Kamati
ya PAC Leo imekutana na Benki Kuu ya Tanzania kupokea Maelezo kuhusu
fedha tshs 201 bilioni za akaunti ya Tegeta Escrow. Fedha hizi
zinahusiana na mkataba IPTL. PAC ina wasiwasi kwamba TANESCO, kwa mujibu
wa nyaraka, itatakiwa kulipa fedha nyingi zaidi zinazofikia zaidi ya
tshs 200 bilioni kwa kampuni iliyonunua IPTL.
Kamati imeamua kwamba;
1)
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali afanya ukaguzi maalumu
wa suala zima IPTL na uhalali wa utoaji wa fedha kutoka akaunti maalumu
ya tegeta escrow.
2)
TAKUKURU waanze uchunguzi wa mchakato mzima wa mkataba wa IPTL, umiliki
wa kampuni hiyo na uhamishaji wa umiliki kwenda kampuni ya PAP.
Kamati
imeshangazwa na kitendo cha Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini
kuanzisha ukaguzi maalumu wakati yeye mwenyewe ni mtia saini kwenye hati
ya kutoa fedha hizo na mshiriki mkubwa katika mchakato mzima. Hivyo,
kamati imeagiza ukaguzi maalumu kutoka kamati PAC ili kuweza kupata
ukweli.
PAC
imetoa mpaka mwisho wa mwezi Aprili kwa taarifa ya ukaguzi huo kuwa
umekamilika na kuwataka wahusika wote wa mchakato wa IPTL kusubiri
matokeo ya ukaguzi.
PAC imetaka pia maamuzi ya mahakama kuheshimiwa.
Imetolewa na
Mwenyekiti PAC-Zitto Kabwe(MB)
Dodoma
Jumapili 16 Mechi 2014
No comments:
Post a Comment