Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Friday, December 30, 2011

SIMBA KUKIPIGA NA MTIBWA SUGAR MCHEZO MAALUM WA KUUAGA NA KUUKARIBISHA MWAKA 2012


Mashabiki wa Simba, wakishangilia katika moja ya mchezo wa timu yao Uwanja wa Taifa.

KLABU ya soka ya Simba itacheza mechi ya kirafiki dhidi ya Mtibwa Sugar ya Morogoro katika pambano litakalofanyika katika Uwanja wa Azam, Chamazi jijini Dar es Salaam JIONI ya Jumamosi, Desemba 31 mwaka huu.

Pambano hilo litakuwa la mwisho kwa Simba kucheza jijini Dar es Salaam mwaka huu. Pambano hilo pia litakuwa la mwisho kwa Simba kabla haijakwenda Zanzibar kushiriki michuano ya Kombe la Mapinduzi iliyopangwa kuanza Januari 2 mwakani.

Simba itaondoka Dar es Salaam kwenda Zanzibar Januari Mosi mwaka huu (Jumapili).

Pambano dhidi ya Mtibwa litakuwa sehemu ya maandalizi ya michuano ya Mapinduzi, Ligi Kuu ya Tanzania na michuano ya kimataifa ambayo Simba itashiriki mwakani.

Mechi hiyo itakuwa ya kwanza kwa Kocha Mkuu wa Simba, Profesa Milovan Cirkovic, kukaa kwenye benchi la ufundi na kuiongoza klabu yake hiyo ambayo ni mabingwa watetezi wa Kombe la Mapinduzi na mabingwa wa kihistoria wa Kombe la Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati.

Viingilio katika pambano hilo vitakuwa ni Sh 5,000 kwa VIP na 2,000 kwa majukwaa mengine. Simba imeweka kiingilio hicho ili kuwawezesha wananchi wengi zaidi kuhudhuria pambano hilo na kusherehekea kumaliza mwaka salama huku wakiitazama soka la uhakika.

Profesa Cirkovic ameahidi kwamba kwenye pambano hilo atashusha kikosi kamili cha wachezaji wa Simba ili kubaini ni kwa namna gani wachezaji wake wameyaelewa mafunzo yake.

“Nawakaribisha wapenzi na wanachama wa Simba na wapenda soka kwa ujumla waje kwa wingi kuiona Simba ikicheza. Nimesikia kwamba uwanja wa Azam ni mzuri na utaendana na aina ya mchezo ambao Simba itakuwa ikiucheza chini yangu. Nataka kuonyesha soka la asili la Simba,” alisema.

MTANGAZAJI WA TBC TAIFA HALIMA MCHUKA AFARIKI DUNIA


Rais Jakaya Kikwete na mkewe, Mama Salma, wakimjulia hali aliyekuwa mtangazaji wa TBC Taifa, Halima Mchuka wakati wa uhai wake alipokuwa amelazwa hivi karibuni.

Halima amefariki dunia usiku wa kuamkia leo baada ya jana kuugua ghafla, alipoanza kujisikia vibaya mara tu baada ya kumaliza kipindi cha salam cha mchana na kupelekwa Hospitali.

Kufuatia kifo hicho, KLABU ya soka ya Simba ya Dar es Salaam inatoa salamu za rambirambi kwa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) na tasnia ya habari kwa ujumla kufuatia kifo cha aliyekuwa mtangazaji maarufu wa michezo nchini, Halima Mchuka, aliyefariki usiku wa kuamkia leo
Jina la Halima Mchuka ni maarufu kwa wanamichezo si Tanzania pekee bali ukanda mzima wa Afrika Mashariki na Kati kwa vile yeye aliweka historia ya kuwa mwanamke wa kwanza kutangaza mchezo wa soka redioni.
Katika enzi za uhai wake, Halima alifanya kazi kwa karibu na klabu ya Simba, akitembelea ofisi za makao makuu mtaa wa Msimbazi kwa ajili ya kutafuta taarifa mbalimbali za kimichezo.

Simba itaukumbuka daima mchango wa Halima Mchuka kama mwanahabari, mwanamichezo na mtu ambaye alivutia wanawake wengi kupenda mchezo wa soka na pia kazi ya utangazaji na uandishi wa habari kwa ujumla.
Mwenyezi Mungu aiweke roho ya marehemu mahali pema peponi. Amen.

Imetolewa na
Ezekiel Kamwaga Ofisa Habari
Simba Sports Club
0772 01 72 47

Thursday, December 29, 2011

WACHEZAJI WA TENIS WAJIFUA KWA AJILI YA MICHUANO YA VIJANA

Kocha wa mchezo wa Tenis, Ismail Omari akiwaelekeza wachezaji Joyria Ismail na Srah Bura wakati wa mazoezi leo
Mchezaji wa Tenesi Joyriia Ismail akipiga mpira wakati wa mazoezi leo



Mchezaji wa Tenis Sarah Bura akipiga mpira


ZUGO GYM YAPANIA KUINUA VIJANA KATIKA MASUMBWI






Kocha wa ngumi wa timu ya Zugo GYM ya Gongo la Mboto, Mbaruku Heri (kushoto), akimfundisha bondia Abedi Zugo, jinsi ya kurusha masumbwi Dar es Salaam jana, wakati wa mazoezi ya kujiandaa kucheza na Juma Mohamedi. (Picha na http://www.superdboxingcoach.blogspot.com/

SUPER D BOXING COACH KUENDELEA KUWANOA VIJANA ZAIDI 2012

Super D Boxing Coach kushoto akiwa katika moja ya GYM

super D Boxing Coach




Super D Boxing Coach Akiwa na Talik Balozi wakati wa mazoezi yanayoendelea katika kambi ya Ilala





mazoezi ni Afya akisisitiza Super D Boxing Coach



Super D Boxing Coach akiwa na mwanae Ikota anaefuata nyayo za masumbwi



Na Mwandishi WetuALIYEKUWA bondia wa ngumi za kulipwa Rajabu Mhamila 'Super D' ambaye pia ni kocha wa timu ya ngumi ya Ashanti Ilala amesema anajivunia mafanikio makubwa aliyoyapata katika mchezo wa ngumi katika kipindi cha mwaka 2011.Akizungumza na waandishi wa habari Super D ambaye pia ni mpiga picha wa Magazeti ya Busines Time, Majira, Sports Starehe na jarida la Maisha alisema moja ya mafanikio ni kuwaandaa vijana chipukizi wengi na kuwafikisha katika kiwango kizuri cha kuvuna matuna ya mchezo huo.Alisema pamoja na hilo pia ameweza kushirikiana vema na wadau wa ngumi pamoja na mapromota mbalimbali wanaoandaa mapambano makubwa kwa kutoa mchango wake wa vifaa vya ngumi ili kufanikisha mapambano mbalimbali yaliyofanyika katika kipindi cha mwaka huu.Katika hatua nyingine Super D amekua akitoa mafunzo ya mchezo wa ngumi pamoja na kutambua sheria mbalimbali kwa njia ya DVD zikisambazwa na kocha wa mchezo huo mkoa wa kimichezo wa Ilala 'Super D' kwa ajili ya kuwapa mambondia mbalimbali mbinu za mchezo na mashabiki kujua sheria za masumbwi.Ndani yake wakiwemo mabondia Floyd Mywether, Manny Paquaio, Amiri Khanny, Mohamedi Ali, Mike Tayson David Haye na wengine ambapo kutakuwa na matukio ya mazoezi yao katika mataifa yao ikumbukwe kuwa ni mabingwa wa dunia. na kutakuwa na mapambano makubwa matano ya utangulizi.Alisema mipango yake kwa mwaka 2012 ni kuhakikisha anaendelea kuwainua mabondia wengine chipkizi akiwemo bondia Shomari Mirundi na Ibrahimu Class ambao amewataja ni mabondia wazuri wanaohitaji kuendelezwa vipaji vyao.Alisema bondia Ubwa Salum ambaye alimtwanga Mustapha Doto,kwa pointi 60-57 alishinda ambapo pambano hilo lilikuwa moja ya mapambano ya utangulizi ya pambano kubwa la Rashidi Matumla na Maneno Osward lililofanyika DEsemba 25 mwaka huu.
Superd Boxing Coach

Wednesday, December 28, 2011

NETIBOLI HIYO ZANZIBAR KUSHIRIKI KOMBE LA MAPINDUZI










T


Timu ya netiboli inayounda kikosi cha timu ya Taifa inaondoka kesho kuelekea visiwani ZANZIBAR kushiriki mashindano ya kombe la Mapinduzi ambapo kikosi hicho kitakuwa chini ya kocha MARY PROTAS na kocha kutoka TANZANIA VISIWANI.



Baadhi ya timu zilizoambwa kushiriki mashindano hayo ni ZAMBIA, BOTSWANA, MALAWI, NAMIBIA ,KENYA na UGANDA.



Mjumbe wa kamati ya utendaji wa CHANETA MWAJUMA KISENGO amesema timu hiyo itafanya vizuri kwani ndiyo timu iliyoshiriki mashindano ya ALL AFRICANS GAME nchini MSUMBIJI.

Hamad rashid agoma kuhojiwa na kamati ya mahadil cuf













Raymond Kaminyoge na Aziza Masoud

HALI bado tete ndani ya Chama Cha Wananchi (CUF) baada ya Mbunge wa Wawi, Hamad Rashid Mohamed, kugoma kuhojiwa na Kamati ya Nidhamu na Maadili ya chama hicho kuhusu tuhuma za kuvunja katiba. Mbunge huyo aliibua tuhuma nzito kwamba amekamata waraka wa siri wa viongozi wawili waandamizi wa chama hicho, waliokuwa wakipanga njama za kumfukuza.



Hamad aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa ana sababu tano za kugomea kikao hicho, ambazo ni pamoja na waraka huo wa siri aliodai ulitoka kwa mmoja wa viongozi hao kwenda kwa mwenzake. Waraka huo ambao Hamad alidai kuunasa unasomeka, “Tuwe waangalifu tusiingie katika mtego” na uliandikwa Desemba 14 2011 na kutumwa kwa barua pepe.



“ …anataka nifukuzwe kwenye chama, baadhi walioteua na walioteuliwa katika Kamati ya Nidhamu na Maadili wamekwishanituhumu hadharani na kunitia hatiani hivyo kikao hiki hakitatenda haki,” alisema Hamad.



Alitaja sababu nyingine ya kukataa kuhojiwa kuwa ni kutoelezwa tuhuma zake hasa vifungu vya Katiba alivyodaiwa kuvikiuka. “ Ni vema nikaelezwa ni vifungu vipi vya katiba hiyo nilivyokwenda navyo kinyume,” alisema Hamad. Alifafanua kwamba, alitaka apewe hadidu za rejea za kikao kilichounda Kamati ya Nidhamu na Maadili kwa sababu kikatiba, hakuna chombo kama hicho.



“Katiba ya CUF haina chombo kama hicho, kamati hii imeundwa na nani nikipewa hadidu za rejea za kikao kilichounda kamati hiyo zitanisaidia katika kumbukumbu,” alisema Hamad Rashid. Alisema alitaka pia apewe nakala ya uteuzi wa wajumbe walioteuliwa katika kamati hiyo.



Mbunge huyo pia alisema amegomea kikao hicho hadi atakapopewa kanuni zitakazotumika katika kuendesha shughuli nzima ya kujibu tuhuma hizo na kupewa katiba iliyotumika ambayo ameivunja. “Nataka kupewa vitu hivyo ili niweze kuweka kumbukumbu sahihi kwa kila hatua inayochukuliwa na chama,” alisema mbunge huyo wa CUF.



Akizungumzia kamati hiyo, mbunge huyo alisema kati ya wajumbe wanane, watano hana imani nao kwa sababu wamekuwa wakimtuhumu hadharani. “Hawa wajumbe sina imani nao uamuzi wao hautakuwa wa haki,” alisema Hamad. Juzi Hamad Rashid na wenzake 13 waliitwa na Kamati na Nidhamu ili kujibu tuhuma za kuvunja Katiba ya chama hicho. Hatua hiyo imekuja baada ya mvutano wa muda mrefu kati ya Katibu Mkuu na Mbunge huyo kutuhumiana hadharani.



Waraka wa Siri

Hamad alisema hawezi kuhudhuria kikao hicho kwa kuwa tayari amebaini njama za kushughulikiwa zilizosukwa na vigogo wawili wa chama hicho dhidi yake.“ Nimeshauriana na Makamu na tumeona kuna haja ya jamaa yako (Rashid) na genge lake kuitwa katika Kamati ya Nidhamu na Maadili kuhojiwa,” inasema sehemu ya waraka huo ambao aliusambaza kwa vyombo vya habari.



Waraka huo uliongeza, “ushahidi wa kutosha umekusanywa dhidi yake na wasaidizi wake wakuu na muono wetu ni kuwa tumfukuze uanachama.” Waraka huo ulisisitiza, “Wanachama walio wengi wanatudadisi kwa nini hatuchukui hatua, akishajulikana kuwa si mwanachama atakuwa hana mashiko muache aende CCM au Chadema.” Alipoulizwa Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili na Nidhamu wa CUF, Abdul Kambaya alisema taarifa za Rashid kukataa kuhojiwa na Kamati zitapelekwa katika Kamati ya Utendaji.



“ Ni kweli Hamad amegoma kuhojiwa kuhusu tuhuma zinazomkabili, lakini tunachofanya ni kupeleka taarifa kwa kamati ya Utendaji itakayofanya maamuzi,”alisema Kambaya na kubainisha kuwa kamati hiyo inaendelea kuwahoji wanachama wengine wanaotuhumiwa kuvunja katiba ya chama hicho.



Hivi karibuni Hamad Rashid alijikuta kwenye mgogoro na baadhi ya viongozi wa makao makuu ya chama hicho, baada ya kutangaza dhamira hiyo yake ya kugombea nafasi ya katiba mkuu mwaka 2014. Kuanzia hapo akajikuta ameingia kwenye mgogoro na chama hicho kiasi cha kunusurika kushambuliwa na watu wasiojulikana wakati akigawa misaada katika matawi ya chama hicho, kata ya Manzese. Mvutano huo ulisababisha vurugu katika tawi la Chechnya ambako wanachama wanaomuunga mkono walipambana na walinzi wa Blue Guard na kusababisha umwagaji damu.www.mwananchi.co.tz

Rais Dk. Shein ashiriki katika mazishi ya marehemu Kanali Nassor Waziri Mageta







Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk Ali Mohamed Shein,(wa tatu kulia) pamoja na Viongozi wengine wakiusalia mwili wa Marehemu Kanal Nassor Waziri Mageta,aliyekuwa Mkuu wa Kikosi cha Valantia,katika msikiti masjid Twariq Bububu nje wa mji wa Zanzibar, aliyefariki jana na kuzikwa Kijiji kwao Mkanyageni Wilaya ya Magharibi Unguja.

Wananchi wa Kijiji cha Mkanyageni Wilaya Magharibi Unguja wakilibeba jeneza la Marehemu Kanal Nassor Waziri Mageta,aliyekuwa Mkuu wa Kikosi cha Valantia,aliyefariki jana na kuzikwa Kijiji kwao Mkanyageni Wilaya ya Magharibi Unguja.

Askari wa Vikosi vya SMZ,wakilibeba Jeneza lenye mwili wa Marehemu Kanal Nassor Waziri Mageta,aliyekuwa Mkuu wa Kikosi cha Valantia,aliyezikwa jana katika kijiji cha mkanyageni Wilaya ya Magharibi mkoa wa mjini magharibi Unguja.

Askari wa Vikosi vya SMZ wakiondoa Nguo alizozitumia marehemu Kanali Nassor Waziri Mageta,aliyekuwa Mkuu wa Kikosi cha Valantia, aliyefariki jana na kuzikwa Kijiji kwao Mkanyageni Wilaya ya Magharibi Unguja.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk Ali Mohamed Shein,( katikati) pamoja na Viongozi wengine wakiwa katika maziko ya Marehemu Kanal Nassor Waziri Mageta,aliyekuwa Mkuu wa Kikosi cha Valantia, aliyefariki jana na kuzikwa Kijiji kwao Mkanyageni Wilaya ya Magharibi Unguja.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk Ali Mohamed Shein,akitia udongo katika kaburi la Marehemu Kanal Nassor Waziri Mageta,aliyekuwa Mkuu wa Kikosi cha Valantia,aliyefariki leo na kuzikwa Kijiji kwao Mkanyageni Wilaya ya Magharibi Unguja.

Askari wa Vikosi vya SMZ wakitoa salamu ya hesha katika kaburi la marehemu Kanali Nassor Waziri Mageta,aliyekuwa Mkuu wa Kikosi cha Valantia, aliyefariki jana na kuzikwa Kijiji kwao Mkanyageni Wilaya ya Magharibi Unguja. Picha na Ramadhan Othman IKULU

Tuesday, December 27, 2011

TIGO YAWAZAWADIA WASHINDI WA PROMOSHENI YA 'ZAMU YAKO KUSHINDA'

Ofisa Uhusiano wa Kampuni ya Mawasiloiano ya Tigo Bi. Alice Maro (kushoto) akimkabidhi mfano wa hund i ya shilingi milioni 4 mshindi wa shindano la 'Zamu yako Kushinda' Bi. Glory Remmy Makao makuu ya kampuni hiyo Dar es salaam leo katikati no Ofisa viwango wa Kampuni hiyo Bi. Pamela Shelukindo
Ofisa Uhusiano wa Kampuni ya Mawasiloiano ya Tigo Bi. Alice Maro (kushoto) akimkabidhi mfano wa hund i ya shilingi milioni 4 mshindi wa shindano la 'Zamu yako Kushinda' Bw. Waziri Rashidi Makao makuu ya kampuni hiyo Dar es salaam leo katikati no Ofisa viwango wa Kampuni hiyo Bi. Pamela Shelukindo
Ofisa Uhusiano wa Kampuni ya Mawasiloiano ya Tigo Bi. Alice Maro (kushoto) akimkabidhi mfano wa hund i ya shilingi milioni 4 mshindi wa shindano la 'Zamu yako Kushinda' Bi. Mariam Rashid Makao makuu ya kampuni hiyo Dar es salaam leo katikati no Ofisa viwango wa Kampuni hiyo Bi. Pamela Shelukindo

Monday, December 26, 2011

MANENO OSWARD VS RASHIDI MATUMLA AKUNA MBABE POINT 99 KWA 99 DROO


Bondia Rashidi Matumla (kushoto) akiwa chini baada ya kuteleza uku mpinzani wake Maneno Osward akimsubili kwa ajili ya kumpiga wakati wa mpambano wao uliofanyika Dar es salaam jana wakati wa sikukuu ya Xmasi mpaka mwisho wa pambano point ni 99 kwa 99 hivyo kuwa droo.(Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com)
Bondia Rashidi Matumla (kushoto) na Maneno Osward wakioneshana ufundi wa kutupa masumbwi wakati wa mpambano wao uliofanyika Dar es salaam jana wakati wa sikukuu ya Xmasi mpaka mwisho wa pambano point ni 99 kwa 99 hivyo kuwa droo.(Picha na http://www.superdboxingcoach.blogspot.com/
Bondia Rashidi Matumla (kushoto) na Maneno Osward wakioneshana ufundi wa kutupa masumbwi wakati wa mpambano wao uliofanyika Dar es salaam jana wakati wa sikukuu ya Xmasi mpaka mwisho wa pambano point ni 99 kwa 99 hivyo kuwa droo.(Picha na http://www.superdboxingcoach.blogspot.com/
Bondia Rashidi Matumla (kushoto) na Maneno Osward wakioneshana ufundi wa kutupa masumbwi wakati wa mpambano wao uliofanyika Dar es salaam jana wakati wa sikukuu ya Xmasi mpaka mwisho wa pambano point ni 99 kwa 99 hivyo kuwa droo.(Picha na http://www.superdboxingcoach.blogspot.com/
Bondia Maneno Osward (kushoto) akimuacha Rashidi Matumla chini baada ya kuanguka kwa kuteleza wakati wa mpambano wao uliofanyika Dar es salaam jana wakati wa sikukuu ya Xmasi mpaka mwisho wa pambano point ni 99 kwa 99 hivyo kuwa droo.(Picha na http://www.superdboxingcoach.blogspot.com/)

WAKAZI WA KARIAKOO ZILIZOKUA KOTA ZA BANDARI WAPINGA KUHAMISHWA WALA KUVUNJIWA NYUMBA ZAO




Na Mwandishi Wetu

WAKAZI wa Kariakoo Kota za Bandari kata ya Gerezani wameitaka serikali kutowahamisha wala kuwavunjia nyumba zao hadi hapo kesi yao iliyopo mahakama kuu kitengo cha Ardhi itakapo kamilika.
Hayo yalisemwa leo jijini Dar es Salaam na mwenyekiti wa mtaa huo alipokuwa akiongea na waandishi wa habari kuwa nyumba hizo walinunua kutoka serikali na kupewa mkataba.

Alisema eneo hilo linataka kuchukuliwa na serikali ili kujenga kituo cha mabasi yaendayo kasi bila ya kujali kuwa nyumba hizo waliuziwa ambapo serikali iliingia mkataba na mtu mmoja mmoja.

"Tumesikia fununu kuwa serikali inataka kuja kuvunja nyumba zetu kinguvu ikiwa kesi bado ipo mahakamani",alisema

Kwa upande wake katibu mwenezi wa siasa wa chama cha Mapinduzi Bw.Akida Hafidhi alisema serikali ilifanya makosa kuingia katika eneo hilo ikiwa inajua kabisa kuna mgogoro na kuongeza kuwa wanaomba haki iweze kutendeka kwa kuiachia mahakama kutoa maamuzi kama katiba inavyoelekeza.

Alisema serikali inatakiwa kutambua kuwa wakazi wa eneo hilo wanamiliki nyumba hizo kimkataba na hakuna mtu aliyevunja mkataba huo ambapo walinunua kutoka kwao.

Hata hivyo walisema watashangazwa endapo watasikia kuwa kuna mtu anaingilia uhuru wa mahakama ikiwa ibara ya 4(1) na 107(a) ya katiba ya Tanzania inaeleza wazi kuwa chombo cha mwisho chenye mamlaka ya kutekeleza utoaji haki ni mahakama ya Tanzania.

"Tumesema hivyo kwa sababu tulisikia baadhi ya watendaji serikalini walisema tulienda mahakamani kimakosa huku wakijua dhahili kuwa ni mahala ambapo haki inapatika",walisema

Walisema wanamuomba Rais Jakaya Kiwete asije akadanganywa kwa hilo kuwa kuna makubaliano yaliofanyika huku wakisisitiza kuwa kesi iliyopo ni kuvunjwa kwa mkataba na sio madai ya fidia kama ambavyo baadhi wa watendaji walivyopeleka taarifa serikalini.

WAKAZI WA KOTA ZA BANDARI WAKUTANA WAJADILIKESSY YAO


Baadhi ya wakazi wa zilizokua kota za bandari Gerezani wakimsikiliza mwanasheria wao

Mwanasheria wa wakazi wa zilizokua kota za bandari Gerezani , Dkt. Sengondo Mvungi (kushoto) akizungumza na wateja wake. Dar es salaam jana kuhusu maendeleo ya kesi yao iliyo mahakama kuu ya Tanzania
Mwanasheria wa wakazi wa zilizokua kota za bandari Gerezani , Dkt. Sengondo Mvungi (kushoto) akizungumza na wateja wake. Dar es salaam jana kuhusu maendeleo ya kesi yao iliyo mahakama kuu ya Tanzania
Mwanasheria wa wakazi wa zilizokua kota za bandari Gerezani , Dkt. Sengondo Mvungi (kushoto) akizungumza na wateja wake. Dar es salaam jana kuhusu maendeleo ya kesi yao iliyo mahakama kuu ya Tanzania

WAKAZI WA KARIAKOO ZILIZOKUA KOTA ZA BANDARI WAPINGA KUHAMISHWA WALA KUVUNJIWA NYUMBA ZAO



Na Mwandishi Wetu

WAKAZI wa Kariakoo Kota za Bandari kata ya Gerezani wameitaka serikali kutowahamisha wala kuwavunjia nyumba zao hadi hapo kesi yao iliyopo mahakama kuu kitengo cha Ardhi itakapo kamilika.
Hayo yalisemwa leo jijini Dar es Salaam na mwenyekiti wa mtaa huo alipokuwa akiongea na waandishi wa habari kuwa nyumba hizo walinunua kutoka serikali na kupewa mkataba.

Alisema eneo hilo linataka kuchukuliwa na serikali ili kujenga kituo cha mabasi yaendayo kasi bila ya kujali kuwa nyumba hizo waliuziwa ambapo serikali iliingia mkataba na mtu mmoja mmoja.

"Tumesikia fununu kuwa serikali inataka kuja kuvunja nyumba zetu kinguvu ikiwa kesi bado ipo mahakamani",alisema

Kwa upande wake katibu mwenezi wa siasa wa chama cha Mapinduzi Bw.Akida Hafidhi alisema serikali ilifanya makosa kuingia katika eneo hilo ikiwa inajua kabisa kuna mgogoro na kuongeza kuwa wanaomba haki iweze kutendeka kwa kuiachia mahakama kutoa maamuzi kama katiba inavyoelekeza.

Alisema serikali inatakiwa kutambua kuwa wakazi wa eneo hilo wanamiliki nyumba hizo kimkataba na hakuna mtu aliyevunja mkataba huo ambapo walinunua kutoka kwao.

Hata hivyo walisema watashangazwa endapo watasikia kuwa kuna mtu anaingilia uhuru wa mahakama ikiwa ibara ya 4(1) na 107(a) ya katiba ya Tanzania inaeleza wazi kuwa chombo cha mwisho chenye mamlaka ya kutekeleza utoaji haki ni mahakama ya Tanzania.

"Tumesema hivyo kwa sababu tulisikia baadhi ya watendaji serikalini walisema tulienda mahakamani kimakosa huku wakijua dhahili kuwa ni mahala ambapo haki inapatika",walisema

Walisema wanamuomba Rais Jakaya Kiwete asije akadanganywa kwa hilo kuwa kuna makubaliano yaliofanyika huku wakisisitiza kuwa kesi iliyopo ni kuvunjwa kwa mkataba na sio madai ya fidia kama ambavyo baadhi wa watendaji walivyopeleka taarifa serikalini.

WAKAZI WA KOTA ZA BANDARI WAJADILI KESSY YAO

Baadhi ya wakazi wa zilizokua kota za bandari Gerezani wakimsikiliza mwanasheria wao

Mwanasheria wa wakazi wa zilizokua kota za bandari Gerezani , Dkt. Sengondo Mvungi (kushoto) akizungumza na wateja wake. Dar es salaam jana kuhusu maendeleo ya kesi yao iliyo mahakama kuu ya Tanzania
Mwanasheria wa wakazi wa zilizokua kota za bandari Gerezani , Dkt. Sengondo Mvungi (kushoto) akizungumza na wateja wake. Dar es salaam jana kuhusu maendeleo ya kesi yao iliyo mahakama kuu ya Tanzania
Mwanasheria wa wakazi wa zilizokua kota za bandari Gerezani , Dkt. Sengondo Mvungi (kushoto) akizungumza na wateja wake. Dar es salaam jana kuhusu maendeleo ya kesi yao iliyo mahakama kuu ya Tanzania

JAHAZI MOLDEN TAARAB YATIMIZA MIAKA 5 NA KUZINDUA ALBAM YAKE YA MPENZI CHOCOLATE USIKU WA KUAMKIA LEO DIAMOND



Hassan Yahya Mwinyi Katibu Mkuu wa kundi la Taarab la Safari Malindi kulia akimpongeza Khamis Koha Mkurugenzi Msaidizi wa kundi la Muziki wa Taarab la Jahazi, baada ya kuzindua rasmi albam yao mpya ijulikanayo kama Mpenzi Chocolate na sherehe za miaka 5 ya kundi hilo zilizofanyika mkesha wa Krismasi usiku wa kuamkia leo, kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee ikishuhudiwa na mashabiki lukuki wa muziki wa Taarab huku mtandao wako wa FULLSHANGWE ukiwa ni mmoja wa mashuhuda. Uzinduzi huo ulioambatana na Jahazi Molden Taarab kutimiza miaka 5 ilidhaminiwa na kinywaji cha Serengeti Lager kinachozaliswa na kampuni ya bia ya Serengeti (SBL)

Mwanamuziki Mzee Yusuf ambaye pia ni kiongozi wa kundi hilo akiingia ukumbini kwa staili ya aina yake huku akilakiwa na mashabiki wa muziki wa Taarab.

Mmoja wa kundi hilo Aisha Mahamoud akipagawisha mashabiki mbvele ya Camera na mashabiki wake.

Keki Maalum ya miaka 5 ya Jahazi Molden Taarab ikisubiri kuliwa na wapenzi wa bendi hiyo.

Vinywaji vya kumwaga kutoka kampuni ya bia ya Erengeti vilikuwepo ukumbini kama unavyoona.

HADIJA KOPA AKONGA NYOYO ZA WATU HOLLAND




Mkesha wa Christmass ulikuwa wa aina yake kwa wakazi wa jiji la Den Haag nchini Holland.Malkia wa mipasho akiwapagawisha mashabiki wake.

kwa habari na mapicha zaidi http://magangaone.blogspot.com

MSONDO YAFUNIKA TCC CHANG'OMBE USIKU WA KUAMKIA LEO




Mwanamuziki chipukizi mtoto wa mwanamuziki wa zamani wa bendi ya Msondo TX Moshi William TX Moshi William Hassani Moshi, TX,Junior, akinyanyuliwa juu juu na mashabiki wa bendi hiyo wakati alipokuwa akiimba katika mpambano wa bendi za Msondo Band na DDC Mlimani Park Sikinde jana, kwenye viwanja vya TCC Sigara Chang'ombe jijini Dar es salaam.

Mpambano huo ulivuta mashabiki wengi katika viwanja vya TCC Sigara ambapo bendi ya Msondo, ilionekana kuwapiku wenzao wa Sikinde kutokana na Shamrashamra zilizokuwa zikitawala wakati Msondo wakiimba jukwaani, Onyesho hilo limefanyika usiku wa kuamkia leo ikiwa ni pamoja na kusherehekea sikukuu ya Krismas.

Wanamuziki Shaban Dede na Hassani MoshiTX ,Junior wa Msondo wakiimba jukwaani huku mashabiki wakiwashangilia kwelikweli wakati wa onyesho hilo lililofanyika TCC Chang'ombe usiku wa kuamkia leo.

Hassani Moshi TX Junior akiimba katikati ya mashabiki , huku mashabiiki hao wakimshangilia.

Kutoka kulia ni mwimbaji wa Bendi ya Sikinde Hassan Kunyata, Yusuph Bernald na Shaban Lendi wapiga Saxaphone wakifanya vitu vyao jukwaani.

Mwimbaji wa bendi ya Sikinde Othman Kambi akicheza sambamba na wanenguaji wa bendi hiyo wakati bendi hiyo ilipotupa karata yake ya mwisho usiku wa kuamkia leo.

Mashabiki wakipanga mstari huku wakiserebuka na Msondo.

Umati mkubwa wa mashabiki waliohudhuria katika onyesho hilo usiku wa kuamkia leo.

Wadau wakijimwaga na muziki wa Msondo hebu wacheki.

Mpiga gitaa la solo wa bendi ya Msondo Said Mabela wa pili kutoka kushoto akila pozi kwa picha na wadau usiku wa kuamkia leo.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...