MOJA ya pambano kali la kusisimua kabisa lilifanyika usiku wa kuamkia Jumapili ya Mei 3, 2009 huko Marekani kwenye ukumbi wa Las Vegas kati ya bondia Manny Pacquiao 'The PacMan' na Ricky Hatton maarufu kama Hitman.
Pacquiao alianza pambano hilo kwa kasi akishambulia ngumi lakini kwa tahadhari kubwa dhidi ya Hatton, ambaye si bondia wa kumtabiria, masabiki walikuwa wakipiga kelele kwa kushangailia wakati wote.
Kadiri randi ilivyokuwa ikisonga mbele ndivyo Pacquiao alivyokuwa akishambulia kwa kasi na kuonyesha ubora wa hali ya juu, alkuwa akipiga ngumi za kudonoa yaani 'jab' kali na kwa hesabu za hali ya juu na kufanikiwa kupenyeza ngumi nyingi kwa 'Hitman' akitumia jab na ngumi mkunjo za kulia yaani 'right hooks'.
Katika raundi hiyo ya kwanza Pacquiao alimkamata Hatton mara tatu kwa right hok zake kali zilizotua barabara katika kichwa chake na 'kumpotzea' kabisa Hatton katika raundi hiyo ambapo alikuwa akijitahidi kukwepa bila mafankio makubwa.
Ukingoni mwa raundi hiyo Hatton naye 'akazinduka' na kurusha makombora kadhaa kwa Pacquiao na kumfanya alalie kamba, Hatton mzaliwa wa Manchester akambana Pacquio na kumshambulia kwa right hook na left hook ambazo hata hivyo nyingi ziliishia katika mikono ya Pacquiao.
Hatton akaendelea kumbana Pacquaio kweny kamba lakini mpinzani wake huyo akawa anatumia ngumi ndefu za kati aipiga tumbo na kifua na moja moja akitumbukiza katika uso wa Hatton na ngumi zote zilimwingia Hitman.
Ndipo ghafla alipojinasua kwenye kamba na kupiga ngumi mkunjo kali ya kulia yaani 'right hook' na Hitman akadondoka chini kama mzigo wa kuni katika raundi hiyo ya kwanza.
Umati ukalipuka kwa shangwe na hasa mashabiki wa Pacquiao, Hatton akajizoa chini na mwamuzi akamuhesabia hadi 8, akapanguza glavu zake na kusema yuko fit kuendele anapambano zikiwa zimesalia sekunde 46 raundi ya kwanza kumalizika.
Mwamuzi aliporuhusu tu pambano, Pacquaio hakukawia akamfuata kwa kasi Hatton na kumsukumia 'right hooks', na jabs za nguvu na ngumi nyoofu ya kushoto au 'straight lefts'.
Hatton kwa uzoefu wake akajaribu kujikinga lakini hakuweza kukinga ngumi zote kwani ngumi 5 zilimkamta barabara na kumfanya aone' double double' na ndipo Pacquio akakaza musuli wa mkono wa kushoto na kumtandika Hitman, ngumi kali iliyomwelemea na kujikuta akidondoka tena chini kwa mara ya pili katika raundi ya kwanza.
Ilikuwa ni bahati kwake wakati anakwenda chini zlikuwa zimesalia sekunde 7 na hivyo alivyoanza kuhesabiwa raundi ikawa imemalizika na ikawa ni dhahiri Hatton ameokolewa na kengele, mabondia wote wakaenda kwenye kona zao kufuta pumzi.
Raundi ya pili ilipoanza, Hatton alianza kwa kurusha jab zake nyingi na kutumia zaidi 'left hook' ambazo kadhaa zilimpata Pacquiao ambaye wakati fulani pamona na kupigwa ngumi za nguvu kichwani na kuonekana kulewa, lakini alikuwa na nguvu kiasi cha kushindwa kudondoka.
Pacquiao akawa anatumia ngumi za mnyooko yaani 'straight punch' , kisha akapiga jab ya kushoto akapiga tena ngumi ya kulia na kwa kasi ya ajabu, akaachia ngumi kali ya kushoto iliyompata Hatton na kumpeleka sakafuni.
Ngumi hiyo ilipigwa katikati ya ulingo wakati raundi ya pili inaelekea ukingoni, Hatton akajitutumua kujizoa pale hini kwa ni ay kutaka kuendelea kupigana kama alivyofanya kwenye raundi ya kwanza.
Akamudu kusimama kw akuumb, mwamuzi akaruhusu pambano kuendelea baada ya kuwa amemuhesabia Hatton naye kujibu kuwa ataendelea, Pacquiao hakukawia, akamfuata tena na kumcharaza konde kali la mkono wa kulia na Hatton akadondoka tena chini kama zigo la nyanya.
Safarii hii mwamuzi Kenny Bayless hakujisumbua tena kumhesabia Haatton baada ya kumuona akihema kwa nguvu akiwa amelala chali na wala kutokuwa na dalilia ya kunyanyuka mapema, alibaki akipepesa macho pale chini.
Pambano likawa limemalizika katika raundi ya pili na Manny Pacquiao akawa bingwa kwa kumpoka ubingwa Hatton, akajiwekea rekodi ya mapambano 49 akipoteza 3 sare 2 huku 37 akishinda kwa KO na kuifanya rekodi ya Hatton iwe mapambano 45 akipoteza 2, huku 32 akishinda kwa KOs. Hakika hilo lilikuwa ni moja ya pambano bora la KO.
No comments:
Post a Comment