Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Monday, January 25, 2016

BONDIA FRANSIC CHEKA ATUA NCHINI NA KUMPIGIA MIKWALA MSERBIA GEARD AJOTOVIC

Bondia Fransic Cheka 'kulia' akizungumza na waandishi wa habari awapo pichani juu ya maandalizi yake ya mchezo wa ngumi ambapo aliweka kambi nchi ya Zambia kwa wiki mbili kwa ajili ya kumkabili Mserbia Geard Ajetovic
kwenye viwanja vya Leaders Club Februari 27 kushoto ni
meneja wake, Juma Ndambile wa Kampuni ya Advanced Security Limited Picha na SUPER D BOXING NEWS

Bondia Fransic Cheka 'kulia' akizungumza na waandishi wa habari awapo pichani juu ya maandalizi yake ya mchezo wa ngumi ambapo aliweka kambi nchi ya Zambia kwa wiki mbili kwa ajili ya kumkabili Mserbia Geard Ajetovic
kwenye viwanja vya Leaders Club Februari 27 kushoto ni
meneja wake, Juma Ndambile wa Kampuni ya Advanced Security Limited Picha na SUPER D BOXING NEWSNa Mwandishi wetu

Dar es Salaam.  Bondia  Francis Cheka amerejea nchini kutoka Zambia na kusema Mserbia Geard Ajetovic aiandae kupokea kipigo kikali katika pambano lao la mabara la uzito wa super middle la  Shirikisho la Masumbwi ya  Kulipwa Duniani (WBF).

Cheka na Ajetovic watapambana kwenye viwanja vya Leaders Club Februari 27 katika pambano lililoandaliwa na kampuni ya Hall of Fame Boxing and Promotion.

Akizungumza jana, Cheka alimpongeza  meneja wake, Juma Ndambile wa Kampuni ya Advanced Security Limited kwa kumwezesha kuweka kambi nje ya nchi ikiwa ni mara ya kwanza katika historia ya mchezo huo kwa upande wake.

Alisema kuwa Ndambile na kampuni yake imeonyesha kuwa wanajali na wanamalengo makubwa ya kumwendeleza kutokana na ukweli kuwa amekaa katika kambi ya kisasa yenye mabondia na makocha wazuri nchini Zambia.

“Kwanza naishukuru kampuni ya Advanced Security Limited kwa kufanikisha kambi hii, nimejifua vya kutosha nchini Zambia, mazoezi yalikuwa magumu na yalihitaji uvulivu mkubwa, kwa kutambua lengo langu ni nini, nilifanya kwa juhudu zote na sasa nipo tayari kwa pambano, hata kesho (leo) nipo tayari kwa bondia yoyote duniani,” alisema Cheka.

Alisema kuwa kutokana na siku kuwa nyingi, ataendelea na mazoezi hapa hapa nchini huku akisubiri mipango mengine ya meneja wake kwa upande wa maandalizi.

Meneja wa Cheka, Juma Ndambile ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Advanced Security Limited alisema kuwa  lengo la kampuni yao ni kufanya mapinduzi na kuleta maendeleo katika mchezo wa ngumi za kulipwa hapa nchini.

Ndambile alisema kuwa Cheka ni bondia mwenye kipaji na hakuwa tayari kuona kipaji hicho kinapotea na kuchukua jukumu la kumwendeleza. “Mimi na kampuni yangu tuna mipango ya kuwamiliki mabondia wengi hapa nchini, kama ilivyo kwa Cheka, nao watapata fursa ya kufanya mazoezi nje ya nchi na kupata mapambano ya kimataifa ya ubingwa ili kuiletea sifa taifa,” alisema Ndambile.

Alisema kuwa wanataka kutumia vizuri fursa waliyopewa na WBF ambayo inamtaka Cheka ashinde pambano hilo ili aweze kuwania ubingwa wa Dunia hapa hapa nchini.

2 comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...