Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, July 11, 2012

TIMU YA WATU WENYE ULEMAVU WA NGOZI ALBINO UNITED KUPAMBANA NA WABUNGE JUMAMOSI MJINI DODOMA


Meneja wa Kinywaji cha Grand Malta Consolata Adam akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusu mechi ya kirafiki ya Wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na timu ya watu wenye ulemavu wa ngozi Albino  United utakaofanyika jumamosi mjini Dodoma na kudhaminiwa na TBL kupitia kinywaji chake kisicho na kilevi cha Grand Malta. Kushoto ni Seif Kulate, Said Ndonge na Mohamed Kindunyo.
 
Katibu wa timu ya Albino United, Mohamed Kindunyo akizungumza na waandishi wa habari kuhusu pambano lao na Wabunge litakalofanyika mjini Dodoma siku ya Jumamosi.

NA MWANDISHI WETU
TIMU ya soka inayoundwa na watu wenye ulemavu wa ngozi Albino  Albino United wanatarajia kwenda mkoani Dodoma Ijumaa ambako watakwenda kucheza mechi ya kirafiki na timu ya Wabunge ambao wako mkoani humo kwa shughuli za kibunge.
Akizungumza jana katika Mkutano na waandishi wa Habari uliofanyika katika Ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Katibu wa timu hiyo Said Ndonga amesema wana uhakika kwamba watacheza katika kiwango.

Timu hiyo ambayo katika iliwahi kushiriki katika Ligi ya Shirikisho la Soka nchini TFF  msimu uliopita  na kufika katika ngazi ya Taifa  Wilaya ya Ilala.
Safari na mechi ya Albino United imedhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania  (TBL) kwa kupitia kinywaji chake kisicho na kilevi cha Grand Malta.
Akizungumza katika mkutano huo mdhamini  ambayeni Meneja wa Grand Malta , alisema kwamba watatoa udhamini kwa wachezaji 20 tu kati ya 40 wanaounda timu hiyo ya Albino United kwa kuwasafirisha chakula, malazi na posho.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...