Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, March 14, 2012

MALI ALIZOIBIWA WAZIRI MALIMA ZAKUTWA KWA 'MA-MDOGO'

�div>KAMANDA wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Adolphina Chialo amesema kuwa aliyemwibia Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Adam Malima vitu mbalimbali vyenye thamani ya zaidi ya Sh23.25 milioni katika hoteli ya Nashera mkoani Morogoro sio mwanamke.

Kamanda huyo alisema mtuhumiwa aliyekamatwa na polisi alipohojiwa alieleza kuwa vitu alivyoiba alivihifadhi nyumbani kwa mama yake mdogo na kwamba waziri Malima hakuwa na bunduki aina ya SMG, kama inavyodaiwa na baadhi ya watu.

Naibu Waziri Malima alikumbwa na mkasa huo uliozua maswali mengi saa 10 alfajiri ya kuamkia Machi 9, mwaka huu baada ya watu kueleza sababu tofauti za wizi huo.Baadhi ya watu walidai kuwa Waziri huyo alikuwa na mtu chumbani anayesaidikiwa alitoroka na vitu hivyo na wengine walidai kuwa aliibiwa na mtu aliyepitia dirishani baada ya kufungua dirisha.

Chialo aliliambia Mwananchi jana kuwa mmoja wa watuhuniwa wa tukio hilo alipobanwa alieleza wazi kuwa vitu alivyoiba alivihifadhi kwa mama yake mdogo.“Unajua haya mambo yanakuzwa lakini hayana ukweli wowote, yupo mtu mmoja ambaye baada ya kumbana alieleza kuwa vitu alivyoiba alivihifadhi kwa mama yake mdogo,” alisema Chialo.

Akizungumzia taarifa kuwa Waziri Malima alikuwa na SMG katika chumba chake alisema “Hakuwa na SMG alikuwa na bastola, SMG ni silaha ambayo hata mimi Kamanda wa polisi siwezi kutembea nayo”Alifafanua kuwa silaha hiyo ya kivita humilikiwa kwa kibali maalumu na kwamba si rahisi kwa mtu kuwa nayo kienyeji.

“Hata silaha ambazo alikuwa nazo Waziri Malima ni za kawaida na anazimiliki kihalali” alisema Chialo.

Akitoa ufafanuzi wa tukio hilo, Machi 9 mwaka huu Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani humo, Hamisi Seleman alisema ingawa uchunguzi unaendelea kufanyika, taarifa za awali zilieleza kuwa mtu asiyejulikana alivunja dirisha la chumba namba 125 alichopanga Naibu Waziri huyo kisha kuingia ndani na kuiba vitu hivyo vyenye thamani ya zaidi ya Sh23.25 milioni.

"Vitu alivyoibiwa ni pamoja na laptop tatu, aina ya Dell zenye thamani ya Sh5.6 milioni.

Vinasa sauti viwili vya digitali na headphone zake zote ambavyo thamani yake ni Sh 1 milioni na simu tatu aina ya Nokia C6 ya Sh500,000, Nokia E200 ya Sh250,000 na Blackberry zenye thamani ya Sh5.5 milioni," alisema kamanda huyo na kuongeza:

"Vitu vingine ni pete mbili za almasi zenye thamani ya Sh2.5 milioni, Dola 4,000 za Marekani ambazo ni sawa na Sh6.5milioni, Sh1.5 milioni, kadi mbili za benki, mabegi matatu ya nguo, baraghashia mbili zenye thamani ya Sh50,000 na nyaraka mbalimbali za Serikali.

"Kaimu kamanda huyo alisema kuwa polisi waliokwenda kufanya uchunguzi wa awali walibaini kuwa mtu aliyeiba vitu hivyo hakuwa amevaa viatu kutokana na nyayo za miguu yake zilizoonekana nje ya chumba alichokuwa naibu waziri huyo.Kaimu kamanda huyo ambaye pia ni Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa wa Morogoro, alisema kuwa hata hivyo, mwizi aliyeiba vitu hivyo hakuiba bastola na bunduki aina ya SMG alizokuwa nazo Naibu Waziri huyo ambazo zilikuwa sehemu iliyowazi.

Katika hatua nyingine, polisi mkoani Morogoro, wanawashikilia watu watano wanaotuhumiwa kumwibia Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Malima katika Hoteli ya Nashera wiki iliyopita huku asilimia 90 ya vitu vilivyoibiwa vikipatikana kutoka kwa watuhumiwa hao.

Kamanda Chialo alisema waliokamatwa kuwa mmoja ni mkazi wa Chamwino kwa Mgulasi na wengine ni wakazi wa Mafiga Manispaa ya Morogoro ambao kwa pamoja wanadaiwa kushiriki katika tukio hilo la wizi.


No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...