Mafundi
wakiendelea kulaza mabomba yatakayotumika kusafirishia maji kutoka Mitambo ya
Maji ya Ruvu Chini mpaka kwenye Tanki la kuhifadhia maji lililopo Chuo Kikuu
cha Ardhi jijini Dar es Salaam. Mpaka sasa mafundi hao wameshasambaza mabomba
kwa umbali wa kilomita takribani 29 kati ya kilomita 55. Kazi hii inatarajiwa
kukamilika mwezi Juni, mwaka huu.
Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka
Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango ikiwa katika picha ya pamoja na Meneja wa Mtambo
wa Ruvu Chini, Mhandisi Emmanuel Makusa (Watatu kushoto) kwenye lenye uwezo wa
kusafirisha lita milioni 360 za maji kwa siku wakati walipokuwa kwenye ukaguzi
wa mitambo ya Ruvu Chini.
No comments:
Post a Comment