Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Monday, March 10, 2014

Victoria Prince Mwanza Mabingwa Safari Nyama Choma 2014.


Na Mwandishi Wetu.Mwanza.

Victoria Prince Bar wameibuka mabingwa katika fainali za mashindano ya Safari Lager Nyama Choma 2014 yaliyofanyiaka mswishoni mwa wiki katika Uwanja wa Furahisha jijini Mwanza na hivyo kuzawadiwa fedha taslimu Shilingi milioni moja(1,000 000/=) na Kikombe.
Mshindi wa pili katika fainali hizo ni Gemestone Bar ambao walizawadiwa fedha taslimu shilingi laki nane (800,000/=), mshindi wa tatu ni SD Executive Bar ambao walizawadiwa fedha taslimu Shilingi laki sita (600,000/=), mshindi wan nne ni Shooters Pub ambao walizawadiwa fedha taslimu Shilingi laki nne (400,000/=) na nafasi ya tano ilichukuliwa na Lunala Bara ambao walizawadiwa fedha taslimu Shilingi laki mbili (200,000/=)
Akizungumza na wakazi jiji la Mwanza waliohudhuria fainali hizo, Mkuu wa Wilaya ya Ilemela, Bi. Amina Masenza  aliwashukuru kampuni ya bia Tanzania(TBL) kwa kuanzisha mashindano hayo yenye mvuto wa pekee na yenye kutoa ajira na kukuza kipato kwa wachoma nyama na si hilo tu hawa walianza kwa semina malumu ya mafunza hivyo Serikali inaamini wanazingatia taratibu zote za afya kwa kuandaa nyama inyokidhi viwango kwa mlaji.
Pili aliwapongeza baa tano zilizoingia fainali kwani wao ndio baa bora katika baa zote zinazochoma nyama mkoani humo na aliwaomba waendelee kuilinda hadhi na sifa hiyo waliyopewa katika jiji la Mwanza na mwisho aliwapongeza mabingwa wa Victoria Prince kwa kutwaa ubingwa wa mashindano ya Safari Nyama Choma kwa mwaka 2014 na kuwaomba ambao hawakufanikiwa kupata nafasi hiyo wajiandae kwa mashindano yajayo ya Safari Nyama Choma 2015.
Nae Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo aliwapongeza mabingwa wa mwaka 2014, Victoria Prince na pia aliwashukuru wote walioshiriki toka mchakato ulipoanza mpaka kufikia kumpata bingwa lakini pia aliwashukuru wakazi wa Mwanza waliojitokeza kwa wingi kuja kushuhudia nani anatwaa ubingwa mwaka huu.
Mwisho shelukindo aliwaomba wakatumie vyema zawadi walizopata kwa kuboresha majiko yao kwa mashndano yajayo ya 2015.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...