Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Friday, March 30, 2012

KAMPUNI YA TIGO YAFUNGUA OFISI YA HUDUMA KWA WATEJA BAADA YA MATENGENEZO MAKUBWA MLIMANI CITY

Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt, Cyril Chami akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa kampuni ya tigo baada ya kuzindua ofisi ya huduma kwa wateja baada ya matengenezo makubwa mlimani city leo

Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt Cyril Chami akipatiwa maelezo ya moja ya bidhaa za simu zilizopo
simu humeiona muheshimiwaWaziri wa viwanda na biashara Dkt.Cyril Chami akikata utepe kuashiria uzinduzi huo leo kulia ni Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Tigo Bi.Hilda Damas
Msema Chochote Sauda Simba Kilumanga akionea

Baadhi ya Wafanyakazi wa Kampuni ya Tigo waliokuwepo katika ufunguzi huo wakiwa katika picha ya pamoja leo

Wednesday, March 28, 2012

SERIKALI YAIPIGIA DEBE TWIGA STARS



Na Mwandishi Wetu
SERIKALI imeipongeza Kampuni ya Heineken Afrika Mashariki kwa kuiteua Tanzania kuwa miongoni mwa nchi zinazotembelewa na Kombe la UEFA, huku ikiiomba kuwekeza kwenye sekta ya michezo hapa nchini hususan, timu ya taifa ya wanawake, Twiga Stars.
Pongezi na maombi hayo yalitolewa juzi usiku na Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara, katika hafla ya kulishuhudia kombe hilo iliyofanyika kwenye Hoteli ya Kilimanjaro Kempinski jijini Dar es Salaam.
Dk. Mukangara alisema wanatambua uwepo wa Heineken hapa nchini, kwani wanaziona bidhaa zao, hivyo kwa namna moja ama nyingine wanachangia uchumi wa nchi kupitia kodi.
Alisema kwa uamuzi huo wa kulileta kombe hilo maarufu duniani, wameongeza chachu na hamasa ya michezo hapa nchini, lakini litakuwa jambo bora kama watawekeza kwenye michezo hapa nchini na kuisaidia Twiga Stars, hasa ukizingatia inajituma na kuonyesha kiwango bora.
Katika hafla hiyo, ambayo waalikwa walipata nafasi ya kupiga picha na kombe hilo, ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali, akiwemo Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utawala Bora, Mathias Chikawe, Mbunge wa Bariadi Magharibi, John Cheyo, Mkurugenzi wa Michezo, Leonard Thadeo, Kaimu Katibu Mkuu wa TFF, Sunday Kayuni, Mwenyekiti wa Yanga, Lloyd Nchunga, Mwenyekiti wa Soka la Wanawake, Lina Madina Mhando na wengineo.

POLISI MJINI MOSHI AKUTWA DISKO NA MISOKOTO YA BANGI


Na Charles Ndagulla, Moshi
JESHI la Polisi mkoani Kilimanjaro, linamshikilia askari wake, namba G842 PC Deogratius, akituhumiwa kukutwa na misokoto minne ya dawa za kulevya aina ya bangi ndani ya ukumbi wa Pub Albeto mjini hapa.
Askari huyo wa kituo cha Polisi Majengo, alikamatwa Machi 25 mwaka huu, majira ya saa mbili usiku, baada ya kufanya fujo kwa kuwashambulia walinzi wa klabu hiyo, pamoja na mmiliki wake, Christopher Shayo maarufu kama Mzee Chris.
Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa jana na Kamanda wa Polisi mkoani Kilimanjaro, Absalom Mwakyoma, imesema kuwa, askari huyo aliingia ukumbini hapo kwa lengo la kunywa pombe na kujiburudisha na muziki.
Mwakyoma alisema, wakati muziki ukiendelea, mlinzi wa ukumbi huo, Rajabu Hamad alijulishwa na wateja wengine kuwa, kuna mtu anawafanyia fujo na baada ya kuingia ukumbini, mlinzi huyo alijikuta aking'atwa mkono na askari huyo.
Mbali na mlinzi huyo kung'atwa kwenye mkono wake wa kulia, pia askari huyo anadaiwa kumshambulia kwa kumpiga ngumi usoni mmiliki wa klabu hiyo na ndipo Polisi walipoitwa na kumtia mbaroni.
Kamanda Mwakyoma alisema kuwa, baada ya askari huyo kukamatwa na kupekuliwa, alikutwa na misokoto minne ya bangi mfukoni mwake na kwamba, kwa sasa yupo mahabusu wakati upelelezi ukiendendea na hatua nyingine za kinidhamu.

MAMBO YALIVYOKUWA KATIKA BONANZA LA WANA HABARI


Kocha wa Kimataifa wa Mchezo wa Masumbwi, Rajabu Mhamila Super D kushoto akimwelekeza jinsi ya kutupa masumbwi mwandishi wa Chanal Ten Meshaki Nzowa

Warembo warioshiriki katika michezo mbalimbali leo kutoka kushoto Mwali Ibrahimu, Ceciria Jeremia na Aneti Kagenda
Super D Boxing Coach akiwa katika Bonanza hilo leo

Super D boxing Coach akiselebuka na mwana dada Hadija Khalili





super D Boxing Coach

Tuesday, March 27, 2012

TOMASI MASHARI AJIFUA KUMKABILI SELEMANI GALILE APRIL 9

Kocha wa Mchezo wa Masumbwi kutoka Sweeden, Juma Ntuve kushoto akimwelekeza bondia Tomas Mashari wakati wa mazoezi ya kujiandaa kupambana na Bondia Selemani Galile April 9.(Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com)
Kocha wa Mchezo wa Masumbwi kutoka Sweeden, Juma Ntuve kulia akimwelekeza bondia Tomas Mashari wakati wa mazoezi ya kujiandaa kupambana na Bondia Selemani Galile April 9(Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com)
Bondia Tomasi Mashari akifanya Mazoezi leo kwa ajili ya mpambano wake wa ubingwa na Selemani Galile litakalofanyika April 9(Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com)
Kocha wa Mchezo wa Masumbwi kutoka Sweeden, Juma Ntuve kushoto akimwelekeza bondia Tomas Mashari wakati wa mazoezi ya kujiandaa kupambana na Bondia Selemani Galile April 9(Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com)

KAMBI YA KUCHUNGUZA AFYA ILIYODHAMINIWA NA TIGO BAGAMOYO YAPATA MAFANIKIO


Kambi ya kuchunguza afya bure Bagamoyo yapata mafanikio makubwa


23 Machi, 2012, Bagamoyo. Watu zaidi ya 700 wamepimwa bure katika kambi ya kuchunguza afya iliyofanyika eneo la Shule ya Msingi Kerege Matumbi wilaya ya Bagamoyo., tarehe 18, Machi 2012, kambi hiyo iliandaliwa na klabu ya rotary ya Oysterbay Dar es salaam, kwa kushirikiana na Hospital ya Hindu Mandal na Kidz Care Tanzania.

Vipimo vya malaria,virusi vya ukimwi,kisukari,masikio,pua,koromeo,macho na magonjwa mengine hatari vilifanywa na madaktari wapatao 40 pamoja na wasaidizi kutoka Chuo cha Aga Khan , Chama cha Kisukari Tanzania, Kituo cha afya cha Muhimbili ,Hospitali ya Shree Hindu Mandal na Chuo cha Afya cha Hurbert Kairuki.

Dawa za bure na miwani zilitolewa kwa watu waliopimwa na kutambulika kuwa na matatizo ya macho. Washiriki pia waliangaliwa afya zao kwa ujumla ili kuweza kutambua magonjwa ya kawaida na sababu hatarishi. Ushauri ulitolewa kuhusu lishe bora na umuhimu wa mazoezi.

Wagonjwa waliokuwa na matatizo ambayo hayakuweza kupatiwa ufumbuzi walipewa rufaa kwenda Hospitali ya Wilaya ya Bagamoyo kwa uchunguzi zaidi. Wagonjwa sita , pamoja na mtoto wa miezi sita ambao walikuwa wanaumwa nimonia, waliwahishwa Hospital ya Wilaya ya Bagamoyo kwa matibabu.

“Siwezi kuelezea jinsi kambi hii ilivyokuwa na manufaa kwa Wanachama wa Rotary na wote waliojitolea, alisema Bw. Maninder Lamba ambaye ni Rais wa Club ya Rotary ya Oysterbay Dar es Saalam. “ Huduma kwa wengine kwanza (‘Service Above Self) ni itikadi muhimu ya Rotary Club, tunajisikia kubarikiwa kwa kupata nafasi hii ya kuandaa tukio hili na kuweza kuwasaidia watu wengi wenye uhitaji”alisema.

Wakati watu wakisubiri kuonana na daktari waliburudishwa na kikundi cha maigizo kutoka Comunita Volontari per il Mondo (CVM) kilichobobea katika kutoa burudani inayogusa elimu ya afya pamoja na umuhimu na njia za kujikinga na mambukizi ya Virusi vya Ukimwi na Malaria. Vyandarua vya bure vilitolewa kwa kundi lililoko katika hatari ya maambukizi: watoto chini ya miaka mitano, wanawake wajawazito na watu wenye zaidi ya miaka 55.

“Kambi hii isingefanikiwa bila moyo wa kujitolea wa uliofanywa na madaktari pamoja na wasaidizi wao zaidi ya 60, alisema bwana Thomas Scherer, ambaye ni Mkurugenzi wa Miradi ya klabu ya Rotary Oysterbay Dar es salaam. “Hii ni mara yetu ya pili kuendesha kambi kama hii, na katika kuila kambi tunajifunza na kupata uzoefu zaidi wa namna ya kuendesha kambi kwa ufanisi zaidi na kupata matokeo mazuri zaidi. Tunatazamia kuendesha kambi katika maeneo yenye uhitaji zaidi na upatikanaji wa huduma bora za kiafya ni mdogo.


Gharama ya hii kambi imegharamiwa na shughuli mbalimbali za kuchangisha fedha zinazofanywa na klabu ya Rotary ya Oysterbay, pamoja na udhamini kutoka Tigo, D B Shaparyia Ltd na CMC Automobile.

“Tunashukuru ukarimu wa wadhamini wetu, tumeweza kutoa vipimo vyote, ushauri na dawa bure” alisema Bw. Lamba.

“Afya bora ni moja ya vitu muhimu kwetu” alisema bwana Diego Gutierrez ambaye ni Meneja Msaidizi wa Tigo. “Kwa kujikita katika kutoa taarifa na msaada wa kitabibu kwa wale waliokosa fursa ya kupata matibabu, tumechukua jukumu la kuleta mabadiliko katika maisha yao” alisema.

Kuhusu Rotary

Rotary international ni klabu ya kwanza duniani,yenye zaidi ya wanachama milioni moja nukta mbili kwenye klabu zake33,000 zilizopo duniani. Klabu za rotary ni viongozi wa biashara ambao wanafanya kazi, kitaifa,kimkoa na kimataifa kupambana na njaa,kuboresha afya na huduma ya vyoo,kutoa elimu, na kuondoa ugonjwa wa polio. Na kauli mbiu yetu ni “service Above Self” –huduma kwa wengine kwanza.


Klabu ya Rotary ya Oysterbay jijini Dar es salam inakaribisha wanachama wapya. Kufahamu zaidi juu ya klabu hii,wanachama wake shughuli zake za kujitolea nchini Tanzania, tembelea www.rotarydar.com.

Kuhusu Tigo:

Tigo ni mtandao wa simu za mkononi ya kwanza Tanzania, ilianza biashara mwaka 1994 na ni mtandao wa simu Tanzania wenye ubunifu wa hali ya juu na bei nafuu kupita zote nchini. Tigo ni sehemu ya MillicomInternational Cellular S.A (MIC) na hutoa huduma za simu za mkononi kwa gharama nafuu na inayopatikana maeneo mengi kiurahisi kwa wateja zaidi ya milioni 30 katika masoko 13 yanaoibuka Afrika na Amerika ya Kusini.

Msingi wa mafanikio ya Tigo ni uzingatiaji wa mikakati mitatu ambao,ni Gharama nafuu, Uwepo na Upatikanaji .Tunajenga dunia ambapo huduma za simu ni za bei nafuu, zipo na zinapatikana kila mahali na kwa wote. Hii inahakikisha kwamba wateja wetu wanapata huduma bora zaidi kwa bei nafuu kuliko zote katika mikoa yetu 26, Tanzania Bara na Zanzibar.

Kwa taarifa zaidi tembelea: www.tigo.co.tz

Monday, March 26, 2012

Katibu Mpya wa Baraza la Wawakilishi aapishwa


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk.Ali Mohamed Shein,akimuapisha Yahya Khamis Hamad,kuwa Katibu wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar,leo baada ya kumteuwa kushika nafasi hiyo,hafla ya kiapo ilifanyika Ikulu Mjini Zanzibar.{Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.}
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk.Ali Mohamed Shein,akimuapisha Luteni Kanali Mohamed Mwinjuma Kombo,kuwa Mkuu wa Kikosi cha Valantia Zanzibar,leo baada ya kumteuwa kushika nafasi hiyo,hafla ya kiapo ilifanyika Ikulu Mjini Zanzibar.{Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.}

RAIS KIKWETE AONGOZA MAZISHI YA ALIYEKUWA MKUU WA WILAYA YA LIWALE HAYATI VICTOR PAUL CHIWILE LEO KIBAHA


Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akitoa heshima zake za Mwisho kwa aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Liwale Marehemu Victor Paul Chiwile
wakati wa mazishi Kibaha Picha ya Ndege mkoa wa Pwani leo Machi 26, 2012
(PICHA NA IKULU)
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Makamu wa Rais Dkt Mohamed Gharib Bilal, Waziri Mkuu Mh Mizengo Pinda, Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mh Mwantumu Mahiza na Mkuu wa Mkoa wa Lindi wakiwa mazikoni
Rais Jakaya Kikwete akiweka shada la maua kwenye kaburi la aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Liwale Marehemu Victor Paul Chiwile
wakati wa mazishi Kibaha Picha ya Ndege mkoa wa Pwani leo Machi 26, 2012

TBL YAWAZAWADIA MAWAKALA WAO WAKE


Meneja Usimamizi wa Kitengo cha Fedha wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Aloyce Qande (kushoto), akimkabidhi tuzo mshindi wa tatu wa uuzaji bora wa vinywaji vya kampuni hiyo Kanda ya Kusini,Robinson Matemba wa Turiani. Morogoro.katika hafla ya kuwazawadia mawakala bora iliyofanyika mwishoni mwa wiki katika Hoteli ya Serena, Dar es Salaam.Wa pili kushoto ni Meneja Mauzo na Usambazaji wa TBL Kanda ya Kusini, James Bokela na Reginald Mosha ambaye ni Meneja Huduma za Biashara wa TBL.
Meneja Usimamizi wa Kitengo cha Fedha wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Aloyce Qande (kushoto), akimkabidhi tuzo mshindi wa kwanza wa uuzaji bora wa vinywaji vya kampuni hiyo Kanda ya Kusini, Mkurugenzi wa Massawe Grocery ya Kibaha, Jacob Massawe, katika hafla ya kuwazawadia mawakala bora iliyofanyika mwishoni mwa wiki katika Hoteli ya Serena, Dar es Salaam.
Meneja Usimamizi wa Kitengo cha Fedha wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Aloyce Qande (kushoto), akimkabidhi tuzo mshindi wa kwanza wa uuzaji bora wa vinywaji vya kampuni hiyo Kanda ya Kusini, Mkurugenzi wa Massawe Grocery ya Kibaha, Jacob Massawe, katika hafla ya kuwazawadia mawakala bora iliyofanyika mwishoni mwa wiki katika Hoteli ya Serena, Dar es Salaam.
Mawakala wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), walioshinda kwa kuwa wauzaji bora wa vinywaji vya kampuni hiyo kwa Kanda ya Kusini, wakinyanyua juu tuzo walizozawadiwa katika hafla iliyofanyika mwishoni mwa wiki katika Hoteli ya Serena, Dar es Salaam. Kutoka kulia ni mshindi wa kwanza,Mkurugenzi wa Massawe Grocery ya Kibaha, Jacob Massawe, Mshindi wa pili, Mkurugenzi wa Wazo Road Haulege ya Tegeta, Valency Msacky na Robinson Matemba wa Turiani. Morogoro.

CHAMA KIPYA CHA ADC CHAPEWA USAJILI WA MUDA


msajili wa vyama vya siasa John Tendwa akiongea na waandishi wa habari leo ofisini kwake jijini Dar es salaam kabla ya kukikabidhi cheti chama kipya cha siasa hapa nchini kinachujulikana kama (ALLANCE FOR DEMOCRATIC CHANGE ADC) (PICHA ZOTE NA PHILEMON SOLOMON WA FULLSHANGWE)
John Tendwa kushoto akimkabidhi cheti cha usajili wa muda mwenyekiti wa chama cha ALLANCE FOR DEMOCRATIC CHANGE ADC Bw. Said Miraji kulia ni kaimu katibu mkuu wa chama (ADC)Bw. Lucas Limbu.
)Mwenyekiti wa chama chan ADC akiongea na wa waandishi wa habari mara baada ya kukabidhiwa cheti cha usajili wa muda leo.
Baadhi ya wakereketwa wa chama cha ADC wakishangilia.
Mwenyekiti wa ADC kulia Bw; Said Miraji akizindua tawi jipya
Mwenyekiti wa ADC kushoto Bw. Said Miraji akipandisha bendera ya chama hicho makao makuu yilioko buguruni jijini Dar es salaam kulia kaimu katibu mkuu Bw. Lucas Limbu wa chama hicho.

WATATU WAPATIKANA KUSHIRIKI MAONYESHO YA WIKI YA MKITINDO YA AFRIKA YA KUSINI


Mwanamitindo wa kimataifa wa Tanzania, Millen happiness Magese (katikati) akipiga picha ya pamoja na washindi watatu waliopata tiketi ya kuonyesha mavazi katika wiki ya mitindo ya Afrika Kusini, Victor Casmir, Victoria Casmir na Anastazia Gura. Wengine katika picha ni Aminat Ayinde kutoka kampuni ya America Next top model cycle 12 (wa kwanza kushoto), Ritha Poulsen (wa kwanza kulia) na Mustapha Hassanali aliyesimama nyuma. Picha kwa hisani ya Millen Magese group of company
**************************************
Na Mwandishi Wetu, Jijini
Wanamitindo watatu, Anastazia Gura (21) na mapacha, Victoria Casmir (20) na Victor Casmir wameshinda usaili uliondeshwa na kampuni ya Millen Magese Group Company Limited chini ya mpango wake wa kuitangaza Tanzania kupitia fani ya mitindo ujulikanao kwa jina la Tanzania International Fashion Exposé (TIFEX).

Wanamitindo hao wamefanikiwa kupita katika usaili huo ambao uliwajumuisha wanamitindo 350 kutoka katika maeneo mbali mbali ya jiji la Dar es Salaam na mikoa ya jirani.

Kutokana na ushindi huo, wanamitindo hao wanatarajia kuondoka mwishoni mwa mwezi huu kuelekea nchini Afrika Kusini kushiriki kwa mara ya kwanza katika historia katika fani ya mitindo ya wiki ya mitindo ya Afrika Kusini maarufu kwa jina la South Africa Fashion Week.

Akizungumza baada ya usaili huo, Millen alisema kuwa amestushwa sana na ujio wa wanamitindo mbali mbali mbali waliofika katika usaili huo japo alitangaza kwa muda mfupi.

Millen alisema kuwa awali alipanga kuchukua wanamitindo wawili, lakini kutokana na idadi kubwa iliyojitokeza, ameongeza nafasi moja kama shukrani yake ya witikio huo mkubwa.

Alisema kuwa walipata kazi kubwa sana kuchagua wanamitindo hao watatu, lakini kwa kushirikiana na wanamitindo maarufu Aminat Ayinde kutoka kampuni ya America Next top model cycle 12 na Ritha Poulsen, waliweza kufanikisha zoezi hilo mapema zaidi.

Millen alisema kuwa washindi hao wamepata fursa pekee ya kujitangaza wenyewe kimataifa na kufuata nyayo zake.

Alisema kuwa lengo kubwa la kampuni yake ni kuendeleza fani ya uanamitindo na vile vile kuitangaza Tanzania nje ya mipaka yake kwa kupitia fani ya mitindo na hata kwa njia ya utalii.

Aliongeza kuwa japo Tanzania ina wanamitindo wengi na wabunifu, bado kuna pengo kubwa ukilinganisha na maendeleo ya fani hiyo katika nchi ya Afrika Kusini na Nigeria.

Alisema kuwa nchi hizo zimepiga hatua kubwa sana na yeye kuhamasika kuanzisha kampuni yake iliyozinduliwa mwezi Machi mwaka jana kwa lengo la kuziba pengo hilo na kuleta maendeleo ili wahusika wafaidike na matunda ya fani yao.

UZINDUZI WA MUONEKANO MPYA WA BIA YA BILIMA EXTRA LAGER


Meza Kuu wakigonganisha chupa kuashilia uzinduzi wa muonekano mpya wa Bia ya Balimi Extra Lager Mkoani Shinyanga jana.Kutoka kulia ni Meneja Masoko wa TBL, Fimbo Butallah,Meneja mauzo wa Kanda, Malaki Sitaki, Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga,Amina Masenza, Meneja mauzo wa Mkoa wa Shinyanga, Robert Michael na Meneja wa Bia ya Balimi Extra Lager, Edith Bebwa
Meneja wa Bia ya Balimi Extra Lager, Edith Bebwa akizungumza na wageni waalikwa wakati wa uzinduzi wa muonekano mpya wa Bia ya Balimi Extra Lager Mkoani Shinyanga jana.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Amina Masenza(kulia) akizungumza na wageni waalikwa wakati wa uzinduzi wa muonekano mpya wa Bia ya Balimi Extra Lager Mkoani Shinyanga jana.Kushoto ni Meneja wa Bia ya Balimi Extra Lager, Edith Bebwa na Meneja mauzo wa Mkoa wa Shinyanga, Robert Michael.
Meneja wa Bia ya Balimi Extra Lager, Edith Bebwa (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na wakina Dada walioshona sare za Balimi Extra Lager wakati wa uzinduzi wa muonekano mpya wa Bia ya Balimi Extra Lager Mkoani Shinyanga jana.

KOMBE LA UEFA NA UNHCR


Waziri Mkuu,Mizengo Pinda akiwapungua watu waliofika kwenye ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu kushuhudia wakati alipokabidhiwa kombe la UEFA jijini Dar es salaam Machi 26, 2012.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akimkabidhi zawadi ya kinyago Mwakilishi mkazi wa shirika la Unoja wa mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), BW Oluseyi Bajulaye ambaye alikwenda ofisini kwa Wziri mkuu kuaga
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...