Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Friday, March 16, 2012

MABONDIA WA KENYA TANZANIA KUPIMA UZITO KESHO KWA AJILI YA MPAMBANO

BONDIA Gabriel Ochiang kutoka Kenya amewasili Dar es salaam LEO kwa ajili ya mpambano wake utakaofanyika jumapili hii na bondia Ramadhani Shauli wa Tanzania utakaofanyika katika ukumbi wa Frensi kona Manzese jijini.Akizungumza mara baada ya kuwasili nchini leo majira ya saa mbili na nusu asubui kwa basi la Akamba bondia huyo kutoka kenya amesema kuwa kama kawaida yake ajamuona Mtanzania wa kumbabaisha zaidi ya aliyekuwa bingwa wa Mabara bondia Mbwana Matumla kwa sasa sijaona bondia mzuri zaidi yakeMabondia hawo wanatalaji kupima uzito kesho kwa ajili wa mpambano wao wa kirafiki wa kimataifa wa raundi nane Naye bondia Ramadhani Shauli akizungumza kwa njia ya simu amesema kwa sasa angalii anapigana na nani yeye amejidhatiti kuendeleza ubabe kwa bondia yoyote anayepigana nae na kwa kuwa nimepata mpinzani kutoka nje ya nchi hapa ndipo watanzania watakapo kiona kiwango changu cha mchezo wa ngumi kwa sasa hapa nchini akuna bondia wa kuni babaisha kwani karibia wote viwango vyao vidogo ndio mana nimemuomba promota aniletee mtu toka nje ya nchi na nimefurai sana kupangiwa mkenya na nipo fiti kwa ajili ya mpambano huo.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...