Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, March 14, 2012

Solomon Mukubwa kulitikisa Pasaka uwanja wa Taifa

Na Mwandishi WetuMWIMBAJI nguli kutoka Kenya, Solomon Mukubwa, anatarajia kutumbuiza katika tamasha la muziki wa Injili la Pasaka litakalofanyika Sikukuu ya Pasaka Aprili 8 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama ambaye ni Mkurugenzi wa Msama Promotions, alisema Dar es Salaam jana kuwa Mukubwa ameahidi kufanya mambo makubwa.Msama alisema mwimbaji huyo wa nyimbo za kumsifu Mungu mwenye ulemavu wa mkono mmoja, hivi sasa anatamba na albamu yake mpya ya Usikate Tamaa, ambayo anaamini itamng'arisha katika tamasha hilo.Msama alizitaja nyimbo zilizomo kwenye albamu hiyo ya Usikate Tamaa kuwa ni Usikate Tamaa, Mungu Wangu Nitetee, Niko na Yesu, Mke Si Nguo, Moyo Tukuza Bwana, Chunga Ahadi Yako na Yesu Jina Zuri.Mukubwa kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), anayeishi Kenya, amewahi kutoa albamu mbili ambazo ni Sijaona Rafiki na Mungu Mwenye Nguvu.Sijaona Rafiki Kama Yesu ambayo ni albamu yake ya kwanza ina nyimbo za Uwe Nami Bwana, Sijaona Rafiki Kama Yesu, Nitayainua Macho, Matendo ya Mungu, Bwana Wastahili na Yesu Kimbilio.Albamu yake ya pili ya Mungu Mwenye Nguvu ina nyimbo za Mungu Mwenye Nguvu, Mkono wa Bwana, Mfalme wa Amani, Siku Moja, Tabia Ina Dawa na Roho Yangu Ikuimbie.Mbali na Mukubwa, wengine waliothibitisha kushiriki tamasha hilo litakalofanyika Sikukuu ya Pasaka ni Rose Muhando, Anastazia Mukabwa, Upendo Nkone, Upendo Kilahiro, Christina Shusho, Atosha Kissava, Mwinjilisti Faraja Ntaboba kutoka DRC na kundi la Glorious Celebration.Pia kwaya mahiri ya Kinondoni Revival inayotamba na albamu yao mpya ya Mtu wa Nne, inatarajia kutumbuiza katika tamasha la Pasaka.Nyimbo zilizomo kwenye albamu hiyo ni Mtu wa Nne, Imekwisha, Chukua Hatua, Mtafuteni Bwana, New Season, Hakikisha, Ninakushukuru na Dini Iliyo Safi.Pia kwaya hiyo ya Kinondoni Revival imewahi kutamba na albamu yao ya Kilio cha Mcha Mungu yenye nyimbo nane za Kilio cha Mcha Mungu, Kwanini Unataka Kujiua, Ayubu II, Vumilia Kidogo, Nafsi Yangu, Natamani Kwenda Mbinguni, Ndugu Yetu Twakutafuta na Twalilia Tanzania ambazo pia wameahidi wataziimba.Msama alisema baada ya waimbaji hao kutikisa Uwanja wa Taifa, mashambulizi mengine yatahamia kwenye Uwanja wa Jamhuri, Dodoma Aprili 9 mwaka huu.Tamasha la mwaka huu malengo yake makubwa ni kuchangisha fedha kwa ajili ya kuwasomesha watoto yatima na kuwasaidia mitaji wanawake wajane.Kiingilio katika tamasha hilo kimetengwa katika kategoria tatu na kitakuwa sh. 2,000 kwa watoto, sh. 5,000 kwa viti vya kawaida na viti maalumu sh. 10,000.Tamasha la Pasaka la mwaka huu pia litashirikisha waimbaji wa nyimbo za Injili kutoka nchi za Uganda, Rwanda, Afrika Kusini na Zambia. Pia kutakuwa na kwaya na vikundi vya burudani.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...