(Picha na Maelezo-Dodoma)
(Na Magreth Kinabo ,MAELEZO Dodoma)
KAMATI ya Uongozi wa
Baraza la Vyama vya Siasa inawaomba wajumbe wote wa Bunge Maalum la Katiba
kuzingatia kanuni kwani zinakataza
vitendo vya utovu wa nidhamu wakati wa vikao vya Bunge hilo .
Kauli hiyo imetolewa
leo mjini na Mwenyekiti wa Baraza hilo, Peter Mziray katika mkutano na waandishi wa habari
uliofanyika kwenye ukumbi wa Bunge mjini Dodoma kufutia baadhi ya wajumbe wa
Bunge hilo kuonesha vitendo visivyo na nidhamu
ikiwemo kuzomea.
“ Kamati ya Uongozi wa
Baraza la Vyama vya Siasa inawaasa wajumbe wote wa Bunge Maalum la Katiba
kubadilika na kuonesha nidamu ambayo Watanzania wote wanategemea kutoka kwao,”
alisema Mziray.
Alisema Kamati hiyo inaamini kuwa mjumbe anaweza kutoa
hoja yake nzito ya kukubali na kupinga jambo ikakubalika au kukataliwa na
wajumbe wengine wengine au Mwenyekiti bila
ya kuzomewa.
Aidha Mwenyekiti huyo
Mziray amemtaka Mwenyekiti wa Bunge Maalum kutoyatambua makundi ya Tanzania
Kwanza na UKAWA kwa kuwa sio makundi rasimu ndani ya Bunge hilo na ndio
yanasababisha vurugu kwa kuweka maslahi ya vya siasa mbele badala ya Taifa.
Amewataka wajumbe wa
Bunge Maalum la Katiba kuacha kujihusisha na makundi hayo
badala yake wachambue na kuunga mkono hoja kwa uzito wa hoja na
kuzingatia masilahi ya taifa badala ya kuzingatia mtazamo wa kundi fulani.
Mziray ameongeza kuwa wajumbe wanatakiwa kuepuka vitendo
ambavyo vinakwamisha mchakato wa kupata Katiba mpya kwa mustakabali wa taifa
hili na Wananchi kwa ujumla.
Katika hatua nyingine Mwenyekiti huyo amesema kuwa Kamati ya
Uongozi imeona ni vema wajumbe wa baraza
hilo, wakuu wa vyama vya siasa, ambao si wajumbe wa baraza hilo wakutane ili
kujadiliana, kushauriana na kuridhiana ili kuweza kufanikisha azma ya kupatikana kwa Katiba Mpya kwa mwafaka.
No comments:
Post a Comment