Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, March 28, 2012

POLISI MJINI MOSHI AKUTWA DISKO NA MISOKOTO YA BANGI


Na Charles Ndagulla, Moshi
JESHI la Polisi mkoani Kilimanjaro, linamshikilia askari wake, namba G842 PC Deogratius, akituhumiwa kukutwa na misokoto minne ya dawa za kulevya aina ya bangi ndani ya ukumbi wa Pub Albeto mjini hapa.
Askari huyo wa kituo cha Polisi Majengo, alikamatwa Machi 25 mwaka huu, majira ya saa mbili usiku, baada ya kufanya fujo kwa kuwashambulia walinzi wa klabu hiyo, pamoja na mmiliki wake, Christopher Shayo maarufu kama Mzee Chris.
Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa jana na Kamanda wa Polisi mkoani Kilimanjaro, Absalom Mwakyoma, imesema kuwa, askari huyo aliingia ukumbini hapo kwa lengo la kunywa pombe na kujiburudisha na muziki.
Mwakyoma alisema, wakati muziki ukiendelea, mlinzi wa ukumbi huo, Rajabu Hamad alijulishwa na wateja wengine kuwa, kuna mtu anawafanyia fujo na baada ya kuingia ukumbini, mlinzi huyo alijikuta aking'atwa mkono na askari huyo.
Mbali na mlinzi huyo kung'atwa kwenye mkono wake wa kulia, pia askari huyo anadaiwa kumshambulia kwa kumpiga ngumi usoni mmiliki wa klabu hiyo na ndipo Polisi walipoitwa na kumtia mbaroni.
Kamanda Mwakyoma alisema kuwa, baada ya askari huyo kukamatwa na kupekuliwa, alikutwa na misokoto minne ya bangi mfukoni mwake na kwamba, kwa sasa yupo mahabusu wakati upelelezi ukiendendea na hatua nyingine za kinidhamu.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...