Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, July 11, 2012

SHINDANO LA MISS UTALII KAGERA KUFANYIKA JUMAMOSI 14-7-2012



Shindano la kumsaka Miss Utalii mkoa wa Kagera 2012, litafanyika katika ukumbi wa Linas Club mjini Bukoba, siku ya tarehe 14-7-2012 kuanzia saa, mbili usiku.

Katika shindano hilo jumla ya Warembo 15 watapanda jukwaani kuchuana kuwania taji la miss Utalii Tanzania 2012- Kagera, ambapo watapita jukwaani katika mavazi ya kitanzania ya Ubunifu, kitalii, kutokea na ya asili, huku wakitangaza Utalii, Utamaduni, urembo wa kitalii, ubunifu na vipaji vya kuimba na kucheza nyimbo na ngoma za asili za makabila ya mkoa wa Kagera na Tanzania kwa ujumla.  

Pia shindano hilo litasindikizwa na burudani mbalimbali za Ngoma za asili, muziki wa dansi kutoka kwa bendi ya Diamond Musica na wasanii wa muziki wa kizazi kipya, Agcox Burchaman kutoka Uganda, Maua na BK Sunday. 

Aidha shindano hilo limedhaminiwa na Cargo Star, Vodacom Tanzania, Kroyera Tours,Vission Radio, Kasibante Radio, Prins Hotel, Paradise Hotel, Linas Club , Mice and Lovely Salon, misstourismorganisation.blogspot.com na Amazing Tanzania Tours (Tours and Safaris) na mtandao wa www.sufianimafoto.blogspot.com.

Washindi wa shindano hilo watawakilisha mkoa wa Kagera katika fainali za miss Utalii Tanzania 2012- Kanda ya Magharibi, na baadae katika fainali za taifa za Miss Utalii Tanzania 2012 zitakazofanyika siku ya mkesha wa Uhuru wa Tanzania 8-12-2012.

Miss Tourism Tanzania  Symbol Of National Heritage - Do Value Added Pageant
"Lets Visit & Promote Tanzania National Parks -Tourism is Life ,Culture is Lining"

Mawasiliano zaidi:
Hotline: + 255 - 715/754/773 - 318 278.
www.misstourismorganisation.blogspot.com
www.facebook.com/missutaliitanzania

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...