KUNA
njia nyingi ya kumtukuza, kumuabudu na kupata Neema ya Mungu ambayo ni
kwenda kanisani na kusali na njia ya nyimbo ambayo mtu unaweza kupata
Baraka kubwa kutokana na nyimbo za injili zinazoimbwa na waimbaji
mbalimbali wa muziki huo; amesema Mama Tunu Pinda.
Mama
Pinda ambaye ni mke wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mizengo Peter Pinda, ameyasema hayo alipozungumza na Hekaheka kuhusu
Tamasha la Pasaka linalotarajiwa kufanyika Aprili 20 mwaka huu ambayo
itakuwa ni Sikukuu ya Pasaka inayoadhimishwa na Wakristo Duniani kote
kwa Kufufuka Yesu Kristo mwana wa Mungu.
Akielezea
faida za kwenda kwenye Tamasha la Pasaka, Mama Pinda anasema ni kwa
ajili ya kwenda kusikiliza nyimbo mbalimbali zitakazokuwa zikiimbwa na
waimbaji wa nyimbo za injili ambako unaweza kupata Baraka na kuachana na
matendo yasiyompendeza Mungu na hatimaye kutenda dhambi.Tamasha
hilo ambalo huandaliwa na kampuni ya Msama Promotions, linatarajiwa
kufanyika Jijini Dar es salaam kwa siku hiyo ya Pasaka na hatimaye
katika Mikoa mingine saba ya Tanzania Bara.
“...Mwaka
juzi nilipokuja kwenye Tamasha la Pasaka kulikuwa kuna watu wengi wa
kila rika wazee, vijana na hata watoto wadogo hali hiyo ilidhihirisha ni
kwa namna gani Watanzania wanapenda nyimbo za injili ambazo ninaamini
wanapata Neema ya Mungu, alisema Mama Pinda.Akaongeza,
“Utamaduni huu wa kusherehekea Sikukuu za kidini kama vile Pasaka kwa
kwenda katika matamasha ya nyimbo za injili ni mzuri kwa sababu
unawaondoa watu katika vishawishi na kuwafanya kuwa karibu zaidi na
uwepo wa Mungu,…”
Amesema
ili kupata Neema ya Mungu ni vyema watu wengi zaidi wakajitokeza siku
hiyo ya Tamasha la Pasaka kwa Dar es salaam na mikoa mingine ambayo
Tamasha litafika ili kuweza kujizolea baraka za Mungu kupitia nyimbo za
injili ambazo zitaimbwa na waimbaji wa ndani na nje ya nchi; huku
akisisitiza kuwa endapo atapata nafasi kwa mwaka huu atahudhuria tamasha
hilo. Hata hivyo alisema
nyimbo za injili ni burudani lakini kwa upande mwingine ni sehemu ya
ibada ambayo msikilizaji anapokea Baraka na mafundisho ya biblia kupitia
nyimbo hizo; lakini pia zinasaidia kutokutenda dhambi kwa kwenda katika
starehe ambazo hazimpendezi Mungu.
“…Sikuku
ya Pasaka inaadhimishwa kwa Kufufuka kwa Yesu Kristu ambayo ni alama ya
ushindi kwa wanadamu, hivyo ni busara kwa Wakristo wote kuhakikisha
tunaacha dhambi na kuyashika yale yote aliyotuachia Yesu Kristo, ambayo
ni Upendo na Amani bila kusahau kuiombea nchi yetu.
Tamasha
la Pasaka ambalo linatarajiwa kuwashirikisha waimbaji mbalimbali wa
nyimbo za Injili kutoka ndani na nje ya nchi, lengo kuu ni kuweza kupata
fedha kwa ajili ya kuwasaidia watoto wanaoishi katika vituo vya kulelea
yatima, akinamama wajane na wengine wenye uhitaji maalum.
Hata
hivyo Mama Pinda aliwataka Watanzania kuwa na Moyo wa kujitoa kwa watu
wahitaji ambao wanahitaji misaada mbalimbali na hawana mtu wa
kuwasaidia. “…Unaweza
kukuta familia moja mtoto anakula chakula mpaka anazasa na kutupwa,
lakini familia nyingine mtoto hana chakula na analala njaa; hivyo ni
jukumu letu sote kusaidiana kama binadamu, tusiiachie serikali kila kitu
ifanye,” alisema Mama Pinda.
Akaongeza
kuwa Mkurugenzi wa Msama Promotion Alex Msama, ni mfano mzuri wa kuigwa
na watu wenye uwezo kuwasaidia wahitaji, kwa kufanya hivyo watapata
Baraka na kuongezewa zaidi.
No comments:
Post a Comment