Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Thursday, March 15, 2012

KIEV,
Ukraine
BINGWA wa uzani wa juu
unaotambuliwa na Chama cha Ngumi za Kulipwa Duniani (WBC), Vitali Klitschko
amesema hana mpango wa kuwa bondia mwenye umri mkubwa kushikilia ubingwa huo na
badala yake, amepanga kujikita kwenye ulingo wa siasa nchini Ukraine.
Shirika
la Habri la Marekani (AP), lilimnukuu bondia huyo juzi alipohojiwa kwamba
ataendelea kuzichapa kwa muda gani.
Akijibu swali hilo, bondia huyo mwenye
umri wa miaka 40 alisema haitakuwa muda mrefu na badala yake, atajikita kwenye
siasa kutokana na kwamba nchini Ukraine kuna nafasi nyingi.
Mwaka 1994 bondia
George Foreman, ndiye aliyeweka rekodi ya kuwa bondia wa kwanza kutwaa ubingwa
huo, akiwa na umri mkubwa wa miaka 45 na Klitschko, alisema kwa ujumla hataki
kuvunja rekodi hiyo ya Foreman.
Kwa sasa Klitschko ndiye kiongozi wa chama
cha upinzani kiitwacho 'Udar' (mgomo) na anataka kuwa meya wa mji wa Kiev nafasi
ambayo aliikosa mwaka 2006, wakati alipowania kwa kauli mbiu ya kupiga vita
rushwa ambapo amepania kuwa tena katika uchaguzi ambao utafanyika baadaye mwaka
huu.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...