Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, July 11, 2012

VODACOM KUZAWADIA WAANDISHI 10 WA MITANDAO NCHINI


Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Bw. Rene Meza

DAR ES SALAAM, Tanzania      

Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania, itatoa tuzo kwa waandishi bora kumi mahiri katika mitandao ya kijamii kutokana na umahiri wao.

Tuzo zitajulikana kwa jina la 'Tuzo za Umahiri wa Digitali za Vodacom', zitatolewa kwa washindi 10 kutokana na jitihada zao na mafanikio yao, ambazo ni kwa mara ya Kwanza kufanywa na kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom.

Akizungumza na wanahabari, Mkurugenzi mtendaji wa Vodacom Tanzania, Rene Meza amesema kuwa, Waandishi wa mitandao ya kijamii wana mchango mkubwa katika kutoa taarifa mbalimbali ndani ya jamii, na mchango huu unatakiwa kuthaminiwa, ambapo wao kama wadau wameamua kuonesha hilo kwa vitendo.

"Wapo waandishi wengi katika mitandao ya kijamii na wanaandika masuala mbalimbali kuhusu biashara au hata yale yanayogusa jamii moja kwa moja. Ni kwa sababu hii ndio maana tunatambua na kuwapatia tuzo hizi kutokana na mabadiliko waliochangia katika utoaji wa taarifa," alisema Meza.

"Huu ni mchango kutoka Mfuko wa M-pesa ambapo waombaji wataweza kuzitumia katika udhamini na kuendeleza shughuli zao," alisema Meza na kuongeza.

"Tunathamini mchango wa kila mtu, na tunahitaji waandishi wa mitandao ya kijamii wote waendelee kufanya kazi zao nasi tutaendelea kuthamini na kutambua mchango wao na kuwapa tuzo.”

aliongeza kuwa, baadhi ya sifa ambazo zitapewa kipaumbele katika tuzo hizi, pamoja na mambo mengine, ni ubunifu na utoaji wa taarifa za kijamii, Kuzingatia weledi wa uandishi na uhuru wa vyombo vya habari, mahusiano na wasomaji katika utoaji wa taarifa, umahiri wa picha na ushirikishwaji wa vyombo vingingine.

Waandishi wa mitandao ya kijamii watashindanishwa kadri inavyowezekana ili kuwawezesha kuongeza weledi na umahiri katika kazi zao.

Kampuni ya Vodacom Tanzania pia itaanzisha  mfuko wa fedha wa maendeleo ya digitali. Kwa mujibu wa Meza fedha hizi zitatumika katika kuendeleza umahiri na kuboresha kazi katika mitandao ya kijamii na tovuti.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...