Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Friday, August 31, 2012

KOCHA WA KIMATAIFA WA MASUMBWI SUPER D ATEMBELEA KAMBI YA TIMU YA TAIFA


Kocha wa Kimataifa wa Mchezo wa Masumbwi Rajabu Mhamila 'Super D' aliechuchumaa akiwa katika picha ya pamoja na mabondia wa Timu ya Taifa pamoja na Makocha wa timu hiyo alipotembelea mazoezi ya timu hiyo yanayoendelea katika GYM ya Gymkhana  kushoto ni Selemani Kidunda aliekuwa akituwakilisha katika mashindano ya Olimpic 2012 yaliyomalizika hivi karibuni wachezaji hawo kwa sasa wanajiandaa na mashindano ya Taifa yatakayoanza September 15 katika uwanja wa Ndani wa Taifa .Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Kocha wa Kimataifa wa Mchezo wa Masumbwi Rajabu Mhamila 'Super D' katikati akiwa katika picha ya pamoja na mabondia wa timu ya taifa na makocha wenzake alipotembelea mazoezi ya timu hiyo yanayoendelea katika GYM ya Gymkhana.Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
Kocha wa Kimataifa wa Mchezo wa Masumbwi Rajabu Mhamila 'Super D'  wa pili kulia akiwa katika picha ya pamoja na mabondia wa timu ya taifa na makocha wenzake alipotembelea mazoezi ya timu hiyo yanayoendelea katika GYM ya Gymkhana.Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

MZEE YUSSUF AFUNGUA KAMPUNI YA USAMBAZAJI WA KAZI ZAKE

Meneja Mauzo wa Kampuni ya  Usambazaji ya MY CollectionMUSSA MSUBA akiwa katika duka la mauzo ya kazi za Jahazi
MSANII WA MZIKI WA TAARABU,MZEE YUSUFU KUSHOTO AKIANGALIA MOJA YA KAZI YAKE ILIYOKUWA FEKI ZILIZOKAMATWA NA WASANII WENYEWE KWA KUSHIRIKIANA NA KAMPUNI YA STEPS ENTANTAINMENT YA JIJINI DAR ES SALAAM
DVD ZA JAHAZI
MUSSA MSUBA

Na Mwandishi Wetu

MSANII wa mziki wa Taarabu nchini Mzee Yussuf ameamua kufungua kampuni yake ya usambazaji ijulikanayo kama MY Collection kwa ajili ya kusambaza kazi zake

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi Meneja Mauzo wa Kampuni hiyo Mussa Msuba amesema wameamua kufungua duka kwa ajili ya kuuza CD NA DVD za bendi ya Jahazi inayongozwa na Mzee Yussuf duka hilo lililopo makutano ya barabara ya likoma na Muhonda

linalojihusisha na huzwaji wa DVD za taarabu kwa jumla na rejareja kwa ajili ya kuwaweka karibu wapenzi wake ili waweze kupata burudani kupitia nyimbo zao kwa kuwaburudisha wakiwa majumbani

Msuba amesema kuwa Mzee yusufu yupo mbioni kutoa albamu yake ya mduara itakayokuwa hivi karibuni ambayo ni yake binafsi mbali na hilo bendi hiyo itatoa video yake ya Live za albamu zake zote za Two in One,Kazi ya Mungu, Nakula ka Naksh Naksh,tupendane,Daktari wa Mapenzi

Ambazo zitakuwa madukani kwa ajili ya kuwapa wapenzi wao burudani wakiwa majumbani mwao

Nae Mzee Yussuf aliongeza kwa kusema ameanzisha Kampuni yake binafsi baada ya kuona kwamba kazi zake nyingi zimekuwa zikichakachuliwa kutokana na kuwepo kwa wizi wa kazi za Sanaa

Kampuni yake imekuwa ikisambaza kazi zake kwa ajili ya kuogopa kuibiwa kutokana na wimbi wa kazi za wasanii nchini

Duka lililopo mtaa wa Muhonda na Likoma kwa ajili ya CD za Jahazi pekee  mbali na duka hilo mzee Yusufu anamiliki Duka lingine la Nguo lililopo Magomeni Mapipa kwa ajili ya kujiongezea kipato chake mbali na bendi yake

Bendi ya Jahazi mpaka sasa imekwisha toa albam nane ambazo zipo madukani zinauzwa kwa ajili ya watu wotekupata burudani wakiwa majumbani mwao

Kwa sasa bendi hiyo ipo mbioni kuachia albamu yake ya tisa ambayo aijapewa jina inatarajiwa kuzinduliwa mwezo October kwa ajili ya kutoa burudani kwa wapenzi wao na kuwataka mashabiki wao kuja kuangalia na kusikiliza nyimbo mpya popote pale wanapotoa burudani zao katika kumbi mbalimbali za jijini Dar es salaam


DUKA LA MZEE YUSSUF LILILOPO KATIKA MAKUTANO YA MTAA YA LIKOMA NA MUHONDA LINALOSAMBAZA KAZI ZA BENDI YA JAHAZI

WAHANDISI KUADHIMISHA SIKU YAO MWEZI SEPT, JIJINI DAR


Mhandisi Prof. Ninatubu Lema
- Wawataka Watanzania  kutumia Wakandarasi Waliosajiliwa
Na Aron Msigwa – MAELEZO.

Dar es salaam.

Katika kuelekea maadhimisho ya Siku ya Wahandisi nchini Bodi ya Usajili wa Wahandisi nchini imewataka watanzania kutumia huduma za  wakandarasi waliosajiliwa kisheria ili kuepuka kupata maafa na hasara inayotokana na ujenzi hafifu usiokidhi viwango.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam mwenyekiti wa bodi hiyo Prof. Ninatubu Lema amesema  kuwa wakati umefika kwa watanzania kuwaamini wahandisi wa ndani kutokana na kazi nzuri zinazofanyika na  hatua kubwa iliyofikiwa katika utoaji wa huduma bora  za ushauri na ujenzi tofauti na kipindi kilichopita.

Amesema katika kuimarisha  na kuboresha huduma za ushauri na ujenzi  nchini Bodi ya Usajili wa Wahandisi nchini kwa kushirikiana na wadau wengine wa taasisi za kihandisi  pamoja na wale wa Jumuiya ya Kihandisi watakutana jijini Dar es salaam kwa lengo la kuoinyesha jamii kile ambacho wahandisi wa Kitanzania wanaweza kukifanya katika kuleta maendeleo nchini.

Ameeleza kuwa hivi sasa kuna wahandisi wengi wanaofanya shughuli za usimamizi wa miradi mbalimbali ya ujenzi wa miundombinu nchini ikiwemo miradi ya barabara , gesi na shughuli za uchimbaji wa madini pia wapo wahandisi wa kitanzania wanaofanya kazi za ushauri katika mataifa mbalimbali ndani na ne ya bara la Afrika.

‘’Kwa upande wetu Tanzania wakati tunapata uhuru tulikua na wahandisi 2 na sasa wako zaidi ya elfu kumi ,jambo hili ni kubwa kwa sababu mchango wa wahandisi sasa tunauona katika kuleta maendeleo ya taifa maana bila ya kuwa na wahandisi vitu vyote tunavyoviona kama barabara, majengo, na miundombinu mbalimbali haviwezi kuwepo”

Prof. Lema amesema maadhimisho ya Siku ya Wahandisi nchini yanalenga kuwatambua wahandisi na makampuni  na mashirika ya Kihandisi yaliyotoa mchango mikubwa ya kihandisi katika maendeleo ya taifa na kuwahamasiha wahandisi wengine kufanya shughuli zao vizuri zaidi.

Ameongeza  kuwa maadhimisho yataambatana na tuzo mbalimbali zenye lengo la kuwatia Moyo wanafunzi wahitimu kutoka vyuo vikuu na Taasisi za Uhandisi nchini pamoja na taasisi zitakazotia fora kwenye maonyesho ya ufundi pia kuwafanya vijana washawishike kusomea taaluma ya uhandisi.

Kwa upande wake msajili wa Bodi ya Usajili wa wahandisi Eng. Steven Mlote akizungumzia kuhusu ubora wa majengo yanayoendelea kujengwa kwa wingi jijini Dar es salaam amesema kuwa wamiliki wa majengo hayo wanao mchango mkubwa katika kuhakikisha kuwa ujenzi wa majengo yao unazingatia viwango.

Amesema yeye kama msajili anawashauri wamiliki wa majengo kuhakikisha kuwa majengo yao yanayojengwa hivi sasa yanajengwa na wahandisi waliosajiliwa huku akitoa tahadhali kwa wale wanaokiuka kanuni zilizowekwa katika kusimamia ujenzi wa majengo nchini.

“Nawaomba wamiliki wote kuhakikisha kuwa pindi wanapoanza ujenzi wa majengo yao wahakikishe kuwa wanawatumia makandarasi waliosajiliwa, na mtu yeyote anayeruhusu jingo lake kujengwa na watu au kandarasi zisizosajiliwa anakiuka sheria na anastahili kushtakiwa” amebainisha Mlote.

Kwa upande wake Eng. Benedict. Mukama amewataka wananchi kutoa ushirikiano katika kuyabaini majengo yote yanayojengwa nchini chini ya viwango na kutoa taarifa kwa mamlaka husika ili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi ya makandarasi wanaohusika na ujenzi wa miradi hiyo huku akieleza kuwa katika mwaka wa fedha 2011/2012 zaidi ya miradi 164 iliyokuwa inajengwa kinyume cha utaratibu bila kuzingatia viwango ikiwemo ya barabara imesimamishwa.

Aidha amesema maadhimisho haya ya siku ya wahandisi 2012 ambayo yanaadhimishwa nchini kwa mara ya 10 yatakuwa na mvuto wa pekee kwa kuwa yanawawahusisha washiriki kutoka kutoka nchi za Maziwa Makuu,Afrika ya Mashariki na zile za Jumuiya ya Maendeleo ya  kusini mwa Afrika (SADC).

Kamanda Aggrey Marealle arudisha fomu ya kugombea Ujumbe wa NEC ya CCM


Mjumbe  wa Mkutano Mkuu wa Taifa wa Chama Cha Mapinduzi, (CCM), na Kamanda wa Vijana Wilaya ya Moshi mjini, Aggrey Marealle (kushoto) akirudisha fomu kwa Katibu wa CCM wilaya ya Moshi mjini, Allu Ismaili ili kugombea Ujumbe wa NEC ya CCM. Hafla hiyo ilifanyika katika Ofisi za CCM Wilaya ya Moshi mjini. (Na Mpiga Picha Wetu)

SERENA APAA, VENUS WILLIAMS AKIAGA US OPEN 2012



NEW YORK, Marekani

Wakati Serena akisonga mbele, ndugu yake na bingwa wa zamani wa US Open, Venus Williams alijikuta akitolewa mashindanoni kwa kukubali kichapo cha 6-2 5-7 7-5 kutoka kwa Angelique Kerber

NYOTA anayeshika nafasi ya nne katika viwango vya ubora wa tenisi duniani, Serena Williams hakupata shida kufuzu raundi ya tatu ya micuano ya Wazi ya Marekani ‘US Open’ baada ya kupata ushindi wa moja kwa moja dhidi ya Mhispania Maria Jose Martinez Sanchez.

Bingwa huyo wa michuano ya Wimbledon na Olimpiki, alitumia muda wa saa moja na dakika 22 (1:22) kuibuka kidedea kwa seti mbili kwa bila za 6-2 6-4 dhidi ya nyota asiyekuwa na kiwango Sanchez.

Wakati nyota huyo akisonga mbele, ndugu yake na bingwa wa zamani wa US Open, Venus Williams alijikuta akitolewa mashindanoni kwa kukubali kichapo cha 6-2 5-7 7-5 kutoka kwa Angelique Kerber.

Nyota namba mbili kwa ubora duniani, Agnieszka Radwanska alilazimika kufanya kazi ya ziada kutoka nyuma na hatimaye kumshinda Mhispania Carla Suarez Navarro kwa 4-6 6-3 6-0.

Kwa upande wake mkali wa mchezo huo raia wa Serbia, Ana Ivanovic aliibuka kidedea na kutinga raundi ya tatu ya michuano hiyo kwa ushindi wa 6-2 6-2 dhidi ya Msweden Sofia Arvidsson.

Katika raundi ya tatu, Ivanovic anatarajia kupata upinmzani mkali kutoka kwa yoso wa miaka 19 Sloane Stephens, yoso aliyeingia katika 50 bora ya wacheza tenisi wanamama, aliyetinga hatua hiyo kwa kumchapa Tatjana Malek wa Ujerumani kwa 5-7 6-4 6-4.

Licha ya kutupwa nje ya mashindano, bingwa mara tano wa Wimbledon Venus alisema; "Nilijihisi Marekani kwa mara ya kwanza " kutokana na aina ya sapoti aliyooneshwa na kutoka kwa mashabiki wa nyumbani kwenye Uwanja wa Arthur Ashe.

"Hii ni mara ya kwanmza ambayo nimecheza hapa na kuona kundi kubwa la mashabiki likiwa nyuma yangu kama hivi. Nilisubiri uungwaji huu kwa muda mrefu, hatimaye nimeupata ingawa matokeo hayakuwa mazuri," alisema Venus.

"Ilikuwa ya kushangaza sana. Nilijisikia kama niliyeshinda dhahabu. Kiukweli ilimaanisha kitu. Kwa sasa naangalia mbele kuona namna navyoweza kutumia ipasavyo sapoti mara mbili yah ii niktakayopata katika michuano ya mwaka ujao nikiwa bora zaidi."

MKUTANO MKUU WA MWAKA WA WANAHISA WA TBL


 Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kampuni ya Bia Tanzania (TBL),  ambaye pia ni Waziri Mkuu mstaafu, Cleopa Msuya (kulia) akihutubia wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa 39 wa Wanahisa kwenye Hoteli ya Kilimanjaro Hyatt Regency, Dar es Salaam jana.

 Mwanahisa wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Mchiwa Chedego akiuliza swali wakati wa Mkutano Mkuu wa 39 wa Wanahisa kwenye Hoteli ya Kilimanjaro Hyatt Regency, Dar es Salaam jana.

Mwanahisa Arphaxar Masambu akichangia hoja wakati wa mkutano huo.

 Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kampuni ya Bia Tanzania (TBL),  ambaye pia ni Waziri Mkuu mstaafu, Cleopa Msuya (kulia) akifafanua jambo wakati wa Mkutano Mkuu wa 39 wa Wanahisa kwenye Hoteli ya Kilimanjaro Hyatt Regency, Dar es Salaam jana. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria, Steve Kilindo pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Robin Goetzsche.

 Wanahisa wakiperuzi taarifa ya hesabu za kampuni hiyo kwamaka 2012/13.

                                  Sehemu ya wanahisa wakiwa katika mkutano huo wa mwaka.

                         Baadhi ya wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kampuni hiyo.

 Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa TBL, Steve Kilindo (kushoto) akiteta jambo na Mkurugenzi Mtendaji wake, Robin Goetzsche.

                                           Baadhi ya wanahisa wakiwa katika mkutano huo.

                          Mwanahisa Adrian Makelele akichangia hoja wakati wa mkutano huo.

 Mkurugenzi Mtendaji wa TBL, Robin Goetzsche akijibu maswali ya wanahisa. Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi, Cleopa Msuya.

Bodi ya Wakurugenzi wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) ikiongozwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TBL,  Waziri Mkuu mstaafu, Cleopa Msuya (katikati waliokaa) wakiwa katika picha ya pamoja na wanahisa baada ya Mkutano Mkuu wa Wanahisa wa kampuni hiyo kumalizika jana jijini Dar es Salaam.

SUN CITY MABINGWA SAFARI POOL TEMEKE.


Mkurugenzi wa Klabu ya Kurasin City , Isaac Dirangw (kushoto) akimkabidhi Kikombe  nahodha wa timu ya Sun City, Emmanuel Msengi baada ya kuibuka mabingwa katika fainali za Safari Pool Taifa ngazi ya Mkoa zilizo malizika mwishoni mwa wiki katika klabu ya Kurasini  City,Mkoa wa kimichezo wa Temeke jijin I Dar es Saalaam.Katikati ni Katibu Mkuu wa chama cha Pool Taifa, Amos Kafwinga.


 
Na Michael Machellah
TIMU ya mchezo wa pool ya Sun City,  ilifanikiwa kutwaa ubingwa wa mashindano ya pool ya 'Safari Lager National Pool Championship 2012' baada ya kuibamiza Mpo Afrika 13-7 katika mchezo wa fainali wa mashindano hayo ngazi ya mkoa wa yaliyofanyika katika Klabu ya Kurasini City Mbagala.

Sun City kwa kutwaa ubingwa huo walijinyakulia Kombe na fedha taslim Sh.700,000 na pia kuwa wawakilishi wa mkoa huo katika fainali za taifa zitakazofanyika Septemba mkoani Mwanza kwa kushirikisha timu 16 ambazo zitakuwa mabingwa kwenye mikoa yao.
Mpo Afrika ilikamata nafasi ya pili na kuzawa kitita cha shilingi 350,000  na mshindi wa tatu katika mashindano hayo walikuwa ni wenyeji ambao ni Kurasini City ambao walizawadiwa shilingi 200,000 na wane ni BMK ambao walizawadiwa shilingi 100,000.
Timu shiriki zingine ambazo ni Bashnet,MTN,East London na SupesStar zilipewa kifuta jasho cha shilingi 50,000 kila timu kwa kufikia hatua ya robo fainali katika mashindano hayo kwa Mkoa wa kimichezo wa Temeke.
 
Upande wa mchezaji mmoja mmoja “Singles” (wanaume), Jackso Steven kutoka klabu ya Mpo Afrika alitwaa ubingwa kwa kumchapa Hassan Hussein wa MTN 5-1,na kujinyakulia kitita cha shilingi 350,000 ambapo Hassan Hussei alikamata nafasi ya pili na kuzawadiwa shilingi 200,000, wakati Hassan Abubakari kutoka klabu ya MTN alikamata nafasi ya tatu na kuzawadiwa shilingi 150,000.
Upande wa mchezaji mmoja mmoja “Singles” (wanawake),Beatrice Charles kutoka Klabu ya Mpo Afrika alitwaa Ubingwa kwa kufunga Swaumu Hamisi wa Sun City 5-1, na kuzawadiwa shiloingi 250,000 nafasi ya pili ilichukuliwa na Swaumu Hamisi ambaye alizawadiwa shilingi 150,000 na mshindi wa tatu alikuwa ni Madina Idd  kutoka Klabu ya Kurasini City ambaye alijinyakulia shilingi 100,000
Zawadi kwa washindi wote zilikabidhiwa na Mkurugenzi wa Klabu ya Kurasini City, Isac Dirangw ambaye alikuwa mgeni rasmi katika kilele cha mashindano hayo katika Mkoa wa kimichezo wa Temeke

MBUYU TWITE ALIPOFANYA MAZOEZI YA KWANZA AKIWA NA YANGA DAR


Picha tofauti zikimuonesha beki mpya wa Mabingwa wa Soka wa Kombe la Kagame, Yanga, Mbuyu Twite akijifua na wenzake katika mazoezi ya kujiandaa na Ligi Kuu Tanzania Bara kwenye Uwanja wa Shule ya Sekondari Loyola jijini Dar es Salaam leo.
 Twite akipokea maelekezo kutoka kwa kocha wa Yanga Tom Saintfiet

 Twite akipiga 'push-up' katika mazoezi yake ya kwanza akiwa na Yanga jijini Dar es Salaam yaliyofanyika leo kwenye Uwanja wa Shule ya Sekondari Loyola, Mabibo Dar es Salaam.

RIADHA TAIFA YAIPIGA KUMBO SIMBA VS AZAM NGAO YA JAMII



DAR ES SALAAM, Tanzania

MASHINDANO ya Taifa ya Riadha yanayotarajiwa kufanyika kwenye Uwanja wa Taifa kuanzia Septemba 7 hadi 9, yamelilazimisha Shirikisho la Soka nchini (TFF) kusogeza tena mbele hadi Septemba 11 kwa mechi ya Ngao ya Jamii kati ya Simba na Azam FC itakayofanyika uwanjani hapo.

Akizungumza na waandishi wa habari leo, Ofisa Habari wa TFF, Boniface Wambura alisema kuwa, jaribio lao la kukishawishi Chama cha Riadha (RT) kumaliza kwa wakati mashindano hayo katika siku ya mwisho ili kupisha mechi hiyo hapo Jumapili lilishindwa.

Kutoka na hali hiyo, TFF ilikubali matokeoa na kuamua kuisogeza mechi hiyo kwa mara nyingine hadi Jumanne alasiri, ambapo pambano hilo la kuashiria ufunguzi wa Ligi Kuu ya Vodacom linalohusisha bingwa wa ligi hiyo Simba dhidi ya mshindi wa pili ambayo ni Azam.

“Ligi Kuu sasa itaanza rasmi hapo Septemba 15, siku nne baada ya pambano la Ngao ya Jamii. Kanuni zinataka wiki moja kabla ya ufunguzi kupigwa kwa Ngao ya Jamii, lakini uwapo wa mashindano ya riadha umetulazimisha kufanya hivi. Tuna imani siku nne zitawatosha kujiweka tayari kwa ligi,” alisema Wambura.

Mzunguko wa kwanza wa ligi hiyo utamalizika Novemba 11, ambapo pambano gumzo baina ya mahasimu wa soka la Tanzania, Yanga na Simba zitacheza mechi ya kwanza baina yao hapo Oktoba 3 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Aliongea kuwa, katika mechi za pazia la ufunguzi wa ligi, mabingwa watetezu Simba watacheza na African Lyon kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, huku Polisi Morogoro na Mtibwa Sugar zikitoana ngao huko Jamhuri, Morogoro.

Ratiba hiyo inaonesha kuwa, Wajelajela waliorejea Ligi Kuu msimu huu Tanzania Prisons ya Mbeya siku hiyo itaoneshana ubabe na Yanga huko Sokoine, Mbeya, siku ambayo pia Mgambo JKT na Coastal Union zote za Tanga ziachuana huko Mkwakwani.

Mechi nyingine katika ufunguzi huo ni ile baina ya maafande wa JKT Ruvu na Ruvu Shooting watakaokipiga kwenye dimba la Chamazi Dar es Salaam, Kagera Sugar dhidi ya Azam FC  kwenye nyasi za Kaitaba, Bukoba, huku Toto Africans na Oljoro JKT wakioneshana kazi huko CCM Kirumba, Mwanza.

Ligi hiyo itamalizika Mei 18 mwakani kwa timu zote kujitupa dimbani, ambapo Toto Africans itafunga na Ruvu Shooting CCM Kirumba, Mgambo JKT dhidi ya African Lyon huko Mkwakwani, wakati JKT Ruvu itamaliza na Mtibwa Sugar KWENYE Uwanja wa Chamazi.

Miamba na mahasimu wa soka nchini Simba na Yanga watafunga msimu kwa pambano baina yao kwenye Uwanja wa Taifa, huku Tanzania Prisons itaumana na na Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Sokoine, Oljoro JKT dhidi ya Azam huko Sheikh Amri Abeid na Polisi Morogoro dhidi ya Coastal Union, Uwanja wa Jamhuri.

Aidha, Wambura aliongeza kuwa, endapo wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya klabu barani Afrika, Simba na Azam hazitafanikiwa kuvuka hatua mojawapo ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na Kombe la Shirikisho, ratiba hiyo itafanyiwa marekebisho.

SIMBA, YANGA ZAKOMOANA USAJILI, ZAWEKEANA PINGAMIZI TFF



 Wachezaji wa Simba na Yanga wakisalimiana katika moja ya mechi baina yao

DAR ES SALAAM, Tanzania
WAKATI Kamati ya Sheria, Maadili na Hadhi za Wachezaji ya TFF chini ya Mwenyekiti wake Alex Mgongolwa ikitarajiwa kukutana kesho Jumapili Septemba 2 kupitia pingamizi za usajili kwa wachezaji msimu wa 2012/13, klabu ya Yanga imeiwekea Simba pingamizi mbili.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Ofisa Habari wa TFF, Boniface Wambura alisema kuwa, Yanga inapinga Simba kuwaacha wachezaji Dan Mrwanda, Haruna Shamte, Kanu Mbiyavanga na Lino Masombo.

“Pingamizi la Yanga kwa Simba kuhusu nyota hao ni kuwa, walishapatiwa leseni za kucheza Ligi ya Tanzania walizozitumia kwenye mashindano ya Kombe la Kagame wakiwa na Simba. Pia inapinga Ramadhan Chombo ‘Redondo’ kujiunga Simba kwa vile ana leseni ya kuchezea Azam kwa msimu wa 2012/13,” alisema Wambura.

Pingamizi lingine la Yanga kwa Simba ni kuwa, imezidisha idadi ya wachezaji wa kigeni wanaotakiwa kusajiliwa, kwa maelezo inao nyot wanane wakati wanaoruhusiwa ni watano, ambapo imewataja wachezaji hao kuwa ni Lino Masombo, Felix Sunzu, Emmanuel Okwi, Mussa Mude, Kanu Mbiyavanga, Pascal Ochieng, Komalmbil Keita na Daniel Akuffor.

Wakati yenyewe ikiweka pingamizi hizo kwa Simba, Yanga imewekewa pingamizi mbili Kagera Sugar inayopinga usajili wa beki David Charles Luhende kwa vile ada ya uhamisho haijalipwa, huku Simba nayo ikipinga usajili wa Kelvin Yondani kwa madai ina mkataba naye uliosainiwa Desemba 23, 2011.

Kwa mujibu wa Wambura, jumla ya wachezaji 17 wamewekewa pingamizi za usajili wao kwa klabu za Ligi Kuu, ambapo Simba licha ya kupinga usajili wa Yondani, yenyewe inapingwa kuwasajili Edward Christopher Shija na Samir Said Luhava wa Falcon ya Chakechake, Pemba kwa madai ya kutofuatwa kwa taratibu za uhamisho wao

Azam FC kwa upande wake inapinga usajili wa Ramadhan Chombo ‘Redondo’ kwenda Simba kwa maelezo bado ina mkataba naye unaomalizika Juni 11 mwakani, wakati Simba imewasilisha malalamiko ya mchezo usio wa kiungwana katika usajili wa Mbuyu Twite aliyeko Yanga.

Katika madai yao hayo, Simba inasema Twite alisaini mkataba na klabu yao Agosti 1 mwaka huu mbele ya viongozi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Rwanda (FERWAFA) klabu ya APR, akilipwa dola za Kimarekani 30,000 na nyingine 2,000 ikiwa ni fedha ya kujikimu na nauli yake ya kujiunga na klabu hiyo.

Toto Africans ya Mwanza imewawekea pingamizi wachezaji Enyinna Darlinton aliyeombewa usajili na Kagera Sugar na Mohamed Soud anayekwenda Coastal Union kwa maelezo kuwa bado ina mikataba na wachezaji hao, huku Rollingstone Multipurpose Ateclass Foundation ya Arusha inapinga usajili wa Kigi Makassy.

Rollingstone inataka kulipwa fidia ya kumlea Makassy aliyejiunga Simba akitokea Yanga, kwa kuwa mchezaji huyo bado hajafikisha umri wa miaka 23, kama taratibu za uhamisho na matunzo ya mchezaji zinavyoelekeza.

Aidha, Wambura aliongeza kuwa, Shirikisho la Vyama vya Mpira wa Miguu Uganda (FUFA), limetuma Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) kwa ajili ya mchezaji Ayoub Hassan Isiko aliyejiunga na Mtibwa Sugar akitokea timu ya Bull FC ya nchini humo.

ITC hiyo ilitumwa juzi Agosti 30, hivyo kufanya wachezaji ambao ITC hazijapatikana hadi sasa kubaki wawili tu, huku zikiwa zimesalia siku tatu kufungwa kwa dirisha la usajili wa wachezaji hapo Septemba 4.

Wachezaji ambao ITC zao bado hazijapatikana ni Salum Kinje na Pascal Ochieng kutoka AFC Leopards ya Kenya waliojiunga na Simba.

ITC hizo zinatarajiwa kupatikana wakati wowote kwani tayari TFF limeshaziomba kwa Shirikisho la Mpira wa Miguu Kenya (FKF) baada ya nyaraka zote zilizokuwa zikitakiwa kupatikana.

LIVERPOOL MIKONONI MWA ANZHI MAKHACHKALA EUROPA LEAGUE



 MONACO, Ufaransa

Makhachkala inayopata nguvu ya kutosha kutoka kwa nyota wa zamani wa FC Barcelona, Samuel Eto'o, imejikuta akipangwa na Liverpool katika kundi  A la Europa League, pamoja na timu za Udinese na Young Boys ya Uswisi

WEKUNDU wa Anfield klabu ya Liverpool ya England, imeangukia mikononi mwa kikosi kinachonolewa Guus Hiddink kinachotumia pesa nyingi kusajili na kulipa wachezaji cha Anzhi Makhachkala ya Russia katika mechi za hatua ya makundi ya Europa League.

Makhachkala inayopata nguvu ya kutosha kutoka kwa nyota wa zamani wa FC Barcelona, Samuel Eto'o, Imejikuta akipangwa na Liverpool katika kundi  A la Europa League, pamoja na timu za Udinese na Young Boys ya Uswisi.

Newcastle United pia ya England imerejea katika soka la Ulaya na italazimika kumenyana vema kupenya hatua hii ya makundi ya awali, ambapo imepangwa pamoja na Bordeaux ya Ufaransa, Club Brugge ya Ubelgiji ma Maritimo ya Ureno katika kundi D.

Kwa upande wao Tottenham Hotspur imeangukia kundi J la Europa League, itakopimana ubavu dhidi ya Panthinaikos ya Ugiriki, Lazio ya Italia, na Maribor ya Slovenia.

Ukiondoa kundi A, D na J ya michuano hiyo, makundi mengine katika michuano ya pili kwa ukubwa ngazi ya klabu Ulaya yako kama ifauatavyo: Kundi B linatimu za Atletico Madrid, Hapoel Tel Aviv, Plzen na Academica, huku kundi C likiwa na Marseille, Fenerbahce, M’Gladbach na AEL Limassol.

Kundi E linajumuisha timu za Stuttgart, FC Copenhagen, Steuau Bucuresti na Molde, huku kundi F likiwa na PSV Eindhoven, Napoli, Dnipro na AIK Solna, wakati kundi G kuna Sporting, FC Basel, Genk na Vidoeton. Kundi H kuna Inter Milan, Rubin Kazan, FK Partizan na Neftci.

Lyon, Athletic Club, Sparta Prague na Hapoel Kiryat Shmona zimepangwa kundi F, ambapo kundi K linajumuisha Bayer Leverkusen, FC Metalist Kharkiv, Rosenborg na Rapid Vienna, huku kundi L likiwa na FC Twente, Hannover, Levante na Helsingborgs.

MBUYU TWITE ATUA KUIMARISHA UTANI WA JADI YANGA NA SIMBA


 Beki wa kimataifa wa timu ya Yanga ya Dar es Salaam, Mbuyu Twite, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, jana wakati alipowasili akitokea Rwanda, tayari kwa kujiunga na timu yake ya Yanga baada ya gumzo la muda mrefu na mvutano wa hapa na pale wa Watani wa Jadi Yanga na Simba, ambao kila mmoja alikuwa kijinadi kuwa amemsajili mchezaji huyo huku mmoja akibaki kuambulia manyoya.

Akizungumza na mtandao huu kuhusu kutua nchini huku akiwa ametinga Jezi no 4, yenye jina la Mwenyekiti wa Simba Ismail Rage, beki huyo amesema kuwa yeye ni mchezaji kama walivyo wengine na anatambua kuwa ametua katika timu yenye upinzani mkubwa na mahasimu wao Simba, hivyo yeye ametua kuendeleza Utaji wa Jadi  baina ya timu hizo, na ndiyo maana ameamua kuvaa jezi yenye jina la Rage, ili kuonyesha maana halisi ya  utani huo pamoja na kutokea mtafaruku wa hapa na pale kati ya vilabu hivyo.

Aidha Twite, amesema kuwa ''Namuheshimu sana Rage, na namuomba aniache nifanye kazi niliyotumwa na Baba yangu kama alivyoniamini na kuniruhusu kuja kuitumikia Yanga na kuwarejeshea Faranga yao Simba'' alisema Twite kwa kiswahili kilichopindapinda.

Twite amewataka mashabiki wa Yanga kumuamini na kupuuza yanayoendelea kuenea juu yake kuwa huenda akikosa kuichezea timu hiyo kutokana na kuchanganya madawa na kusema kuwa yeye ni mchezaji halali wa Yanga timu ambayo imefuata taratibu zote zinazotakiwa.

''Ujue hata mimi nilikuwa na wasiwasi japo nilipokea faranga za Rage, kwani hatukufanya vile imefanya Yanga hadi kufikia jana nilipopokelewa na mashabiki wengi wengi wengi sana wa yanga pale kwa uwanja wa Ndege'' alisema Twite.
Mbuyu Twite, akilakiwa na mashabiki lukuki wa Yanga kwenye uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jana.

WA5 WATINGA FAINALI YA SHINDANO LA MISS KANDA YA MASHARIKI TALENT, KUUMANA KESHO MORO


 Warembo wa 5, waliofanikiwa kutinga katika hatua ya Fainali ya shindano la Miss Kanda ya Mashariki, baada ya kuchuana vikali katika shindano lao dogo la Redd's Miss Kanda ya Mashariki Talent, lililofanyika jana usiku kwenye Hoteli ya Usambara, mjini Morogoro. Kutoka (kushoto) ni Mrembo, Joyce Baluhi, Shakhila Hassan, Zuhura Gola, Irene Veda na Salvina Kibona, wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kutangazwa washindi.
 Mrembo, Rose Lucas, akionyesha umahiri wake kwa kushambulia jukwaa ipasavyo kujaribu bahati yake kwa kuwakomvis Majaji, wakati wa shindano hilo.
 Mrembo, Shakhila Hassan, akiimba wimbo wa dini, Ebeneza na kuwapagawisha Majaji na mashabiki waliohudhuria onyesho la mpambano huo jana usiku.
 Mrembo, Joyce Baluhi, akisebeneka na wimbo wa Demu Mwigizaji wa Tunda Man, na kuwakosha vilivyo, Majaji na mashabiki waliohudhuria shindano hilo.
 Mrembo, Irene Thomas, akishambulia jukwaa kwa kucheza Dancehall........
 Mkurugenzi wa Kamati ya Miss Tanzania, Hashim Lundenga (wa pili kushoto) akiwa meza kuu na Miss Tanzania 2010, Geneviv Emmanuel (kulia) na Miss Morogoro 2010, Asha Saleh, wakifuatilia shindano hilo.
 Baadhi ya wadhamini wa shindano hilo, pia walikuwepo kuwakilisha, (kushoto) ni mmoja kati ya wadhamini wa shindano hilo, Kitwe General Traders, ambapo pia wadhamini wengine ni pamoja na mtandano huu wa www.sufianimafoto.blogspot.com, Kampuni ya SPM:- Sufiani Photo Magic, Redd'd, Dodoma Wine, Usambara Safari Lodge, Chilakale Resort, B-Ze Hotel, Clouds Fm, Endepa, Gazeti la Jambo Leo na Simple & Easy Car.
 Sehemu ya mashabiki waliohudhuria shindano hilo.
 Sehemu ya mashabiki waliohudhuria shindano hilo, 'kuona na kunywa kikali'.....
 Washiriki wakicheza wimbo wao wa ufunguzi wa shoo hiyo kwa pamoja.
 Majaji wakishauliana jambo wakati shindano hilo likiendelea..........
 Hapa ni mshiriki, Irene Veda, akijifua kwa kupuliza Sax phone kabla ya kuanza kwa shindano hilo...
 Hapa ni kabla ya kuanza shindano hilo, warembo wakipiga picha ya pamoja kushoo Love.
 Namba za Bahati zilizotinga Tano Bora ...............
Mrembo, Irene Veda, akiimba na kupuliza Sax Phone......
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...