Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Tuesday, March 20, 2012

kampuni ya Tigo yagawa baiskeli za walemavu Dodoma


Tigo yaendelea kuwaezesha watu wanoishi na ulemavu



17 Machi, 2012, Dar es Salaam. Tigo imetoa baiskeli tisa zaidi kwa chama cha watu wanoishi na ulemavu Dodoma kama muendelezo wa ushirikiano kwa chama cha wajasiriamali wanaoishi na ulemavu. Huu ni mpango shirikishi wakuboresha kiwango cha maisha kwa kutoa fursa za kuanzisha biashara zao binafsi.

Tunaamini kuwa uraisishaji wa kutoka sehemu moja kwenda nyingine , uwezo wa kufanya kazi katika mazingira ya aina yoyote na kipato cha uhakika ni kitu muhimu sana kwenye maisha ya kila siku ya binadamu” alisema Fadhila Saidi Meneja wa Tigo Mkoa wa Dodoma . “ Huu ni mpango muhimu kwetu, kwani inaonyesha wazi wajibu na nia yetu yakuboresha maisha ya watu “ alisema .

Makabidhiano yamefanyika leo manispaa ya Dodoma na baisekeli zilikabidhiwa na bi. Fadhila Saidi kwa niaba ya Tigo. Meya wa manispaa ya Dodoma bwana Emmanuel Mwiliko alizipokea kwa niaba ya Chama Cha Wajasiriamali wanoishi na ulemavu.

Tungependa kuunda dunia ambayo watu wanaoishi na ulemavu wanawezeshwa kibiashara “ alisema Bw. Emmanuel Mwiliko.” Hii haita waongezea udhubutu peke yake, bali itawabadilisha kuwa wanajamii ambao wanachangia kwenye uchumi wa nchi “ alisema .

Kupita mafunzo ya ujasiriamali , Tigo imewapa wanachama wa hichi kikundi , simu za mikononi, lain za simu na mafunzo kuhusu huduma za Tigo , hususan Tigo Pesa na Tigo Rusha. Hii itasaidia kupanua wigo ya biashara zao na kuinua uwezo wa kuzalisha .

Hii ni awamu ya pili ya msaada uliotolewa na kampuni mwezi huu. Tigo imeshatoa baisekeli 26 Dar es salaam na inatarajia kutoa nyingine 15 arusha hivi karibuni.

Kuhusu Tigo:

Tigo ni mtandao wa simu za mkononi ya kwanza Tanzania, ilianza biashara mwaka 1994 na ni mtandao wa simu Tanzania wenye ubunifu wa hali ya juu na bei nafuu kupita zote nchini. Tigo ni sehemu ya MillicomInternational Cellular S.A (MIC) na hutoa huduma za simu za mkononi kwa gharama nafuu na inayopatikana maeneo mengi kiurahisi kwa wateja zaidi ya milioni 30 katika masoko 13 yanaoibuka Afrika na Amerika ya Kusini.

Msingi wa mafanikio ya Tigo ni uzingatiaji wa mikakati mitatu ambao,ni Gharama nafuu, Uwepo na Upatikanaji .Tunajenga dunia ambapo huduma za simu ni za bei nafuu, zipo na zinapatikana kila mahali na kwa wote. Hii inahakikisha kwamba wateja wetu wanapata huduma bora zaidi kwa bei nafuu kuliko zote katika mikoa yetu 26, Tanzania Bara na Zanzibar.


Kwa taarifa zaidi tembelea: www.tigo.co.tz


No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...