Bondia wa
ngumi za kulipwa Fadhili awadh amefariki dunia katika hospital ya mwananyamala baada
ya kuugua kwa siku kadhaa. Fadhili awadh alikuwa ni miongoni mwa mabondia
waliochaguliwa kucheza mpambano wa
ubingwa tarehe 29 mwezi huu wa tatu dhidi ya mpinzani wake toka tanga Alan
Kamote, hivyo pia alikuwa katika maandalizi ya mpambano huo. Sababu ya kifo
chake kwa ripoti ya daktari wa mwananyamala kwa kiongozi wa ngumi Ibrahim Kamwe
ni kuwa fadhili alikuwa na malaria na alitumia dozi ya metakelfin, na hali ilibadirika
pale alipojaribu kufanya mazoezi na
kujisikia vibaya na kuwahishwa katika hospitali hiyo ambayo alikaa kwa siku
mbili akiendelea na matibabu na hatimae umauti ulipomkuta. Fadhili awadh mwenye
umri wa maika 32 alikuwa anaendelea vizuri katika mchezo huo kiasi cha kufikia
kucheza pambano la ubingwa katika ukumbi wa PTA sabsaba, akiwasindikiza
mabondia japhet kaseba na Thomas mashali . sisi tulimpenda lakini mungu
alimpenda zaidi ,Ailaze roho ya marehemu Fadhili awadh “tiger” peponi,mwili wa marehemu umesafilishwa kwenda morogoro kwa ajili ya maziko bondia huyo enzi za uhai wake alicheza mapambano 12 amepoteza 5 na kushinda 7 ambapo mpambano wake wa kwanza katika harakati za ngumi za kulipwa alicheza tarehe
10,09,2010 |
na mpambano wake wa mwisho alicheza na Mfaume Jumanne feb 16 katika ukumbi wa kwa mama rajabu chanika na kufanikiwa kushinda kwa K,O ya raundi ya pili
No comments:
Post a Comment