Na Mwandishi Wetu
Bondia
Shabani Kaoneka sasa atapanda ulingoni juni 14 jumapili hii kukabiliana
na Cosmas Kibuga uzito wa kg 72 baada ya mpinzani wake wa mwanzo Said
Mbelwa kuingia mitini akizungumzia mpambano uho mwandaji Muhsin Shaliff
amesema kuwa maandalizi ya mpambano uho yamekamilika kwa asilimia 98
kufikia 100
mbali na mpambano uho wenye upinzani
mkali kutakuwa na michezo mingine itakayo wakutanisha Adam Ngange wa
Chanika na Mfaume Mfaume wa Manzese mpambano wa kg 61 mpambano
utakaofanyika katika ukumbi wa TASUBA uliopo Bagamoyo mjini
siku hiyo pia kutakuwa na bondia
Abdallah Pazi 'Mfalme wa wazalamu' atakaepambana na Mrisho Rajabu 'Dame'
wakati bondia kutoka Kiwangwa Bagamoyo Iddi Pialali 'Simba
aliyejeruiwa' atakumbana na Sweet Kalulu mpambano wa kg 63 raund sita
ngumi zingine zitawakutanisha Raymond Mbwago atapambana na Halidi Honga
siku hiyo pia kutapambwa nja burudani
kutoka kwa Jumanne Iddi pamoja na Sam wa Ukweli watakaopamba jukwaa hilo
kwa ajili ya burudani za muziki wa kizazi kipyaa
Katika mpambano huo siku hiyo kutakuwa
na uzwaji wa DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi kali pamoja na kutambua
sheria zake zikiwa na mabondia wakali kama vile
Floyd Mayweathar,Manny Paquaio, Saul 'canelo' alverez ,Mike Tyson,Mohamed Ali,Ferex Trinidad,Miguel Cotto na wengine wengi
pia kuta kuwa na vifaa vya mchezo
vitakaokuwa vikitolewa na Rajabu Mhamila 'Super D' kwa mabondia
watakaofanya vizuri siku hiyo na vingine kuuzwa kwa pesa taslimu na
kocha huyo kwa ajili ya kuamasisha