wilaya aliwatoa tamko na kuwataka wakazi wa Kiwangwa kutokwenda Bagamoyo na waBagamoyo kutokwenda Kiwangwa, kwa kipindi chote cha mvua ili kuepuka maafa yanayoweza kutokea kwa kutumbukia na kusombwa na maji, ama daraja hilo la Jeshi kukatika kutokana na maji kuanza kupita juu ya daraja hilo jana.
 Mkuu wa Wilaya, akizungumza na madereva wa magari waliokuwa wakisubiri kuvuka eneo hilo pamoja na vijana waliokuwa wakitoa huduma ya kuwavusha watu.
 Vijana wakifanya kazi yao ya kuwavusha watu eneo hilo.
BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI»

WAKAZI WA KIJIJI CHA KABWE WILAYA YA NKASI MKOANI RUKWA WAFAIDIKA NA UVUVI WA SAMAKI ZIWA TANGANYIKA



 Pichani ni baadhi ya akina mama wakiwa wametoka kununua samaki kwenye bandari ndogo ya Kabwe,Wilayani Nkasi mkoani Rukwa mapema leo jioni,Akina mama hao wameeleza kuwa wengi wao wamekuwa wakijishughulisha na biashara ya samaki ili kujiingizia kipato katika suala zima la kujikwamua na umaskini.
 Mkazi wa kijiji cha Kabwe,akiwa amebeba dishi lililosheheni samaki aina ya Migebuka,anasema kama uonavyo hiyo shehena ya  migebuka huuzwa shilingi 30,000/=
Wavuvi wakitia nanga kando kando ya bandari ya Kabwe .Credit Michuzi Jr Blog

Inauma! Ajali yaua waombolezaji 12



WATU 12 waliokuwa njiani kwenda kuomboleza msiba wa mtoto aliyepoteza maisha baada ya kusombwa na mafuriko, wamefariki dunia na wengine saba wamejeruhiwa, baada ya gari lao kugongwa na malori mawili kwa wakati mmoja.
Abiria hao walikuwa wanasafiri na gari dogo aina ya Toyota Pick Up namba T 170 AKZ kwenda kuhani msiba uliotokea katika kijiji cha Kongei kilichoko Hedaru mkoani Kilimanjaro.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kilimanjaro , Robert Boaz waliofariki ni Stella John (45), Salma Kizoka (33), Marry Senzige (49), Neema Daniel (52), Rehema George, (29), Sophia Mbike (51), Ritta Kallani (55) na Kallan Stephano (55), Kolina Mmasa (55) na Bahati Daudi (25),

Wengine ni Farida Kiondo (24) na Maria John (33) wote wakazi wa Kongei na kwamba miili yao imehifadhiwa katika hospitali ya Wilaya ya Same.

Boaz aliwataja majeruhi kuwa ni Zubeda Mrindoko (42),Mipa Chediel (29) na Zubeda Mlita (32) ambao wamelazwa katika hospitali ya rufaa ya KCMC kutokana na hali zao kuwa mbaya zaidi.

Wengine waliolazwa hospitalini Same ni Joyce Kandogwe (29), Subira Juma (22), Ramadhan Msangi (31) na Adinan Rajab (31).

Ajali hiyo ilitokea juzi saa 2:00 usiku katika barabara kuu ya Tanga-Moshi, nje kidogo ya mji wa Hedaru, ikihusisha magari matatu ambayo ni Fuso (T 299 ANM) ikitokea Moshi kwenda Dar es Salaam na Scania (T 737 AKW) pamoja na tela lake namba T 776 CCN ikitokea Dar es Salaam kwenda Moshi, kwa mujibu wa Mkuu wa Wilaya ya Same, Herman Kapufi.

Alisema watu hao walikuwa wamepanda gari la Diwani wa Kata ya Hedaru (CCM), Gerald Gwena aliyekuwa amewapakia waombolezaji hao kwenye pick-up yake ambayo iligongwa kwa nyuma na Fuso na baadaye gari hilo kuparamiwa kwa nyuma na Scania na kisha kusababisha vifo na majeruhi.

"Waombolezaji hawa walikuwa wanakwenda na diwani kuifariji familia ya marehemu mzee Mwanga ambaye mtoto wake wa kiume, Dismas Mwanga alifariki baada ya kusombwa na mafuriko”, alisema.

Alisema Dismas mwenye miaka tisa aliyekuwa anachunga kondoo milimani alifariki dunia juzi mchana baada ya kusombwa na mafuriko yaliyotokana na mvua kubwa zilizonyesha mfululizo.

Alisema hata, hivyo mpaka sasa haijafahamika iwapo mvua hizo zimesababisha vifo na hasara nyingine.

Kapufi alisema kamati yake ya ulinzi na usalama imekutana kwa dharura kujadili ajali hiyo na hatua ambazo wilaya hiyo itachukua.

Kamanda Boaz, alisema chanzo cha ajali hiyo ni kuzimika ghafla kwa  gari hilo mali ya diwani Gwena ambaye alikimbia baada ya ajali hiyo.

"Ajali hiyo ilitokea baada ya gari hilo kuzimika na Fuso iliyokuwa karibu kuteleza barabarani baada ya kujaribu kusimama ili isigongane na Pick Up iliyokuwa na waombolezaji, lakini lilivutwa na tope lililokuwa limejaa barabarani kisha kugonga kabla ya kupinduka na kuangukia upande wa kulia wa barabara ambako kulikuwa na lori la Scania.

Kamanda alisema watu 10 walikufa papo hapo , wawili walifia hospitalini na saba wamejeruhiwa.
Alisema juhudi za kuwasaka madereva  hao wa Fuso pamoja na diwani huyo zinaendelea.

CHANZO: NIPASHE JUMAPILI

Sunday, March 30, 2014

WBO WATOA UJUMBE MASHALI AKIMGALAGAZA KASEBA KWA POINT


Mabondia Japhert Kaseba na Thomas Mashali wakipambana wakati wa mpambano wao uliofanyika katika ukumbi wa PTA Sabasaba kugombania ubingwa wa UBO Africa Mashali alishinda kwa Pointi picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Mtoto Zainabi 'Ikota' Mhamila katikati akiwa na mkata wa Ubingwa wa UBO Africa katika kona ya bondia Japhert Kaseba kabla ya kuanza kwa mpambano wao mkanda uho aliubeba kwa ajili ya kuwaonesha mashabiki pamoja na mabondia waliokuwa wakiwania mkanda huo

Mtoto Zainabu 'Ikota' Mhamila akiwa na mkata wa Ubingwa wa UBO Africa kabla ya mpambano kuanza katika kona ya Thomas Mashali ambaye alishinda na kuunyakuwa mkanda huo kwa kushinda kwa point

Mtoto Zainabu 'Ikota' Mhamila katikati akiwa na mkanda wa ubingwa wa UBO kabla ya kuanza mpambano huo uku Rais wa ngumi za kulipwa nchini Emanuel Mlundwa akiwakumbusha mabondia Thomas Mashali kushoto na Japhert Kaseba sheria zitakazotumika katika mpambano huo www.superdboxingcoach.blogspot.com
Bondia Kalage Suba kushoto akipambana na Alan Kamote wakati wa mpambano wao wa ubingwa wa Universal Boxing Organisation UBO katika ukumbi wa PTA Sabasaba Kamote alishinda kwa TKO ya raundi ya saba oicha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Bondia Alan Kamote akiwa na ubingwa wa Universal Boxing Organisation UBO
Mtoto Zainabu 'Ikota' Mhamila katikati akiwa na mkanda wa ubingwa wa UBO kabla ya kuanza mpambano huo
Baadhi ya watoto ambao wanafanya mazoezi katika GYM mbalimbali walijitokeza kuamasisha ujumbe wa World Boxing Ordanization 'WBO'  kushoto nio Rashidi Matumla na kulia ni Promota kutoka tanga Ally Mwazoa ambaye anakuja kwa kasi uku akiwa na mapasmbano matatu mfululizo yatakayofanyika PTA Sabasaba

Mabondia wakongwe Jock Hamisi kushoto akipambana na Said Chaku wakati wa mpambano wao waliotoa droo

Katika kuhakikisha ujumbe wa WBO unazingatia mtoto Zainabu 'Ikota' Mhamila akipiga padi huku akisimamiwa na Emanuel Mlundwa

Baadhi ya watoto waliojitokeza katika kampeni ya kufanya mazoezi watoto wasipewe madawa wakiwa katika picha ya pamoja na wageni mbalimbali uku wakiwa na zawadi zao walizopewa mabegi flana na glove zenye ubora wa ali ya juu

Zainabu 'Ikota' Mhamila

Ashanti Utd yawafumua maafande wa Oljoro JKT


Ashanti United ambao wameibuka na ushindi leo dhidi ya Oljoro JKT ya Arusha
 WATOTO wa Jiji, Ashanti United jioni ya leo imezinduka na kufufua matumaini yao ya kubaki katika Ligi kuu Tanzania Bara baada ya kuwacheza kwata maafande wa Oljoro JKT ya Arusha kwa kuwalaza mabao 2-1 katika pambano pekee la ligi hiyo lililochezwa leo.
Pambano hilo lilichezwa kwenye uwanja wa Chamazi na washindi walienda mapumziko wakiongoza kwa bao 1-0 lililofungwa na Hassani Kabunda, huku Oljoro wakipoteza penati katika dakika ya tano tu ya mchezo huo.
Kipindi ca pili wenyeji walipata bao la pili lililofungwa kwa mkwaju wa penati na Hassani Kabunda kabla ya Oljoro kujipatia bao la kufutria machozi lililotokana pia kwa mkwaju wa penati kupitia kwa Shaibu Nayopa.
Ushindi huo uliokuwa ukihitajiwa mno na Ashanti umeiwezesha timu hiyo inayonolewa na kocha mahiri, King Abdallah Kibadeni, kufikisha jumla ya pointi 21 kutokana na mechi 23 na kushika nafasi ya 11.
Oljoro ambayo inapigana kuepuka kushuka daraja kama ilivyo kwa wapinzani wao, imeendelea kusota kwenye nafasi ya 13 ikiwa na pointi 16, tatu zaidi ya wanaoburuza mkia Rhino Rangers ambayo kesho itakuwa wageni wa JKT Ruvu kwenye uwana wa Chamazi.
Mechi nyingine zitakazopigwa kesho ni kati ya vinara wa ligi hiyo, Azam itakayokwaruzana na Simba kwenye uwanja wa Taifa, Yanga watakuwa ugenini kuumana na Mgambo JKT, huku mabingwa wa zamani Mtibwa Sugar na Coastal Union watapepetana uwanja wa Manungu, Morogoro na Kagera Sugar itaialika Ruvu Shooting na jiji la Mbeya litashuhudia Mbeya City na Prisons-Mbeya zitaumana uwanja wa Sokoine.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...