Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, March 14, 2012

Vodacom yachezesha droo ya kwanza ya mwezi kupitia promosheni ya M-Pesa

Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano wa Vodacom Tanzania Rukia Mtingwa (kulia) akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) kabla ya kuchezesha droo ya kwanza ya mwezi kupitia promosheni ya M-pesaili kupata mshindi wa shilingi Milioni kumi, wa pili kulia ni Afisa Masoko wa M-pesa Reenu Verma, na Meneja wa Mifumo ya kompyuta Bw. Patrick Makungu pamoja na mwakilishi wa Bodi ya michezo ya kubahatisha Tanzania bi. Chiku Saleh.
Mwakilishi wa Bodi ya michezo ya kubahatisha Tanzania Chiku Saleh (kushoto) akinukuu namba ya simu ya mshindi wa shilingi milioni kumi aliepatikana katika droo ya kwanza ya mwezi iliyochezeshwa na Kampuni ya simu za mkononi Vodacom Tanzania kupitia promosheni ya M-pesa, wa pili kushoto ni Meneja wa Mifumo ya kompyuta wa kampuni hiyo Bw. Patrick Makungu katikati ni Afisa Masoko wa M-pesa bi. Reenu Verma, anayeshuhudia (kulia) ni Kaimu Mkuu wa kitengo cha Mahusiano wa Vodacom Rukia Mtingwa

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...