Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Sunday, July 8, 2012

TIMU YA TANZANIA YAENDA LONDON KATIKA MICHEZO YA OLIMPIKI


 Wachezaji wakiwa tayari kwa safari ya kuelekea London, Uingereza katika michezo ya Olimpiki.
 Wachezaji wa timu ya Tanzania inayokwenda kushiriki michezo ya Olimpiki wakiwa katika picha ya pamoja muda mfupi kabla ya kuondoka majira ya saa kumi jioni kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kwenda London, Uingereza. Picha na Habari Mseto Blog
 Muogeleaji wa mita 100 wa Tanzania Magdalena Moshi akiwa na kaka yake (kushoto) katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere muda mfupi kabla ya kuelekea London, Uingereza katika michezo ya Olimpiki.
Kocha wa Riadhaa, Zakaria Ngwandu muda mfupoi kabla ya kuondoka
Mkurugenzi wa Michezo Tanzania, Leonard Thadeo, akiwaasa wachezaji kujituma katika michezo hiyo huku akisisitza kuwa na nidhamu kwa muda wote wa kambi na mashindano

DAR ES SALAAM, Tanzania

TIMU ya Tanzania inayokwenda kushiriki michezo ya Olimpiki imeondoka leo kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kwenda London, Uingereza, huku ikiwa na matumaini ya kurudi na medali.

Timu hiyo ya Tanzania yenye wanamichezo sita ambao ni wa Kuogelea, Ngumi za Riadhaa na Riadha imeondoka jana majira ya jioni kushiriki michuano hiyo inayoanza Julai 27 hadi Agosti 12 mwaka huu, yakishirikisha nchi 205.

Akizungumza muda mfupi kabla ya kupanda ndege, mmoja wa wachezaji hao, bondia wa ngumi za ridhaa, Seleman Kidunda, amejinasibu kufanya maandalizi ya kutosha kumuwezesha kurudi na medali, ingawa pia aliomba dua za Watanzania.

“Naenda kulipigania taifa kuhamasisha mabondia ambao wanadhani kuwa Tanzania haiwezi. Lengo ni kuitangaza nchi na Afrika, hasa ukizingatia kuwa haya ni mashindano makubwa duniani. Muhimu kwa Watanzania kutuombea dua,” alisema Kidunda.

Kwa upande wake, Kocha wa ngumi, Mrakibu wa Magereza, (SP), Remmy Ngabo, alisema amempa Kidunda mazoezi ya kutosha na anaamini yatamsaidia kwenye mashindano hayo yanayoanza kuanza




Mwanariadha wa Marathon, Zakia Mrisho alisema kwa upande wake anaenda London kwa nia moja tu ya kurudi na ushindi na kwamba hakutakuwa na kisingizo cha maandalizi, kwania amefanya ya kutosha kumpa medali.
Aidha akizungumza wakati wa kuiaga timu hiyo, Mkurugenzi wa Michezo Tanzania, Leonard Thadeo, amewaasa wachezaji hao kujituma katika michezo hiyo huku akisisitza kuwa na nidhamu kwa muda wote wa kambi na wa mashindano.

Aliongeza kuwa, mashindano hayo yatakuwa na ushindani mkubwa, hivyo wanapaswa kujituma zaidi ili waweze kurejea na medali.

Wanamichezo waliondoka jana ni Zakia Mrisho, ambaye ni mwanariadha anayekimbia mita 5000, Selemani Kidunda ngumi za Ridhaa, Samson Ramadhan, Riadha, Msenduki
Mohmed na Faustine Mussa ambaye anakimbia marathon.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...