Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Tuesday, March 20, 2012

WABONGO WACHANGAMKIA FOMU MISS WORLD 2012

WABONGO WACHANGAMKIA FOMU MISS WORLD 2012


SIKU chache baada ya kutangazwa kwa zoezi la kusaka mwakilishi wa Tanzania kwenye mashindano ya urembo ya dunia ‘Miss World 2012’, warembo 11 wamejitokeza mpaka sasa kuchukua fomu za kuwania nafasi hiyo.
Mwaka huu Tanzania itatuma mwakilishi tu na si Miss Tanzania, hiyo nimetokana na mabadiliko ya kalenda yaliyofanywa na waandaaji wa shindano la Miss World ambapo mwaka huu fainali zake zimepangwa kufanyika mwezi Agosti 2012 nchini China.
Mkurugenzi wa Lino International Agency inayoratibu shindano la Miss Tanzania, alisema kwamba zoezi hilo linaloonekana kuvutia wengi linakwenda vema na hiyo inatokana na kasi ya warembo kuwa juu.
Alisema zoezi hilo litaendelea kwa wiki kadhaa ambapo majina ya washindani hayatawekwa hadharani kabla ya kamati kuchuja warembo wenye sifa na kubakiza kumi ambao watapanda jukwaani katika ‘Min Miss Tanzania’ ili kumpata mwakilishi huyo.
Aidha, Lundenga aliongeza kuwa kati ya wasichana hao hakuna hata mmoja aliyewahi kushiriki shindano lolote la urembo licha ya warembo waliopata kushiriki Miss Tanzania hadi hatua ya fainali (isipokuwa aliyetwaa taji) kuwa na nafasi ya kushiriki tena ilimradi akidhi vigezo vinavyohitajika.
Wiki iliyopita kamati hiyo ilitangaza mchakato mpya wa kumpata mwakilishi huyo ili kuendana na kalenda ya Miss World huku mchakato wa mashindano ya Redd’s Miss Tanzania 2012 katika ngazi zote utaendelea kama kawaida na mshindi wa Redd’s Miss Tanzania 2012 atawakilisha nchi kwenye fainali za mashindano ya urembo ya dunia mwaka 2013.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...