Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Saturday, March 17, 2012

MAZISHI YA MWAKILISHI WA JIMBO LA BUBUBU ZANZIBAR JANA

Wananchi mbalimbali wakiwa wamebeba Jeneza la aliyekuwa Mwakilishi wa Jimbo la Bububu Marehemu Salum Amour Mtondoo, wakati wakielekea Msikitini kwa ajili ya Kumsalia.Marehemu alifariki juzi katika Hospitali ya Mnazi Mmoja Mjini Zanzibar.
Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ali Hassan Mwinyi akiweka udongo katika kaburi la aliyekua Mwakilishi wa Jimbo la Bububualiekuwa Muakilishi wa Jimbo la Bububu Marehemu Salum Amour Mtondoo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohd Shein akiongoza wanananchi mbalimbali katika mazishi ya aliekuwa Mwakilishi wa Jimbo la Bububu Zanzibar.Mazishi hayo yaliofanyika huko kijijini kwao Bumbwini Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Seif Sharif Hamadi akimimina Udongo katika Kaburi la aliekuwa Mwakilishi wa Jimbo la Bububu Marehemu Salum Amour Mtondoo aliezikwa huko kijijini kwao Bumbwini Mkoa wa Kaskazini Unguja.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...