Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Saturday, March 31, 2012

WANAFUNZI WA SHAHADA YA KWANZA YA SOSHOLOJIA CHUO KIKUU CHA DODOMA (UDOM) WALIVYOSHIRIKI BONANZA LILILOFANYIKA MWISHONI MWA WIKI ILIYOPITA NDANI YA UD


Hiki ndio Kikosi cha Wanafunzi wa Mwaka wa 2 wanaosomea shahada ya Kwanza ya Sosholojia ya Chuo Kikuu Cha Dodoma(UDOM) ambacho Kilipambana na Kikosi Cha Mwaka wa 3 ambao wanasomea Shahada ya Kwanza ya Sosholojia ya Chuo Kikuu Cha Dodoma Katika Bonanza lililofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita.
Hiki ndio Kikosi Cha timu ya Wanafunzi wa Mwaka wa 3 wanaosomea Shahada ya Kwanza ya Sosholojia ya Chuo Kikuu Cha Dodoma Wakiwa katika Dua kabla ya mechi dhidi ya wanafunzi wa kozi hiyo katika bonanza lililofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita Chuoni hapo
Baadhi ya Wachezaji wa Mwaka wa 3 wakiwa katika picha ya pamoja na wanadarasa wenzao kabla ya mechi kuanza
Mlinda Mlango Wa Mwaka Wa 3 Sosholoji Josephat Lukaza akijitahidi kuokoa mkwaju wa Penati Bila mafanikio.
Wanafunzi wa Mwaka wa 2 wakishangilia Mara baada ya Kuibuka kidedea kwa mikwaju ya Penati Dhidi ya Wanafunzi wa Mwaka wa 3.
Mwenyekiti Wa Jumuiya ya Wanafunzi wanaosoma Sosholoji Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOMSSO) Mh Emmanuel Misungwi akiongea na Wachezaji wa netball wa pande zote 2 za Mwaka wa 2 na 3 kabla ya kufungua rasmi Mechi hiyo katika bonanza lililofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita Chuoni hapo.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanafunzi wanaosoma Shahada ya Kwanza ya Sosholojia ya Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOMSSO) Mh Emmanuel Misungwi akifungua rasmi mechi ya netball kati ya Wanafunzi wa Mwaka wa 2 na mwaka wa 3 katika bonanza lililofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita Chuoni Hapo
Mchezaji wa Mwaka wa 3 akidaka mpira wakati wa mechi hiyo dhidi ya wanafunzi wa mwaka wa 2 wa Shahada ya Kwanza ya Sosholojia ya Chuo Kikuu Cha Dodoma katika bonanza lililofanyika Mwishoni mwa Wiki iliyopita Chuoni Hapo


Pichani juu ni Baadhi ya Wanafunzi wa Mwaka wa 2 na wa 3 wakifuatilia Kwa makini mechi ya Netball katika ya Wanafunzi wa Mwaka 2 na 3 katika bonanza lililofanyika Mwishoni mwa Wiki iliyopita Chuoni hapo
Wanafunzi wa Mwaka wa 2 Sosholoji wakiwa busy na kusoma gazeti huku mechi kati ya Mwaka wa 2 na wa 3 ikiendelea.

Baada ya Mechi ya Mpira wa Miguu kati ya Wanafunzi wa Mwaka wa 2 na wa 3 Wanafunzi wa Kike wa Mwaka 2 na wa 3 waliingia katika mashindano ya Kukimbia

Mwanafunzi wa Mwaka wa 2 anayesoma Shahada ya kwanza ya Sosholojia Rachel Akishindana kupiga danadana na Mwanafunzi wa mwaka wa 3 katika bonanza lililofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita chuoni hapo.
Mdada Lelya Akipiga danadana wakati akishindana na Mwanadada wa mwaka wa 2 Rachel pichani juu.


Wanafunzi wanaosoma Shahada ya Kwanza ya Sosholojia ya Chuo Kikuu Cha Dodoma kuanzia Mwaka wa Kwanza hadi wa tatu wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya michezo yote kumalizika katika bonanza hilo lilolofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita chuoni hapo.Picha na Josephat Lukaza Wa http://josephatlukaza.blogspot.com

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...