Diego Armando Maradona - Kocha aliyetimuliwa klabu ya Al Wasl
DUBAI, Falme za Kiarabu
NGULI wa soka duniani raia wa Argentina,
Diego Maradona amefukuzwa kazi huko Falme za Kiarabu, alikokuwa akiinoa
klabu ya Al Wasl, baada ya miezi 14 ya kufanya kazi hiyo.
Kufukuzwa
kazi kwa Maradona kulitarajiwa tangu Juni, wakati bodi nzima ya klabu
ya Al Wasl ilipojiuzulu, kufuatia hitimisho la msimu usio na taji.
Maradona,
51, alijiunga na Al Wasl ya Dubai Mei 2011 na hadi anafukuzwa ana salio
la mwaka mzima la mkataba ambao kimsingi klabu imeuvunja rasmi.
Nyota
huyo wa zamani wa soka ametimuliwa, baada ya kutoipa mafanikio tarajiwa
Al Wasl, iliyomaliza ligi ikiwa nafasi ya nane kwenye msimamo.
"Kufuatia
majadiliano ya pamoja kati ya Bodi ya Wakurugenzi wa Al Wasl kupitia
nakutathmini benchi la ufundi chini ya kocha Diego Maradona, imeamua
kusitisha kazi ya Maradona na dawati zima la ufundi," ilisomeka taarifa
ya klabu kwenye tovuti yake.
Maradona, mshindi wa Kombe la Dunia akiwa na Argentina
mwaka 1986, alipamba vichwa vya habari huko Falme za Kiarabu hapo Machi
mwaka huu, wakati alipojiingiza katika mabishano na mgogoro na
mashabiki wa timu yake.
Katika
mechi hiyo ambayo Al Wasl ilifungwa mabao 2-0 kwenye Ligi ya Kulipwa ya
Falme za Kiarabu ‘UAE Pro League’ kutoka kwa Al Shabab, alipanda
jukwaani kujaribu kumlinda mke wake, baada ya mashabiki kuonekana
kupanga kuwafanyia vurugu wake na wapenzi wa wachezaji.
Maradona
alichukuliwa ili kufufua heshima ya Al Wasl ndani na nje ya dimba,
lakini ikajikuta ikimaliza pointi 29 nyuma ya mabingwa Al Ain.
No comments:
Post a Comment