Mkurugenzi
wa Masoko Na Mahusiano Kutoka Dhamana ya Uwekezaji Tanzania Bwana
Daudi Mbaga Akitoa Mada Kuhusu Kuwekeza kwenye Mifuko Iliyo chini ya
Dhamana ya Uwekezaji Tanzania Kwajili ya Maisha Mara Baada ya Kustaafu
kwenye Semina ya Wafanyakazi wanaokaribia Kustaafu Iliyoandaliwa na
TAGLA Mkoani Morogoro.
Washiriki
wa Semina ya Wanaokaribia Kustaafu Wakifuatilia Kwa Makini Mada
Iliyokuwa Ikitolewa Kuhusu Uwekezaji katika Mfuko wa Jikimu Iliyokuwa
Inatolewa Na Mkurugenzi wa Masoko Ndugu Daudi mBAGA (hayupo
Pichani)Kutoka Dhamana ya Uwekezaji Tanzania Inayoendelea Mkoani
Morogoro
Mmoja wa Washiriki wa Semina Hiyo aAkiuliza Swali kuhusu Uwekezaji katika Mfuko wa Jikumu.
Watanzania
Wameshauriwa Kuwekeza kwenye Mifuko Iliyo Chini ya Dhamana ya Uwekezaji
Tanzania Kwa Lengo la Kuwekeza kwajili ya Maisha mara Baada ya
Kusataafu.Wito Huo Umetolewa na
Mkurugenzi wa Masoko na Mahusiano Kutoka Dhamana ya uwekezaji Tanzania
Bwana Daudi Mbaga Wakati Akitoa Mada Kwenye Semina ya wafanyakazi
Wanaokaribia Kustafu Inayoendelea Mkoani Morogoro.
Alisema
Kwamba Watanzania Wengi huwa hawajui Nini Cha Kufanya Pindi
Wanapostaafu Hali Inayosababisha Watanzania Wanapostaafu wakishapokea
Mafao Yao wanajaribu Kufanya Kila Shuguli Mbalimbali Lakini Kutokana na
kutokuwa na Uzoefu wa Shuguli Hizo shuguli nyingi hazidumu.
Bw
Mbaga Amewashauri Watanzania hasa Wale wafanyakazi wanaokaribia
Kustaafu Kuwekeza Mifuko iliyopo Chini ya Dhamana ya Uwekezaji Tanzania
Kama MFUKO WA JIKIMU Wenye "Kauli Mbiu Ishi Vizuri Unastahili". Kwa
Lengo la Kuwasaidia Wastaafu Ili Kuondokana na Kupata Hasara na
Kufurahia Maisha Zaidi Mara Baada ya Kustaafu.
Ameongeza
Ni vizuri kwa watanzania kuwekeza katika Mfuko Huo kwa kuwa Upo Chini
ya taasisi ya Serikali na uwekezaji wao ni wa Uhakika.Pia Kuwekeza
Katika Mfuko Huu watanzania watapata Faida Nyingi kwani Mfuko Huu
Unaendeshwa Kitaalamu na Wataalamu Waliobobea Katika Msawala ya
Uwekezaji ,Urahisi wa wawekezaji wanaweza kufuatilia Maendeleo ya
Masoko ya FedhaKwa Kufuatilia Mandeleo ya Mifuko.
Mkurugenzi
alisema Uwekezaji katika Mfuko Huo ni wa Uhakika kwasababu Unampa
Mwekezaji Unafu wa Gharama za Uwekezaji, Uwazi ,Faida Nzuri,Urahisi wa
Kujiunga katika Mfuko Huu.
No comments:
Post a Comment