Baadhi ya watunzi na waimbaji wa albamu mpya ya Msondo Ngoma, Eddo Sanga na Juma Katundu |
Akizungumza na MICHARAZO, mmoja wa viongozi na mwanamuziki wa bendi hiyo, Shaaban Dede 'Super Motisha' alisema Msondo imekamilisha kurekodi nyimbo hizo kwa mtayarishaji Malone Linje baada ya kipindi kirefu cha danadana juu ya suala hilo.
Dede ambaye ndiye mtunzi wa wimbo uliobeba jina la albamu hiyo, alisema nyimbo hizo zinahaririwa kwa sasa kabla ya kuanza kurushwa hewani na viongozi kujipanga kwa ajili ya uzinduzi wake.
'Tunashukuru kwa sasa tumeshamaliza kurekodi albamu yetu mpya, mashabiki waliokuwa na kiu ya muda mrefu sasa kiu hiyo imeisha kwani mambo yamekamilika nawakati wowote zitaachiwa hewani baada ya kuhaririwa," alisema.
Nyimbo zilizopo katika albamu hiyo ni pamoja na 'Suluhu' alioutunga Dede, ' Lipi Jema' na 'Baba Kibene' za Eddo Sanga, 'Nadhiri ya Mapenzi' wa Juma Katundu, 'Kwa Mjomba Hakuna Urithi-Huruka Uvuruge na 'Machimbo' uliotungwa na bendi nzima.
Mara ya mwisho Msondo kutoa albamu ilikuwa miaka minne iliyopita walipoachia 'Huna Shukrani' ilikuja baada ya bendi hiyo kuzindua albamu yao ya 'Kicheko kwa Jirani' mwaka 2010.
No comments:
Post a Comment