Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Thursday, March 6, 2014

PROIN PROMOTIONS LIMITED KUANZA KUSAKA VIPAJI VYA UIGIZAJI NCHINI TAREHE 1 APRIL 2014


Meneja wa Mradi wa Kusaka Vipaji Vya Uigizaji Tanzania (Tanzania Movie Talents) Bw Joshua Moshi akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wakutambulisha kampeni mpya ya kusaka Vipaji vya uigizaji kutoka kampuni ya Proin Promotions Limited mapema leo katika Ofisi za Proin Promotions Limited, Mikocheni, Mtaa wa Ursino, Pembeni ni Meneja Masoko wa Proin Promotions Limited Bw Evance Stephen
Meneja Masoko wa Proin Promotions Limited, Bw Evance Stephen (katikati) akielezea jinsi ya Kampuni ya Proin Promotions itakapozunguka katika Mikoa ya Tanzania Kwaajili ya Kusaka Vipaji vya Uigizaji Tanzania kwenye Mkutano na waandishi wa Habari mapema leo katika Ofisi za Proin Promotions Limited, Mikocheni, Mtaa wa Ursino,, Shindano litaendeshwa na Kampuni ya Proin Promotions Limited.
 Meneja Mradi wa Kusaka Vipaji vya Uigizaji Tanzania (Tanzania Movie Talents) Bw Joshua Moshi (wa kwanza Kushoto) pamoja na Meneja Masoko wa Proin Promotions Limited, Bw Evance Stephen wakisikiliza Maswali kutoka kwa waandishi wa habari wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika leo katika Ofisi za Proin  zilizopo Mtaa wa Ursino Mikocheni
 
 
TAARIFA KWA UMMA
Kampuni ya Proin Promotions Limited ambao ni watengenezaji, wauzaji na wasambazaji wa Filamu za Kitanzania Inakuja na Kali ya Mwaka 2014 katika kuhakikisha inasaka vipaji vya uigizaji Tanzania ili kuhakikisha inaleta mabadiliko na kuibua vipaji katika tasnia ya filamu nchini ambayo inaonekana imesahaulika kabisa kwa kuleta Shindano la Kusaka Vipaji vya Filamu Tanzania lijulikanalo Kama
TANZANIA MOVIE TALENTS
 (TMT) ambapo litazunguka katika kanda sita Tanzania katika Kushindanisha vijana wenye vipaji vya kuigiza na hatimaye Kila mkoa utatoa washindi wa tatu na watasafirishwa hadi Jijini Dar Es Salaam kwa ajili ya raundi ya pili ya mchujo na hatimaye kufanyika Fainali Kubwa ambapo Mshindi wa Kwanza Atajishindia Kitita Cha Shilingi Milioni 50 za Kitanzania. Kanda ambazo zitazungukiwa na timu nzima ya Proin Promotions Limited katika kusaka vipaji vya uigizaji ni Kanda ya ziwa (Mwanza na Kigoma),Kanda ya Kaskazini(Arusha),Kanda ya Kati (Dodoma),Kanda ya Nyanda za Juu Kusini(Mbeya),Kanda ya Pwani (Dar Es Salaam), Kanda ya Kusini(Mtwara) ambapo katika kila kanda watatoka washindi watatu na watano katika kanda ya pwani ambao watakuja Dar-es-salaam kwa ajili ya raundi ya pili ya mchujo.Raundi ya pili itakuwa na  jumla ya watu 23.Kisha kutakuwa na fainali kubwa kabisa ya Kumsaka mshindi wa
TANZANIA MOVIE TALENTS
 ambayo itafanyika Katika Jiji La Dar na Mshindi wa Kwanza kunyinyakulia Kitita cha Shilingi Milioni 50 za kitanzania(
50,000,000/=).
Washindi kumi bora watafanya filamu ya pamoja na Mshindi wa Kwanza atakuwa chini ya Uangalizi wa Kampuni ya Proin Promotions Limited ambapo atakuwa akifanya kazi na Kampuni hiyo Mahiri katika Kutengeneza, kusambaza na kuuza Filamu za Kitanzania. Proin Promotions Limited ambao ni watengenezaji wa Filamu ya Foolish Age, Figo, Long Time ,Kigodoro na Kitendawili wanatarajia kuanza zoezi la hili Aprili 1 mwaka huu katika kanda ya ziwa mkoa wa Mwanza.Watakao ruhusiwa kushiriki katika shindano hili ni vijana wa kitanzania ambao hawajawahi kufanya filamu yoyote wenye umri kuanzia miaka 14 na kuendelea.Filamu ya washindi kumi bora itatengenezwa na kusambazwa na Kampuni ya Proin Promotions Limited.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...