Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, April 17, 2019

NGUMI MZIKI KUPIGWA SIKU YA PASAKA KATIKA UKUMBI WA CCM MWINYIMKUU MAGOMENI
Na Mwandishi Wetu

ZIKIWA zimebakia siku chache kabla ya mpambano wa masumbwi uliokuwa ukisubiliwa kwa hamu na mashabikji lukuki wa mchezo wa ngumi nchini Tanzania utakaofanyika April 21 siku ya sikukuu ya Pasaka katika ukumbi wa CCM Mwinyimkuu

Msanii chipkizi wa wa kizazi kipya David James 'Level Lizze' kutumbuiza wapenzi na mashabiki wa mchezo wa ngumi watakaokuja siku hiyo msanii huyo anaetamba na vibao vyake kadhaa vikiwemo umeni control kingine nimechelewa na bas nipe msanii huyo ameahaidi kukonga nyoyo za mashabiki watakaokuja katika mtanange uho utakaowakutanisha

Hussein Pendeza na Juma Ramadhani Choki siku ya April 21  Pasaka Day
Mpambano uho ulioandaliwa na Promota wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' amesema kuwa pambano hilo litafanyika siku ya sikukuu ya pasaka likiwa limepewa nguvu na 

Bondia Mtanzania Omari Kimweri 'Lion Boy 'anaefanya shughuli zake nchini Australia  na Ibrahimu Class 'King Class Mawe' anaefanya shughuli zake Marekani U.S.A  Mabondia hwo ndio waliotia nguvu kwa ajili ya mtanange huo kufanyika  siku hiyo kwa kuwa vijana wanatakiwa kuendeleza rekodi zao za masumbwi kila wakati ndio mana akaongeza nguvu ili mpambano uho ufanyikeSuper D aliongeza kwa kusema kuwa mbali na pambano hilo siku hiyo kutakuwa na mapambano mbalimbali yatakayokuwa yanafanyika siku hiyo ambapo bondia  Idd
Mkwera ataoneshana umwamba na Rojas Masamu na  Shomari Milundi ataoneshana umwamba na Bakari Mbede wakati ibrahimu Makubi atavaana na Haruna Ndalo na Ramadhani Mbegu 'Migwede' atakabiliana na Rashidi Mnyagatwa na Salum Tandu zidi ya Gerald Mkude na Sunday Kiwale 'Moro Best' atalindima na Luckman Ramadhani Vicent Mbilinyi na Shabani Mbogo Hussein Shemdoe na Shehe Azizi na Ahmadi Kombo atakumbana na Sandali Nyambala

Mapambano yote hayo yanaletwa kwenu na kampuni tanzu ya kizalendo ya Super D Boxing Promotion ambayo ipo nchini Tanzania kwa ajili ya kuinuwa vipaji ya vijana mbalimbali ili kuendeleza vipaji vyao pendwa


na kupitia kampuni ya Super D Promotion imejizatiti kuweka angalau pambano moja kila baada ya miezi milili ili kuwasaidia vijana mbalimbali kukuza vipaji vyao na kujiendeleza kupitia mchezo uho wa masumbwi nchini

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...