Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Tuesday, March 20, 2012

WAZIRI MSTAAFU EDWARD LOWASSA ATEMBELEA SHULE YA MTAKATIFU ANN’S MJINI MOROGORO


Waziri Mkuu Mstaafu,Mh. Edward Lowassa akiongozana na Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Mtakatifu Ann's ya Mkoani Morogoro,Sista Dennis wakati alipofika shuleni hapo na kuzungumza na wanafunzi wa shule hiyo,ambapo aliwataka wanafunzi hao kusoma kwa bidi ili waweze kuwa viongozi wa baadaye.
*******************************
Na mwandishi Wetu, Morogoro
Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa, amewataka wanafunzi wa kike kusoma kwa bidi ili waweze kuwa viongozi wazuri na tegemezi wa baadaye.
Lowassa, ametoa kauli hiyo wakati alipokuwa akizungumza na wanafunzi na viongozi wa Shule ya Sekondari ya wasichana ya mtakatifu Anns iliyopo mjini Morogoro leo.
Baada ya kutembelea na kujionea mazingira halisi ya shule hiyo, Lowassa alitoa zawadi ya mipira kwa kila darasa katika shule hiyo, ikiwa ni moja ya njia ya kuhamasisha michezo mashuleni.
Naye Mkuu wa shule hiyo, Sister Dennis, pamoja na wanafunzi na watawa wengine wa shuleni hiyo walimshukuru Lowassa kwa kufanya ziara hiyo shuleni hapo na kushukuru kwa kuwapatia zawadi ya mipira na kumtakia afya njema ili aweze kuendelea kuwatumikia watanzania.
Waziri Mkuu Mstaafu,Mh. Edward Lowassa akisalimiana na Mmoja wa Walimu wa Shule ya Mtakatifu Ann's iliopo Mkoani Morogoro,Sista Martha wakati akiwasili shuleni hapo.Kulia ni Mke wa, Lowassa,Mama Regina Lowassa na wa pili (kushoto) ni Mkuu wa Shule hiyo, Sista Dennis
Wanafunzi wa Shule ya Sekindari ya Wasichana ya Mtakatifu Ann's ya Mkoani Morogoro wakiimba wimbo maalum wa kumkaribisha,Waziri Mkuu Mstaafu.
Waziri Mkuu mstaafu,Mh. Edward Lowassa pamoja na Mkewe Mama Regina Lowassa wakiwa katika picha ya pamoja na Walimu wa Shule ya Mtakatifu Ann's ya Mkoani Morogoro.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...