Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Tuesday, March 27, 2012

KAMBI YA KUCHUNGUZA AFYA ILIYODHAMINIWA NA TIGO BAGAMOYO YAPATA MAFANIKIO


Kambi ya kuchunguza afya bure Bagamoyo yapata mafanikio makubwa


23 Machi, 2012, Bagamoyo. Watu zaidi ya 700 wamepimwa bure katika kambi ya kuchunguza afya iliyofanyika eneo la Shule ya Msingi Kerege Matumbi wilaya ya Bagamoyo., tarehe 18, Machi 2012, kambi hiyo iliandaliwa na klabu ya rotary ya Oysterbay Dar es salaam, kwa kushirikiana na Hospital ya Hindu Mandal na Kidz Care Tanzania.

Vipimo vya malaria,virusi vya ukimwi,kisukari,masikio,pua,koromeo,macho na magonjwa mengine hatari vilifanywa na madaktari wapatao 40 pamoja na wasaidizi kutoka Chuo cha Aga Khan , Chama cha Kisukari Tanzania, Kituo cha afya cha Muhimbili ,Hospitali ya Shree Hindu Mandal na Chuo cha Afya cha Hurbert Kairuki.

Dawa za bure na miwani zilitolewa kwa watu waliopimwa na kutambulika kuwa na matatizo ya macho. Washiriki pia waliangaliwa afya zao kwa ujumla ili kuweza kutambua magonjwa ya kawaida na sababu hatarishi. Ushauri ulitolewa kuhusu lishe bora na umuhimu wa mazoezi.

Wagonjwa waliokuwa na matatizo ambayo hayakuweza kupatiwa ufumbuzi walipewa rufaa kwenda Hospitali ya Wilaya ya Bagamoyo kwa uchunguzi zaidi. Wagonjwa sita , pamoja na mtoto wa miezi sita ambao walikuwa wanaumwa nimonia, waliwahishwa Hospital ya Wilaya ya Bagamoyo kwa matibabu.

“Siwezi kuelezea jinsi kambi hii ilivyokuwa na manufaa kwa Wanachama wa Rotary na wote waliojitolea, alisema Bw. Maninder Lamba ambaye ni Rais wa Club ya Rotary ya Oysterbay Dar es Saalam. “ Huduma kwa wengine kwanza (‘Service Above Self) ni itikadi muhimu ya Rotary Club, tunajisikia kubarikiwa kwa kupata nafasi hii ya kuandaa tukio hili na kuweza kuwasaidia watu wengi wenye uhitaji”alisema.

Wakati watu wakisubiri kuonana na daktari waliburudishwa na kikundi cha maigizo kutoka Comunita Volontari per il Mondo (CVM) kilichobobea katika kutoa burudani inayogusa elimu ya afya pamoja na umuhimu na njia za kujikinga na mambukizi ya Virusi vya Ukimwi na Malaria. Vyandarua vya bure vilitolewa kwa kundi lililoko katika hatari ya maambukizi: watoto chini ya miaka mitano, wanawake wajawazito na watu wenye zaidi ya miaka 55.

“Kambi hii isingefanikiwa bila moyo wa kujitolea wa uliofanywa na madaktari pamoja na wasaidizi wao zaidi ya 60, alisema bwana Thomas Scherer, ambaye ni Mkurugenzi wa Miradi ya klabu ya Rotary Oysterbay Dar es salaam. “Hii ni mara yetu ya pili kuendesha kambi kama hii, na katika kuila kambi tunajifunza na kupata uzoefu zaidi wa namna ya kuendesha kambi kwa ufanisi zaidi na kupata matokeo mazuri zaidi. Tunatazamia kuendesha kambi katika maeneo yenye uhitaji zaidi na upatikanaji wa huduma bora za kiafya ni mdogo.


Gharama ya hii kambi imegharamiwa na shughuli mbalimbali za kuchangisha fedha zinazofanywa na klabu ya Rotary ya Oysterbay, pamoja na udhamini kutoka Tigo, D B Shaparyia Ltd na CMC Automobile.

“Tunashukuru ukarimu wa wadhamini wetu, tumeweza kutoa vipimo vyote, ushauri na dawa bure” alisema Bw. Lamba.

“Afya bora ni moja ya vitu muhimu kwetu” alisema bwana Diego Gutierrez ambaye ni Meneja Msaidizi wa Tigo. “Kwa kujikita katika kutoa taarifa na msaada wa kitabibu kwa wale waliokosa fursa ya kupata matibabu, tumechukua jukumu la kuleta mabadiliko katika maisha yao” alisema.

Kuhusu Rotary

Rotary international ni klabu ya kwanza duniani,yenye zaidi ya wanachama milioni moja nukta mbili kwenye klabu zake33,000 zilizopo duniani. Klabu za rotary ni viongozi wa biashara ambao wanafanya kazi, kitaifa,kimkoa na kimataifa kupambana na njaa,kuboresha afya na huduma ya vyoo,kutoa elimu, na kuondoa ugonjwa wa polio. Na kauli mbiu yetu ni “service Above Self” –huduma kwa wengine kwanza.


Klabu ya Rotary ya Oysterbay jijini Dar es salam inakaribisha wanachama wapya. Kufahamu zaidi juu ya klabu hii,wanachama wake shughuli zake za kujitolea nchini Tanzania, tembelea www.rotarydar.com.

Kuhusu Tigo:

Tigo ni mtandao wa simu za mkononi ya kwanza Tanzania, ilianza biashara mwaka 1994 na ni mtandao wa simu Tanzania wenye ubunifu wa hali ya juu na bei nafuu kupita zote nchini. Tigo ni sehemu ya MillicomInternational Cellular S.A (MIC) na hutoa huduma za simu za mkononi kwa gharama nafuu na inayopatikana maeneo mengi kiurahisi kwa wateja zaidi ya milioni 30 katika masoko 13 yanaoibuka Afrika na Amerika ya Kusini.

Msingi wa mafanikio ya Tigo ni uzingatiaji wa mikakati mitatu ambao,ni Gharama nafuu, Uwepo na Upatikanaji .Tunajenga dunia ambapo huduma za simu ni za bei nafuu, zipo na zinapatikana kila mahali na kwa wote. Hii inahakikisha kwamba wateja wetu wanapata huduma bora zaidi kwa bei nafuu kuliko zote katika mikoa yetu 26, Tanzania Bara na Zanzibar.

Kwa taarifa zaidi tembelea: www.tigo.co.tz

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...