Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Saturday, March 17, 2012

THABEET KATIKA TIMU YA TATU NBA


Hasheem Thabeet katikati na jezi
ya timu yake mpya
MCHEZAJI wa kulipwa wa mpira wa kikapu wa Tanzania, Hasheem
Thabeet amechukuliwa
na klabu ya Portland Trail Blazers inayoshiriki kwenye Ligi
ya Mpira wa Kikapu nchini Marekani (NBA) kutoka klabu ya Houston Rockets.
Kwa mujibu wa taarifa za kwenye mitandao mbalimbali ya
intaneti, Portland Trail Blazers imefanikiwa kumnyakua Mtanzania huyo kutoka
Rockets kwa kubadilishana na mchezaji mwingine Marcus Camby, jana ambayo ilikuwa
siku ya mwisho iliyowekwa na NBA kwa ajili ya
klabu zinazocheza ligi hiyo kufanya utaratibu huo wa
kubadilishana wachezaji.
Mlinzi Jonny Flynn, pia amejiunga na klabu ya Portland
Trail Blazers kama sehemu ya utaratibu huo, Thabeet ambaye sasa amechukuliwa na
Blazers kabla alichukuliwa na Houston Februari mwaka jana, akitokea Memphis na
alifanikiwa kuichezea Rockets mechi tano pekee
katika msimu huu wa ligi.
“Tunatazamia kuwa yale yatakayofanywa na Jonny pamoja na
Thabeet yanaweza kuleta mafanikio katika timu yetu na pia tunamshukuru Marcus
kwa mchango alioutoa kwa kipindi cha misimu mitatu aliyokuwa nasi na tunamtakia
kila la heri huko alikoenda,” alisema Kaimu Meneja Mkuu wa Blazers Chad
Buchanan.
Katika michezo 120 ya misimu mitatu akiwa na klabu za
Memphis na Houston, Thabeet mwenye umri wa miaka 25, ana wastani wa pointi 2.2,
na jumla ya dakika 10.7 pamoja na rebaundi 2.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...