Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Thursday, May 5, 2016

NSSF ILIVYOSHIRIKI MEI MOSI KITAIFA MKOANI DODOMA



Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Prof. Godius Kahyarara (katikati waliokaa), Mkurugenzi wa Uendeshaji wa NSSF, Crescentius Magori (kulia) na Meneja Kiongozi Masoko na Uhusiano wa NSSF, Eunice Chiume (kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa NSSF nje ya Ofisi ya Mkoa wa Dodoma wakati wa sherehe za Sikukuu za Mei Mosi zilizofanyika kwenye Uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Prof. Godius Kahyarara (kulia), Mkurugenzi wa Uendeshaji wa NSSF, Crescentius Magori na Meneja Kiongozi Masoko na Uhusiano wa NSSF, Eunice Chiume na Meneja wa NSSF Mkoa wa Dodoma, Rehema Chuma wakati wa sherehe za Sikukuu za Mei Mosi zilizofanyika kwenye Uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma.
Rais John Magufuli (wa pili kushoto) akishiriki kuimba wimbo wa mshikamano na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa (kulia), Rais wa Shirikisho la vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), Gratian Mukoba (wa pili kulia) na Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu , Jenista Mhagama wakati wa kilele cha sherehe za Sikukuu za Mei Mosi zilizofanyika kitaifa mkoani Dodoma.
Wafanyazi wa NSSF wakiwa na bango lao.
Wafanyakazi wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), wakipita kwa maandamano mbele ya mgeni  rasmi Rais John Magufuli (hayupo pichani), katika kilele cha Sherehe  za Mei Mosi zilizofanyika kitaifa mkoani Dodoma. 
 Wafanyakazi wa NSSF wakiwa katika Mei Mosi.
 Maandamano ya wafanyakazi wa NSSF yakipita mbele ya mgeni rasmi Rais John Magufuli (hayupo pichani) katika sherehe za Siku ya Wafanyakazi Duniani Mei Mosi.
 Wafanyakazi wakiwa katika maandamano.
 Wafanyakazi wa NSSF wakiingia kwa maandamano.
 wafanyakazi wakiwa katika sherehe za sikukuu ya Mei Mosi.

 Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Prof. Godius Kahyarara (kulia), Meneja wa NSSF Mkoa wa Dodoma, Rehema Chuma,  Meneja Kiongozi Masoko na Uhusiano wa NSSF, Eunice Chiume na Mkurugenzi wa Uendeshaji wa NSSF, Crescentius Magori wakitoka bada ya kumalizika kwa sherehe za Sikukuu ya Mei Mosi iliyofanyika kwenye Uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma.

MABONDIA KUTOKA ZANZIBA WASAINI KUZIPIKA KATIKA 'USIKU WA MAHAVY WEIGHT'


Bondia wa uzito wa juu nchini kutoka Zanzibar Ashiraf Selemani katikati akitia saini mkataba wa kuzichapa na bondia kutoka Thailand June 4 mpambano utakaofanyika uwanja wa ndani wa Taifa kulia ni bondia Amour Mzungu nae kutoka Zanzibar akushudia kulia ni Anton Rutta katibu mkuu wa shilikisho la ngumi za kulipwa nchini PST akishudia Picha na SUPER D BOXING NEWS

ASHIRAF AKISAINI MKATABA WA KUZIPIGA JUNI
Bondia Amnour Mzungu akisaini mkataba wa kuzipiga na Japhert Kaseba kugombania ubingwa wa U.B.O Afrika June 6





BONDIA AMOR MZUNGU
BONDIA AMOR MZUNGU

Airtel yatoa Fursa za Ajira kwa wanafunzi katika vyuo vikuu mbalimbali nchini

Meneja Rasilimali watu wa Airtel, Bi, Gabriella Kaisi (kulia) akiwapongeza James Kwayu (katikati) na Abubakar Nassor ambao ni wanafunzi wa vyuo waliofaidika na aiira katika kampuni ya Airtel kupitia ushirikiano kati ya Airtel na chama cha wanafunzi vyuoni  Tanzania AIESEC  wenye lengo la kuwawezesha vijana walioko vyuoni kupata ajira katika makampuni mbalimbali kila mwaka.
 xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
· Airtel yatoa ajira kwa wanafunzi wenye vipaji katika vyuo vikuu
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imedhamini kongamano la ajira  kwa vijana wa chuo kikuu linaloandaliwa na AIESEC Tanzania  lenye lengo la kuwaweka pamoja waajiri (makapuni) na waajiriwa watarajiwa (wanafunzi)  kwa lengo la kuwapatia Fursa zitakazowasaidia katika kuendesha shughuli za kiuchumi.
Kila Mwaka AIESEC huandaa kongamano la ajira kwa vijana linaloshirikisha wanafunzi zaidi ya 1500 kutoka katika vyuo vikuu mbalimbali nchini. Kuanzia mwaka jana Airtel imejikita na kushiriki  katika kongamano hilo ikiwa ni sehemu ya kuendeleza dhamira yake ya kuwawezesha vijana wanaohitimu vyuoni kupata ajira.
Akiongea kuhusu mpango huo, Meneja Rasilimali watu wa Airtel , Gabriella Kaisi alisema”Tunayofuraha kuwa sehemu ya mpango huu kwa kushirikiana AIESEC Tanzania lengo likiwa ni kuwafikia na kuwaajiri vijana wenye vipaji kutoka katika vyuo vikuu mbalimbali nchini. Tunaamini kila kijana ana nafasi ya kufikia ndoto zake  na ndio mana tunatoa fursa  kwa vijana kufanya kazi pamoja nasi. 
Mwaka jana tuliwawezesha vijana watatu wahitimu kutoka vyuo vikuu vya IFM pamoja na chuo kikuu cha Dar es salaam kupata ajira katika ofisi zetu za Airtel. Vijana hao ni pamoja na Abubakar Nassor ambaye anafanya kazi katika kitengo cha masoko James Kwayu yuko katika kitengo cha Huduma kwa wateja na Gerald Msafiri anafanya kazi katika kitengo cha mauzo.
Vijana hawa watapata nafasi ya kwenda kufanya kazi nje ya nchi katika makao makuu ya Airtel  nchini Kenya na India  kwa muda wa mienzi miwili kuanzia mwezi wa Mei hadi Julai 2016. Watakaporudi watapangia kufanya katika vitengo tofauti ili kupata uzoefu na mwanga zaidi aliongeza Kaisi
Akiongea kuhusu program hiyo, moja kati ya waliofaidika na mpango katika kitengo cha masoko, Abubakar Nassor alisema” najisikia furaha kuwa mwanachama wa AIESEC Tanzania kwani kumeniwezesha kupata fursa hii adimu ya ajira, uzoefu katika kazi na nafasi ya kujifunza katika kampuni kubwa ya simu duniani. Nimejipanga vyema kujifunza zaidi katika miezi 2 nitakayokuwa  nchini India na Nairobi,   nahaidi kuitumia fursa hii vyema ili kuweza kuzifikia ndoto zangu
Mwaka huu Airtel imejipanga kuendelea kuwafikia vijana wengi zaidi kwa kutoa ajira kwa vijana wengine watano ambao watafanya vizuri na kufaulu mitihani mbalimbali inayoendelea kwa sasa.  

Airtel itatangaza majina ya wanafunzi wengine watakaofudhu na kuchaguliwa kwa mwaka huu mara baada ya hatua za uajiri zitakapokamilika.

ZIFF 2016 WAMETANGAZA MAJINA YA FILAMU KALI ZITAKAZOSHINDANISHWA KATIKA TAMASHA HILO



Tamasha la filamu la Zanzibar (ZIFF) limetangaza majina ya filamu zitakazoshindanishwa hapo ifikapo Julai 9 hadi 17. Tamasha lilipokea jumla ya filamu 490 kutoka nchi 32 mwaka 2016.
Jopo la wachaguzi limependekeza filamu 80 ndio zitakazoshindanishwa katika makundi matano maalum: Kundi la Kawaida 59, Sembene Ousmmane 15, filamu 12 Bongo movies.  Nyingine 5 ni la kundi jipya kabisa la filamu zinazoizungumzia Zanzibar itakayopata tuzo ya Emerson.
Kutakuwepo pia mashindano ya Video za Muziki ambazo zitatangazwa mwisho wa mwezi Mei na hizi zitaoneshwa katika maonyesho yanayofanyika katika Ngome Kongwe.
Jambo la kukumbukwa zaidi mwaka huu nikuongezeka kwa jumla ya filamu za kitanzania katika mashindano. Filamu zaidi ya 40 zilitumwa kwa mashindano kwa ujumla na mwaka huu filamu 5 za kitanzania zitashindanishwa katika jopo la Ousmane Sembene kati ya filamu 17.
Kwa ujumla filamu toka Afrika mashariki zinazoingia katika mashindano zimeongezeka pia ambapo kuna 8 toka Tanzania, Kenya 5, Uganda 3 na Rwanda 2.
Mwaka huu kutakuwa na filamu 3 ambazo zitaoneshwa kwa mara ya kwanza duniani  katika tamasha la ZIFF. Filamu hizi zimedhaminiwa na Shirika la Ushirikiano wa Kimataifa la Ujerumani (GIZ) wakishirikiana na ZIFF. Washindi watatu wa shindano la Sembene Ousmane mwaka 2015 walipewa $2000 kila mmoja kuwawezesha kutengeneza filamu mpya katika kipindi cha mwaka na kuzituma tena ZIFF kwa kushindanishwa na nyingine.
Mvuto wa tamasha unazidi kukua ukiangalia kuongezeka kwa nchi zinazotuma filamu. Mwaka huu Estonia na Albania zimetuma filamu zikiungana na nchi nyingine kama Bangladeshi, Finland, Trinidad and Tobago, Bermuda na nyinginezo.
ZIFF pia inaendeleza mchango wake katika tasnia ya filamu kwa kutayarisha warcha maalum juu ya utengenezaji filamu. Mwaka huu ZIFF imetangaza warsha mbili. Ya kwanza ni juu ya matumizi bora ya Camera ya Canon D5 itakayoendeshwa na Barry Braverman toka Marekani ,aliyeifanyia kazi Panasonic na Sony katika kujaribisha vifaa vyao.
Warsha nyingine ni ile itakayodhaminiwa na Goethe Institute ya Ujerumani itayofunza watoto wa shule ufundi wa kutengeneza vikaragosi katika filamu. Hii inatokana na kutambua nafasi ya sanaa katika kukuza vipaji na kuwatayarisha watoto wasanii kwa ajira, uadilifu na ubunifu.
Kwa maelezo zaidi na kupata listi ya filamu zilizochaguliwa tembelea tovuti ya www.ziff.or.tz  na pia tafadhali tu-like katika Facebook

MSANII SNURA MUSHI AJITOKEZA KUOMBA MSAMAHA MBELE YA WATANZANIA KWA VIDEO YAKE YA 'CHURA' KUKIUKA MAADILI YA KITANZANIA

 Msimamizi wa kazi zake Bwana Hemed Kavu maarufu kama HK (kushoto) akisoma taarifa ya Snura Mushi kuomba msamaha kwa Watanzaniaya kutokana na kusambazwa kwa video ya msanii huyo iliyokiuka maadili ya Kitanzania maarufu kama ''Chura'' mara alipokutana na Waandishi wa Habari leo jijini Dar es Salaam.
      PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA-MAELEZO.

Msanii wa kizazi kipya Snura Mushi (kulia) akiomba msamaha mbele ya Watanzania kutokana na kusambaza video yake iliyokiuka maadili ya Kitanzania maarufu kama ''Chura'' mara alipokutana na Waandishi wa Habari leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Msimamizi wa kazi zake Bwana Hemed Kavu maarufu kama HK

NA KHADIJA KALILI

Ikiwa  ni siku moja tu tangu Wizara ya Habari , Utamaduni Sanaa na Michezo  jana kutangaza  kumfungia msanii  Snura Mushi  kujihusisha na masuala ya sanaa  ikiwemo kutumbuiza kutokana nawimbo wake wa Chura ambao aliusambaza kwenye mitandao ya kijamii You tube, WhatsApp na mingine mingi kutokana na kurekodiwa kinyume na maadili ya Mtanzania.

Ndipo leo asubuhi Snura alipoibukia kwenye Ukumbi wa mikutano wa Idara ya Habari MAELEZO,Jijini  Dar es Salaam na kuzungumza na vyombo mbalimbali vya habari.

Baada ya kuwasili ukumbini na kutambulishwa Snura alianza kwa kusema "Karibuni  ndugu zangu  waandishi wa habari , naitwa Snura Anthony Mushi  wengi  wananifahamu  kwa jina la  kisanii  Snura,  na kulia kwangu  ni msimamizi  wa kazi zangu  za sanaa 'Meneja' wangu Hemed Kavu almaarufu  kwa jina la HK.

Kwanza  tunatanguliza shukrani  zetu za dhati  kwa kuitikia wito huu:
"Tumewaita hapa leo kwa ajili  ya kuomba  radhi  umma wawatanzania  kwa ujumla  kwa kosa l;a  kutengeneza , kuzindua  na kuweka  mtandaoni video ya udhalilishaji  wa  mwanamke  isiyozingatia  maadili  ya kitanzania ya muziki unaoitwa 'Chura' alisema Snura.

"Tunaviomba radhi  vyombo vya serikali  vinavyosimamia  sekta  ya sanaa kwa  kutofuata  sheria , kanuni na taratibu zilizopo  katika  uendeshaji wa sanaa nchini".

"Mimi na Meneja wangu  tunaahidi  kutorudia  tena kufanya  tukio  hilo la udhalilishaji , na iwapo  tutarudia  basi tupewe adhabu  kali kwa mujibu wa sheria za nchi hii" alisema Snura.

 Aliendelea kwa kusema kuwa  "pia tunaahidi  kuwa mfano bora  kwa jamii  inayowazunguka   na kwa wasanii  hususan katika masuala yahusuyo  kutunza na kufuata  maadili  na utamaduni  wetu pamoja na  sheria za nchi. Hii ni pamoja na  kupata vibali  katika  mamlaka na taasisi zinazohusika".

Katika hali isiyokuwa ya kawaida pia Snura amekiri kuwa alikua akifanya shughuli zake  za sanaa bila ya kuwa  na usajili  Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA).

"Tunafahamu kwamba baadhi ya wasanii hususan wa  muziki wa kizazi kipya  hawajajisajili   BASATA  kama ilivyokuwa kwangu mimi  lakini kwa sasa  baada ya  kupata maelekezo  kutoka (BASATA), nimeshapata usajili  na sasa natambulika kisheria.
    
Snura aliweka wazi kuwa yeye binafsi aliitwa  Wizarani na kuhojiwa kuhusu wimbo wake wa Chura hivyo  alitambua kwamba utafungiwa akagundulika hakuwa na usajili  BASATA.

Alisema sharti la kwanza alilopewa ilikuwa ni kuitoa video  ya Chura kwenye mitandao ya kijamii  You Tube  kutokana na namna ilivyorekodiwa." Tayari  hili limeshatekelezwa  na video imeshafutwa kwenye akaunti hiyo. alisema HK.

Pia tayari Snura ameshasajiliwa BASATA  hivyo yuko huru kufanya kazi  katika maonyesho  yake ya sanaa .

Akizungumzia kuhusu sharti la tatu  ni  kuiirekodi upya  video  na muziki ya Chura.

KWANINI CHURA  IMEMDHALILISHA SNURA?

Kwa mujibu wa Snura anakiri ni kutokana na kiwango kidogo cha elimu alicho nacho pia upeo wake wa kufikiria ndiyo ulifikia ukomo hivyo asamehewe.

"Mimi sikuwa na lengo la kuwadhalilisha  wanawake wenzangu kukatika viuno hapa kwetu ni jadi na mimi mwenyewe nacheza , kuhusu nguo kulowekwa maji  alisema kuwa wale walivaa mitandio na walilowa maji huku akisisitiza kuwa waliona mazingira ya maisha ya Chura ni kwenye maji hivyo wao waliona sawa kujitumbukiza kwenye maji.
 
"Lakini jiliporudi nyumbani  na kuiangalia vizuri video ya Chura nikaona ina makosa ndiyo maana sikuisambaza kwenye Luninga yoyote" alisema Snura.

Mwisho msanii huyo  pamoja na Meneja wake  wametoa shukrani  za dhati  kwa Wizara  ya Habari , Utamaduni , Snaa na Michezo  pamoja na BASATA kwa ku maelekezo  na elimu  waliyowapatia.

Juku wakiahidi  kufanya kazi  na kuwa mabalozi  wema kama walivyoagizwa.

   

"Hivi sasa tunaufanyia masahihisho wimbo wa Chura  pamoja na video yake na baada ya hapo utaangaliwa na Bodi ya Filamu

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...