Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Thursday, March 15, 2012

TBF NAYO YASIMAMISHA WACHEZAJI, VIONGOZI


KAMATI ya Utendaji ya
Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania (TBF), imewafungia baadhi ya
wachezaji, viongozi na waamuzi kwa utovu wa nidhamu na ukiukwaji wa taratibu za
mashindano.
Katibu Msaidizi wa
TBF, Michael Maluwe, amesema utovu huo wa nidhamu ulifanywa na wahusika wakati
wa michuano ya Kombe la Taifa, iliyofanyika mwishoni mwa mwaka jana ambapo
Kamati ya Utendaji iliyoketi hivi karibuni jijini Dar es Salaam ilitoa maamuzi
hayo baada ya kikao chake cha kupitia ripoti za michuano mbalimbali
.
Alisema viongozi
watatu wa Mkoa wa Shinyanga Ibrahimu Rushemeza, Henry Kizinja William na Tito
Nyalalu wamefungia mwaka mmoja kwa lugha za kebehi, vitisho na matusi kwa
watendaji wa TBF, pamoja na kulazimisha na kushawishi timu zigomee michuano
katika vikao halali.
"baada ya mechi
viongozi hao walivuruga taratibu za kikao wakishinikiza kulipwa fedha, hivyo
hawataruhusiwa kushiriki au kuongoza timu ndani na nje ya
nchi"Alisema.
Alisema, kamati hiyo
pia ilijadili hali iliyotokea katika uwanja wa Leaders ya Kocha Msaidizi wa Mkoa
wa Mwanza, Amri Mohamed, kutokana na kufanyika vitendo vya utovu wa nidhamu
walipocheza na Unguja.
Alisema pamoja na
Mwanza kugomea mechi ya kusaka mshindi wa tatu kwa wanaume, pia ilikaidi adhabu
iliyopewa na TBF baada ya kuvunja kanuni za michuano hiyo kuhusu usajili wa
wachezaji ambapo waliingiza wachezaji wa timu yao uwanjani wakati wa mchezo wa
fainali huku timu mbili husika katika mchezo huo zikijiandaa
kukaguliwa.
"Kitendo hicho
kiliashiria kuleta vurugu na uharibifu wa amani ya mchezo mbele ya mgeni rasmi,
Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara,
hivyo kuitwa polisi wa ziada kulinda usalama.
Kutokana na vitendo
hivyo, mkoa na viongozi wa Mwanza wamefungiwa mwaka mmoja kushiriki michuano
yoyote itakayoandaliwa na TBF, huku katika kipindi hiki
cha adhabu viongozi hao hawataruhusiwa kushiriki au kuongoza ama kujishulisha
na mpira wa kikapu katika michuano yoyote, kliniki za mpira wa kikapu, michuano
ya shule kitaifa, kushiriki mikutano yoyote ya wadau nchini na nje ya
nchi.
Kama hiyo haitoshi
adhabu hiyo imekwenda pia kwa wachezaji Juma Kisoky, Willison Masanja,
Shilinde Francis, Amon Sembelya Mohamedi Ally, Amri Mohamedi, Kizito
Bahati, Ahmed Said, Adam
Jegame, Bundala, Charles, Chacha Tubet, Shinda Vincent, Enock Charles na Kocha
Robert Mwita.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...