Baadhi ya waamuzi wakiwa uwanjani |
WAAMUZI na waamuzi wasaidizi 22 wameteuliwa
kushiriki semina na mtihani wa utimamu wa mwili kwa robo ya kwanza ya mwaka huu
itakayofanyika jijini Dar es Salaam kuanzia Machi 14 hadi 16.
Semina hiyo inashirikisha waamuzi wote wenye beji
za Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) na wale wa ngazi ya juu
(elite) kutoka Tanzania Bara za Zanzibar.
Waamuzi hao ni Charles Simon (Dodoma), Dalila
Jafari (Zanzibar), Ferdinand Chacha (Mwanza), Hamis Chang’walu (Dar es Salaam),
Helen Mduma (Dar es Salaam), Israel Mujuni (Dar es Salaam), Issa Vuai
(Zanzibar), Janeth Balama (Iringa), Jesse Erasmo (Morogoro), John Kanyenye
(Mbeya) na Jonesia Rukyaa (Bukoba).
Josephat Bulali (Zanzibar), Lulu Mushi (Dar es
Salaam), Martin Saanya (Morogoro), Mfaume Nassoro (Zanzibar), Mohamed Mkono
(Tanga), Mwanahija Makame (Zanzibar), Ngaza Kinduli (Zanzibar), Oden Mbaga (Dar
es Salaam), Ramadhan Ibada (Zanzibar), Samwel Mpenzu (Arusha) na Waziri Sheha (Zanzibar).
Wakufunzi wa semina hiyo ambao wanatambuliwa na
Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) ni Joan Minja na Riziki Majala.
No comments:
Post a Comment