Naibu
Balozi wa Tanzania, London, Mheshimiwa Chabaka Kilumanga (pili
kushoto), akiwapokea rasmi Wanamichezo wa Tanzania, watakao wakilisha
Taifa katika Michezo ya Olimpiki leo kabla ya kufanya mazungumzo mafupi
na Rais wa Jamhuri ya Muungano, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete,
katika Hotel ya Churchill, jijini London, Uingereza.
Rais
wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, Mama Salma Kikwete,
Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Mheshimiwa Peter Kallaghe (mbele
Kulia), Mkuu wa Msafara, Bwana Hassan Jarufu (mbele kushoto),
wakifanya mazungumzo na Wanamichezo wa Tanzania katika Michezo ya
Olimpiki, itakayofanyia nchini Uingereza mwaka huu 2012.
Timu
ya Tanzania itakayoiwakilisha nchi katika michezo ya Olimpiki,
itakayofanyika nchini Uingereza, leo wamepata nafasi ya kukutana na
kufanya mazungumzo mafupi na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania,Dk. Jakaya Mrisho Kikwete, katika Hotel ya Churchill, mjini
London, Uingereza.
Mheshimiwa
Rais Kikwete, aliwapa Baraka za Watanzania na kuwaomba wajitahidi na
kuliwakilisha vyema Taifa na kurudisha jina la Tanzania katika ramani
ya michezo kama ilivyokuwa siku za nyuma.
Wanamichezo hao ambao wataliwakilisha Taifa, wameweka kambi yao katika Chuo Kikuu cha Bradford (Bradford University), katika mji wa Bradford, kabla ya kuhamia rasmi kwenye kijiji cha michezo hiyo (Olympic Village) tarehe 24 July, tayari kabisa kwa kuanza ushiriki wao katika mashindao hayo ya Olimpiki.
No comments:
Post a Comment