Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Thursday, March 6, 2014

OPERATION KOKORO YAVUNA WANACHAMA 1800 WILAYA YA MWANGA


Ziara ya Mwenyekiti wa Vijana Wilaya ya Mwanga Mkoa wa Kilimanjaro Komredi Japhar Mghamba akiongozana na Katibu Msaidizi wa Mkoa Maalum wa Vyuo Vikuu Komredi Daniel Zenda inaendelea kwa mafanikio makubwa katika wilaya hiyo ambapo mpaka sasa imefanikiwa kuingiza Vijana 1800 katika Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) pamoja na Chama.

Ziara hiyo iliyobeba jina la Operation Kokoro iliyoanza wiki iliyopita ilipata misikosuko hasa baada ya moja ya msafara wake kushambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana. Operation hiyo inayolenga kuhamasisha Vijana wa Upinzani na wasio na vyama kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM), kuhamasisha Vijana wa CCM kugombea nafasi mbalimbali katika uchaguzi ujao wa Serikali za mitaa hapo baadae October mwaka huu pamoja na kukagua, kuhamasisha na kuelezea katika matawi na kata juu ya utekelezaji wa Ilani ya chama kwa kauli mbiu "CCM Mwanga Ukimya sasa Basi"

Operation kokoro tayari imeshapita katika kata ya Kisangara, na kuendelea katika milima ya upareni maeneo ya Ugweno, Msangeni, Kifula, Mamba na Kikweni. Viongozi hao wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi wametembelea vikundi mbalimbali vya bodaboda, makundi ya wajasiriamali wadogo na wakubwa pamoja na kukagua miradi iliyoainishwa kwenye Ilani ya Chama ambayo inayoendelea kutekelezwa wilayani humo na Serikali ya Chama Cha Mapinduzi.

Viongozi hao wakiwa wanahutubia mkutano wa hadhara katika eneo la Msangeni wamesema kuwa wananchi waendelee kuiamini CCM kwani ndio Chama Bora Cha siasa ambacho kinasikiliza kero za wananchi wake na kuzitafutia ufumbuzi na kutaja kero mbalimbali ambazo tayari zimepatiwa ufumbuzi wa kudumu wilayani humo.

Ziara hiyo inaendelea katika kata na maeneo mengine ya wilaya ya Mwanga.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...