Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Tuesday, September 4, 2018

MBILINYI ANG'AKA KUPAKAZIWA ASISITIZA ANACHEZA TAIFA SEPTEMBA 15


Na Mwandishi Wetu


BONDIA machachali nchini Vicent Mbilinyi anatarajia kupanda ulingoni Septemba 15 katika ukumbi wa uwanja wa ndani wa taifa kuzipiga na Saidi Kidedea mpambano wa raundi 6 ambambo watakuwa wakisindikiza mpambano wa Fred Sayuni na Haidari Mchanjo

akizungumzia mpambano uho Mbilinyi amesema amejiandaa vya kutosha hivyo wamewataka mashabiki wake wasiwe na wasiwasi na maandalizi yake kwani yupo vizuri kila idara na anachotaka yeye ni ushindi wa K.O ya mapema ili asiwasumbuwe majaji watakaokuwepo siku hiyo

aliendelea kwa kusema kumeibuka n mapromota matapeli ambao wametengeneza mabango na kuweka picha yangu mimi na Cosmas Cheka kuwa nacheza siku hiyo mimi kama mimi ni bondia ninae jijua waeamuwa kunipaka matope na kuaribiana tu mimi sina mpambano na Cheka pambano ninalolijua mimi ni la taifa ninacheza na Saidi Kidedea ambapo nimesaini kwa Super D Boxing Promotion ambao ndio nimesaini nao kwa sasa

nae mratibu wa mpambano huo Rajabu Mhamila 'Super D' kutoka kampuni tanzu ya kizalendo ya Super D Boxing Promotion iliyo jizatiti kuendeleza shughuli za mipambano ya masumbwi nchini  alisema  mbali na pambano hilo rinalosubiliwa na mshabiki lukuki siku hiyo pia kutakuwa na mapambano mengine ya kukata na shoka ambapo bondia Abdallah Pazi 'Dula Mbabe' atakumbana na George Dimoso wakati Mohamedi Kashinde ata vaana na Sadiki Momba na Issa Nampepeche atakabiliana na Faraji Sayuni na Bakari Mbede atakutana uso kwa uso na Frenk John

mapambano hayo yote na mengine yataanza saa 12 jioni yani itakuwa mapema ili ngumi hizo ziishe kwa wakati uliopangwa 

siku hiyo pia kutakuwa zikiuzwa DVD mpya za masumbwi ambazo zinaonesha mafunzo mbalimbali ya mchezo wa ngumi yanavyoanza hatua kwa hatua

mpaka kujua kitu kamili katika

mchezo huo pia kunakuwa na mapambano ya mabondia mabigwa wa dunia wa mchezo huo kama Floyd


Maywether, Manny Paquaio,mike Tyson, Mohamed Alli pamoja na mabambano ya ngumi ya ndani zilizo taharishwa na kocha maili wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' ambaye anajishughulisha na uzaji wa vifaa mbalimbali vya ngumi nchini

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...