Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Monday, March 26, 2012

KAMPUNI YA TIGO YATOA MSAADA WA BAISKEL KWA WATU WENYE ULEMAVU MKOA WA ARUSHA


Taarifa kwa vyombo vya habari

Tigo yapeleka mpango wa kijasiriamali kwa watu wanaoishi na ulemavu Arusha

24 march, 2012, Arusha. Tigo imekamilisha msaada wa baiskeli za watu wenye ulemavu kwa kikundi cha watu wanaoishi na ulemavu Arusha ikiwa kama sehemu ya kudumisha ushirikiano wao na vikundi vya kijasiriamali vya watu wanaoishi na ulemavu. Hii ni juhudi ya pamoja ya kuboresha maisha ya watu wenye ulemavu kwa kuwapatia nafasi ya kuanzisha biashara zao wenyewe.

“Tunafuraha kupata nafasi ya kutoa mafunzo na kushirikina na jamii ya watu wanaoishi na ulemavu. Alisema bwana Joseph James, Meneja wa Tigo kanda ya kaskazini.“Mafunzo haya yamekuwa yakitolewa ili kuwawezesha kupata ujuzi wa kijasiriamali, na kuweza kutambua na kutumia nafasi zilizopo ili kujiendeleza kiuchumi na kijamii”.

Hafla hiyo ya makabidhiano imefanyika leo katika viwanja vya Makumbusho ya Azimio la Arusha, na baiskeli hizo zilikabidhiwa kwa niaba ya Tigo na bwana Joseph James na kupokelewa na Meya wa mkoa wa Arusha mheshimiwa Gaudance Lyimo kwa niaba ya chama cha watu wanaoishi na ulemavu (CHAWATA)

“Tunajivunia kuwa sehemu ya mpango huu” alisema mh. Gaudance Lyimo. “watu wengi wamekuwa na ndoto za kuanzisha biashara zao wenyewe, lakini siyo wote ambao wanapata vifaa na mafunzo kuwezesha ndoto zao kutimia. Ni kitu cha kufurahisha kuona kampuni kama ya Tigo kuwa wawezeshaji kwa kutoa vifaa kwa wajasiriamali wanaoishi na ulemavu ” alisema.

Kupitia programu ya mafunzo ya kijasiriamali, Tigo imewapatia wanachama hao simu za mkononi,kadi za simu pamoja na mafunzo ya huduma za Tigo, Tigo pesa na Tigo Rusha. Hii itasaidia kupanua nafasi za kibiashara kwa watu wenye ulemavu na kuongeza kipato chao.

Huu ni mzunguko wa mwisho kwa kampuni ya Tigo kutoa msaada wa baiskeli za walemavuwa ambapo tayari imeshatoa baiskeli 26 katika mkoa wa Dar es salaam mwanzoni mwa mwezi huu na nyingine 9 huko Dodoma mwishoni wa wiki iliyopita.

Kuhusu Tigo:

Tigo ni mtandao wa kwanza wa simu za mkononi Tanzania, ilianzishwa mwaka 1994, ni mtandao wa simu unaongoza kwa ubunifu wa hali ya juu na ni wa bei nafuu kupita zote nchini. Tigo ni sehemu ya MillicomInternational Cellular S.A (MIC) na hutoa huduma za simu za mkononi kwa gharama nafuu na inapatikana maeneo mengi kiurahisi kwa wateja zaidi ya milioni 30 katika masoko 13 yaliyoko Afrika na Amerika ya Kusini.

Msingi wa mafanikio ya Tigo ni uzingatiaji wa mikakati mitatu ambayo ni Gharama nafuu, Uwepo na Upatikanaji .Tunajenga dunia ambapo huduma za simu ni za bei nafuu, zipo na zinapatikana kila mahali na kwa wote. Hii inahakikisha kwamba wateja wetu wanapata huduma bora zaidi kwa bei nafuu kuliko zote katika mikoa yetu 26, Tanzania Bara na Zanzibar.

Kwa taarifa zaidi tembelea: www.tigo.co.tz

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...