Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, July 11, 2012

UZINDUZI WA FILAMU MPYA YA SAYLA



 

Msimamizi wa kampuni ya Dynamic Minds, Angella Karashani akifafanua jambo wakati wa uzinduzi wa filamu mpya ya Salya iliyowashirikisha watu maarufu wakiwemo Wabunge wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania uliofanyika jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni msanii wa Filamu, Wema Sepetu na Wastara  Juma.

Na Khadija kalili

MSANII Wastara Juma akiwa na jopo la wasanii na watu maarufu kutoka katika kada mbalimbali nchini wanatarajia kuzindua filamu yao mpya itakayokwenda kwa jina la Sayla.

Filamu hiyo ambayo imepangwa kuzinduliwa katika mikoa mine ambayo ni Arusha, Morogoro, Dodoma na Dar es Salaam.

Aidha filamu hiyo itazinduliwa Mkoani Dodoma ambako inatarajiwa Wabunge wanaondelea na bunge la Bajeti nchini watahudhuria.

Wastara aliongeza kwa kuwataja baadhi ya wasanii na watu mashuhuri waliocheza filamu hiyo ni pamoja na msanii nyota nchini wa kike nchini Wema Sepetu, huku baadhi ya watu mashuhuri ni pamoja na Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki Shyrose Bhanji.

Wabunge wengine ni Ester Bulaya (Viti Maalum CCM), Halima Mdee na Zitto Kabwe (CHADEMA), watangazaji maarufu ni pamoja na Maimatha Jesse, Ephraim Kibonde na wengineo wengi.
Katika filamu hiyo Wastara nayeye amecheza huku mhusika mkuu ni Angela Karashani , filamu hiyo imeandaliwa na Kampuni ya Dynamic Minds.

Wastara ambaye ni mke wa muigizaji  Juma Kilowoko ‘Sajuki’ amewashkuru Watanzania kwa msaaada wao wa hali na mali na kuwataka wamuunge mkono katika  ununuzi wa filamu hiyo ambayo mapato yake yatakwenda katika kumsadia Sajuki na familia yake kwa ujumla

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...