Shomari Kapombe Mwanamichezo Bora wa 2012 |
Mwenyekiti
wa Kamati ya tuzo, Rehure Nyaulawa amesema leo kwamba baada ya kikao
cha juzi cha Kamati yake juhudi za pamoja baina ya Kamati yake na Kamati
ya Utendaji kuzungumza na wadhamini mbalimbali wakubwa na wadogo kwa
nia ya kufanikisha tuzo hizo zimeanza.
“Kamati
yetu kwanza inawaomba radhi viongozi wa vyama vyote vya michezo
kutokana na tuzo kushindwa kufanyika mwaka jana na hilo kwa mujibu wa
taarifa ya uongozi wa TASWA iliyowasilishwa kwenye kikao chetu,
ilitokana na sababu mbalimbali lakini kubwa ni kujitoa dakika za mwisho
kwa baadhi ya kampuni zilizokuwa zimethibitisha kudhamini tuzo hizo,”.
Hata
hivyo, Nyaulawa ameomba wendelee kutoa ushirikiano mwaka huu na kwa
kuanzia watawatumia barua rasmi za kuomba majina ya wanamichezo wao
waliofanya vizuri kuanzia Januari 2013 hadi Aprili mwaka huu, ambapo
matarajio yao wanamichezo wasiopungua 40 watapewa tuzo.
Amesema
kwamba kamati pia imeamua kwamba kila mwaka tuzo hizo zijena ujumbe
maalum kwa wanamichezo, ambapo kwa kuanzia tuzo za mwaka huu ujumbe wake
utakuwa ni: ‘Wanamichezo Tupige Vita Ujangili’.
“Tunaamini
wale wote wataowania, wale watakaoshinda tuzo hizo na wanamichezo wote
wakiwemo waandishi wa habari za michezo tutashirikiana na jamii kwa
ujumla kwa kuwa mstari wa mbele kuhamasisha vita dhidi ya ujangili kwa
namna tutakavyomudu,”amesema.
Amesema
pia katika kuhakikisha tuzo za mwaka huu zinakuwa bora kwa maslahi ya
wanamichezo wote hapa nchini, kamati imeteua baadhi ya viongozi wa
kiserikali kuwa washauri wa kamati katika masuala mbalimbali na sasa
wanasubiri majibu yao ili waweze kuwatangaza rasmi.
No comments:
Post a Comment