FAIDIKA
Chief Executive Officer Marion Moore (right) hands over a certificate
to Margaret Yohana, an entrepreneur from Famasa Disabled Group who
attended a two days " NAWEZA", a FAIDIKA free financial empowerment
seminar held in Dar es Salaam end of the week. Left is co-author and
project coordinator, Dr Ellen Otaru Okoedion.
An
entrepreneur from Famasa Disabled Group who attended a two days
"NAWEZA", a FAIDIKA free financial empowerment seminar held in Dar es
Salaam end of the week, Helen Makuru (left) is congratulated by VIBINDO
Society Chairman Gaston Kikuwi shortly before receiving her certificate
from FAIDIKA Chief Executive Officer Marion Moore.
FAIDIKA
Chief Executive Officer Marion Moore (right) hands over a certificate
to Famasa Disabled Group Chairperson, Lillian Kabaliki, who was part of
entrepreneurs who attended a two days "NAWEZA", a FAIDIKA free
financial empowerment seminar held in Dar es Salaam at the weekend.
Center is VIBINDO Society Chairman Gaston Kikuwi.
FAIDIKA
Chief Executive Officer Marion Moore (right) hands over a certificate
to an entrepreneur from Famasa Disabled Group who attended a two days
"NAWEZA, a FAIDIKA free financial empowerment seminar held in Dar es
Salaam at the weekend, Fatuma Miringa. Center is VIBINDO Society
Chairman Gaston Kikuwi.
FAIDIKA
Chief Executive Officer Marion Moore (center) speaks to a group of
entrepreneurs from marginalized groups and local Tanzanians from the
streets, who attended a two days "NAWEZA", a FAIDIKA free financial
empowerment seminar held in Dar es Salaam at the weekend. Left is
VIBINDO Society Chairman Gaston Kikuwi and right is Andrew Okallo,
Project designer.
Director
for Small Industries and Small and Medium Enterprises (SMEs) at the
Ministry of Industry and Trade, Consolata Ishebabi, speaks to a group of
entrepreneurs from marginalized groups and local Tanzanians from the
streets, who attended a two days "NAWEZA", a FAIDIKA free financial
empowerment seminar held in Dar es Salaam at the weekend. Left is
VIBINDO Society Chairman Graston Kikuwi and right Emanuel Mwakyusa
co-author of the training manual and moderator.
One of
the entrepreneurs (fourth right) who attended a two days"NAWEZA", a
FAIDIKA free financial empowerment seminar held in Dar es Salaam at the
weekend, being congratulated by the seminar moderators, organizers and
sponsors.
====== ====== ======
FAIDIKA: Kuchukua mikopo ya biashara bila elimu ya ujasiriamali ni hatari
Na Mwandishi Wetu.
Wajasiriamali
wakitanzania wameonywa dhidi ya tabia ya kuchukua mikopo bila kuwa na
elimu sahihi ya kuziendesha biashara zao, lakini badala yake wanapaswa
pia kupata elimu ya ujasiriamali kama wanahitaji kuziendeleza biashara
zao.
Wataalam
wameonya kuwa mikopo bila ya kuwa na ujuzi wa uendesheji biashara
unaweza sababisha biashara kufanya vibaya, mtaji kufa kabisa na
kupelekea mkopaji kubaki na madeni makubwa.
Akizungumza
wakati wa warsha ya siku mbili iliyoandaliwa na FAIDIKA kwa
wajasiriamali wadogo na wa kati kupata mafunzo ya usimamizi wa biashara
na fedha iliyofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, Mkurugenzi
wa viwanda vidogo na biashara ndogo ndogo na wa kati kutoka Wizara ya
Viwanda na Biashara, Consolata Ishebabi alisema biashara za kitanzania
zinashindwa kuendelea kutokana na ukosefu wa elimu ya usimamizi bora na
uongozi wa biashara.
“Watanzania
wengi wajasiriamali wanadhani kuwa na mtaji wa kutosha ni njia pekee ya
kufanikiwa katika biashara. Hili ni wazo potofu. Wengi uchukua mikopo
baada ya hapo biashara zao ushindwa kukua na wanajikuta katika madeni
makubwa,” alisema.
Aliwaasa
wajasiriamali kujenga utamaduni wa kutafuta mafunzo fasaha kabla ya
kuwekeza sana katika biashara ambazo hawazifahamu kiundani.
Kwa
upande wake, Ofisa Mtendaji Mkuu wa FAIDIKA Marion Moore alisema ikiwa
ni kama mchango wa kampuni yake kwenye ustawi wa jamii ya kitanzania,
FAIDIKA imetanua wigo wa elimu ya ujasiriamali mpaka kwa jamii ya
kitanzania isiyokuwa na uwezo, kupitia warsha ya mafunzo ya usimamizi wa
biashara na uhamasishaji ijulikanayo kama ‘FAIDIKA FREE Financial
Empowerment, ikiwa na kauli mbiu ya ‘NAWEZA’.
Warsha
hiyo pia iliyoambatana na uzinduzi wa kitabu cha mafunzo kilichoandikwa
na wataalam watatu wa mafunzo ya biashara, imeanzia jijini Dar es Salaam
na itaendelea katika mikoa mingine.
“Mpango
huu umelenga katika kukuza na kutekeleza mbinu za ukuzaji uchumi kwa
watu wa hali ya chini kama walemavu na watu waishio katika mazingira
magumu kupitia mikopo midogo midogo na elimu ya ujasiriamali na
itafanyika kama warsha ya siku mbili itakayojumuisha masuala yote ya
jinsi gani ya kuanzisha, kuendesha biashara na pia jinsi ya kutumia
teknolojia hususani ya simu za mokoni ili kuboresha biashara,” alisema.
Bi Moore
alisema kuwa mwishoni mwa warsha, washiriki wataweza kutambua ni
biashara ya aina gani wanataka kuifanya, kuandika mchanganuo wa
biashara, kufanya mahesabu ya awali na kuweza kubadilisha maisha yao.
"Haya
ni majaribio ya awali ya elimu kwa umma na utafanyika katika mkoa wa
Dar es Salaam, Mbeya na Arusha, ikilenga jumla ya washiriki 300 kutoka
katika makundi matatu: Wanawake wa Tanzania asilimia 34, watu wenye
ulemavu asilimia 32 na watu wa kawaida mitaani asilimia 34," alisema.
Kwa hatua
nyingine, Ofisa mtendaji mkuu huyo wa FAIDIKA alidokeza kuwa, mbali na
kuwakopesha waajiriwa kama ilivyokuwa desturi yao, taasisi yake ya fedha
hivi karibuni itaanza kutoa mikopo kwa Wajasiriamali wadogo na wa kati,
taasisi ndogo za fedha, kukopesha kwenye biashara, na itakuwa
ikifanyakazi kwa ukaribu na watu wanaojituma, waaminifu na kujiamini
kuwa wanaweza kama ilivyo kauli mbiu yao ya ‘NAWEZA’.
Bi Moore
alibainisha kuwa wajasiriamali watakaopata mafunzo hayo pia wataingia
katika shindano la uandishi wa mchanganuo wa biashara, ambapo mshindi
atapokea zawadi ya pesa taslim itakayokuwa kama mtaji kwa mchanganuo huo
wa biashara ulioshinda.
Kwa niaba
ya washiriki wote wa mafunzo hayo, Mwenyekiti wa Kundi la wajasiriamali
walemavu (FAMASA disabled group), Lillian Kabalika, aliipongeza FAIDIKA
kwa kutambua umuhimu wa kuwasaidia watu wenye ulemavu kwa kuwapatia
elimu ya ujasiriamali bure.
No comments:
Post a Comment