Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Sunday, January 24, 2016

BONDIA VICENT MBILINYI AENDELEA KUJIFUA NA KUTAFUTA WAPINZANI


VICENT MBILINYI KG 63 TANZANIA 2016

Bondia Vicent Mbilinyi akielekezwa jinsi ya kutupa makonde wakati wa mazoezi yake yakawaida Picha na SUPER D BOXING NEWS
Na Mwandishi Wetu
BONDIA Vicent Mbilinyi amendelea kujifua baada ya kumchakaza bondia mkongwe wa siku nyingi Deo Njiku sasa anaendelea na mazoezi ya nguvu kwa aji ya kuwasambalatisha mabondia wengine watakaopita mbele yake

bondia huyo mpaka sasa ameshacheza michezo tisa na kushinda 7 kupoteza  na droo 1 ambapo imemuweka katika rekodi nzuri ya mchezo uho kwa mwaka jana

akizungumza na mwandishi wa habari hizo Mbilinyi amesema kwa sasa yupo fiti kucheza na mtu yoyote kwa keshaiva kikamilifu baada ya kupata mazoezi ya aina mbalimbali yanayo mjengea kujiamini katika mchezo wa masumbwi akiwa chini ya kocha wa kimataifa wa mchezo uho Rajabu Mhamila 'Super D'

aliendelea kwa kusema kuwa nilingia katika ngumi za kulipwa kama najitolea lakini siku zinavyozidi kwenda ndio najijengea mashabiki na kujulikana zaidi katika mchezo niupendao hivyo na ahidi sito waangusha na wala sito lewa sifa wanazonipa nitaendelea kujifua ili niendelee kupambana zaidi katika mchezo

nae kocha anaemnowa bondia huyo Super D amesema kuwa Mbilinyi ana moyo wa kufika mbali hivyo ameonesha nia ya kucheza mchezo uhu katika mazingila magumu hivyo kwa mwaka 2016 ni wake wa kutoka katika mchezo wa ngumi

na naisi katika uzito wake kwa sasa akuna wa kumsumbua kwa sababu amekutana na mabondia wa lika zote ambao wanatamba na waliotamba

Kocha Rajabu Mhamila 'Super D' kwa sasa anawasimamia mabondia wake akiwemo Ibrahimu Class 'King Class Mawe' Shabani Kaoneka, Shomari Milundi, Vicent Mbilinyi Mwenyewe na mwanadada Lulu Kayage ambao wote wapo chini ya Super D Boxing Promotio ambayo kazi yake kubwa ni kuwafundisha na kuwatafutia mipambano mbalimbali  ya nje na ndani

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...